Hizi Harrier 3rd gen zilivyojazana hapa mjini utasema haziuzwi Mil 70+

Hizi Harrier 3rd gen zilivyojazana hapa mjini utasema haziuzwi Mil 70+

Mkuu kwa barabarani mimi amani ya moyo huwa napata nikiwa mkoani. mkoani inabidi uwe na gari yoyote tu ila kwa dar unajihisi mnyonge kwa gari zetu za 15M hizi maana kuna watu wanaendesha michuma ni laana.
Sio mikoa yote mkuu, nenda moshi na arusha bado utaonekana unatembelea kiberiti tu😅😅😅😅
 
Hizo mashine za diagnosis zipo zinazoweza kurudisha hizo mileage nyuma za gari ila ni risk sana maana ni mambo ya kuvuruga control box maana Watanzania wengi wametoka kwenye kuuliza namba gari na zinazotoka Nje ya Nchi wanauliza hiyo mileage na si mwaka wa gari...kwa hiyo wahuni wanacheza na akili zao..
hahhaah duuh! bila kuwasahau na wale wa plate number, kweli wabongo kupigwa wanajitakia
 
Kila la heri mkuu hiyo kwa kipato chako jipe muda zaidi au uza nyumba ununue gari 😂
Unajua mkuu watu tunatofautiana sana, Mimi nataka nijifunze kuweka standard naamini ndani ya Miaka 2 au 3 ijayo hiyo gari ntaipata. Hichi kipindi naendelea kutumia gari ya ofisi na wese bure pamoja service bure, ilimradi sipandi BANCHIKICHA a.k.a Daladala kwenye mizunguko yangu basi naamini ntaipata tu.

Sema gari za ofisi zina masharti uhuru hamna ndio tatizo, unapanda gari isitoke nje ya mkoa labda kwa shughuri za kiofisi ndio shida ilipo.
 
Unajua mkuu watu tunatofautiana sana, Mimi nataka nijifunze kuweka standard naamini ndani ya Miaka 2 au 3 ijayo hiyo gari ntaipata. Hichi kipindi naendelea kutumia gari ya ofisi na na wese bure pamoja service bure, ilimradi sipandi BANCHIKICHA a.k.a Daladala kwenye mizunguko yangu basi naamini ntaipata tu.

Sema gari za ofisi Zina nasharti uhuru hamna ndio tatizo, unapanda gari isitoke nje ya mkoa labda kwa shughuri za kiofisi ndio shida ilipo.
Kwa utaratibu huo utafanikiwa kumiliki hiyo gari mkuu.
 
Saizi watu wana hela mzee mad.

Pongezi kwa mama.


 
Back
Top Bottom