Hizi ndio bei za mbolea ambazo wakulima watanunulia kuanzia Agosti 15, 2022 baada ya bilioni 150

Kwani aliyekapandisha alikuwa nan?
 
kupambana sio tatizo wote tunaunga mkono ila je nani alifikisha bei ya mbolea huko kwenye laki na ushehe?
Bei imepanda kwa sababu ya ugonjwa wa Covid-19 na mgogoro unaondelea kati ya Ukraine na Russia ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji na upatikanaji wa mbolea

Lakini Rais Samia amefanikisha kuleta wawekezaji kwaajili ya kujenga viwanza vya kuzarisha na kusambaza mbolea nchini
 
SIku zote, aliyepita ndiyo hubebeshwa lawama.. HIZO STATEMENT ZA KAMA ILIVYOKUWA AWALI ZIPO KILA PAHALA
 
"Ingeuzwa"......"ingeuzwa"/...."ingeuzwa"......blah blah

Hakuna kitu kama hicho.....
Kiasi kikubwa cha mbolea kinazalishwa nje kwaiyo Rais Samia hana uwezo huo wa kupandisha mbolea

lakini kilichosababisha kupanda kwa mbolea ni ugonjwa wa Covid-19 na mgogoro unaondelea kati ya Ukraine na Russia
 
Wapinzani wa serikali wanaiweza sana kazi ya kutanua magoli, watakuja na sababu nyingine ya kulalamika kwani ni jadi yao siku zote.
 
60 years tunaimba kilimo ni uti wa mgongo!
 
Utashangaa kiukweli hii inaonyesha ni Kwa namna gani serikali inawasikiliza watu wake hasa katika kuhakikisha inawapunguzia makali wakulima kutokana...​
Itakuwa hivi 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220811-125427.png
    114.1 KB · Views: 9
Ndugu zangu hizi zote ni Chenga na pumba tupu wanasiasa uchwara wanaendelea kutuchezesha akili zetu kama mazwazwa hakuna cha bilion wala trilion ni Upuuzi tu wa kushindwa kusimamia mambo ktk taifa,haya sasa huo ndio usanii wa kwenye mbolea na bidhaa nyingine je nini kitafanyika.Watu wakisha piga pesa yao ndio wanaleta ngonjela kuwahadaa watanzania.Ndugu zangu tupambanie katiba tutoke kwenye upumbavu huu unaoendelea ndani ya Tanzania.
 
Misukule ya magufuli lazima itapinga
 
Tahila wewe,nyie wapuuzi kila Jambo mnalaumu na kupinga
 
Bei ni nzuri je wasambazaji katika maduka ya wilayani na agro dealers watanunua tshs.ngapi toka wakala ili nao wafanye biashara au zitapatikana hizo mbolea katika ofisi za vijiji.?
 
Bwanku M Bwanku.

Aina za Mbolea na Bei Zake
Ruzuku inaenda kuwa msaada mkubwa kwa wananchi, hongereni sana serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Wizara ya Kilimo.


1. DAP ingeuzwa Sh 131,676/- bila ruzuku lakini sasa itauzwa Sh 70,000/- ambapo ruzuku ya serikali ni Sh 61,676/-.

2. UREA ingeuzwa Sh 124,734/- bila ruzuku lakini sasa itauzwa Sh 70,000/- ambapo ruzuku ya serikali ni Sh 54,734/-.

3. CAN ingeuzwa Sh 108,256/- bila ruzuku lakini sasa itauzwa Sh 60,000/- ambapo ruzuku ya serikali ni Sh 48,156/-.

4. SA ingeuzwa Sh 82,852/- bila ruzuku lakini sasa itauzwa Sh 50,000/- ambapo ruzuku ya serikali ni Sh 32,852/-.

5. NPK's ingeuzwa Sh 122,695/- bila ruzuku lakini sasa itauzwa Sh 70,000/- ambapo ruzuku ya serikali ni Sh 52,695/-.

Bwanku M Bwanku.
 

Attachments

  • a8ce7f35de4c4375987f3184f80e5eb0.jpg
    81.5 KB · Views: 10
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…