Hizi ndio nchi 10 pekee Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya Serikali.

Umeandika huku hujafanya research yako vizuri, waulize wazee wako 1964 kulitokea nini Tanganyika, Jeshi la wananchi lilianzishwaje?

Hujawahi kusikia hadithi za JK Nyerere kuvaa baibui na kutoroka? Unafikiri alipenda tuu kuvaa baibui? Au alipinduliwa!

Unaujua ugomvi kati ya Kwame Nkrumah na JK Nyerere source ilikuwa nini? Simple hint; Nyerere baada ya kupinduliwa aliwaalika wanajeshi 100 wa uingereza, lililokuwa koloni la Tanganyika kuwadhibiti wanajeshi wa KEA waliompindua Mwalimu.Kwame alichukia mualiko wa wazungu badala ya waafrika, akamdharau Mwalimu.

Last question, kwanini Kukawa na swahilization na kuminimise matumizi ya kiingereza Tanganyika? Nakushauri kasome machapisho ya kutosha harafu uje na hoja au la uliza swali upewe majibu.

No research no right to speak!!!
 
Wanasema try to be smart enough to feel stupid, Pamoja research zako zote nasema hujui unachokiongea FULL STOP.
 

Kenya umeicha wapi au ilishawahi kupinduliwa na nani tangu 1963??? Malawi ilishapinduliwa lini na nani? Zambia, Namibia!
 

Ndio mataifa yenye watu waoga wasiojielewa duniani
 
Kama wananchi wanatawaliwa vizuri na kwa mujibu Wa sheria nzuri,maendeleo na Huduma mhimu wanapata,hamna matumizi mabaya ya madaraka na Mali ya umma mapinduzi ya wananchi wanaojitambuaa hayapo.ila kinyume na hapo ujue ni nchi ya majuha.
 
Kwenye list yangu nilisema nchi zilizopinduliwa au jaribio la mapinduzi.
Your headline reads "HIZI NDIZO NCHO 10 PEKEE AFRIKA AMBAZO HAZIJAWAHI KUWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI", sasa ile kusema SERIKALI ZA MAPINDUZI umemaanisha ni kutawaliwa na utawala ulioingia madarakani kwa kuipindua serikali iliyopo madarakani. Kenya doesn't fit in that category.
 
🤫1964 yalifanyika Mapinduzi katika nchi iliyoungana na Tanganyika,..

Ukisema Tanzania hayajawahi kutokea Mapinduzi unakosea,.. Sahihi ni kusema Tanganyika haijawahi kutokea Mapinduzi, kwani Zanzibari yalitokea Mapinduzi mwaka 1964
 
Agosti 1 1982 kulikua na jaribio la kumbindua rais Daniel Arap Moi.
Jaribio hilo liliendeshwa na mtu anaitwa Ochuka. Baada ya jaribio kushindwa alikimbilia Tanzania. Kukawa na mazungumzo ya kubadilishana wafungwa basi Ochuka akarudishwa Nairobi na baadhi ya wahaini wa mwaka 1983 huku Tanzania ambao walikimbilia Kenya wakarejeshwa. Watanzania wakapatikana na hatia wakafungwa maisha, Ochuka akapatikana na hatia na akanyongwa!
 
🤫1964 yalifanyika Mapinduzi katika nchi iliyoungana na Tanganyika,..

Ukusema Tanzania hayajawahi kutokea Mapinduzi unakosea,.. Sahihi ni kusema Tanganyika haijawahi kutokea Mapinduzi

Tanzania kuna mapinduzi gani? Mapinduzi yalikuwa Zanzibar ambayo ilikufa mwaka 1964 na Tanganyika ikafa mwaka huo huo!
 
Tanzania kuna mapinduzi gani? Mapinduzi yalikuwa Zanzibar ambayo ilikufa mwaka 1964 na Tanganyika ikafa mwaka huo huo!
Zanzibari imekufa lini? Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ni serikali ya nchi gani?
 
Zanzibari imekufa lini? Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ni serikali ya nchi gani?
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar haipo kiongozi! Siku ya Muungano Jamhuri hiyo (Republic) ilizikwa na hivyo dola ya Zanzibar ikafa, halikadhalika dola ya Tanganyika nayo ikafa. Sote kwa pamoja tukapata Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Mkuu nisaidie jambo moja kwa uelewa tu; ni nani alichukua nchi na kuwa kiongozi wa nchi kwa siku hizo ambazo Mkuu wa Nchi yaani Nyerere Je ni Sajini Francis Higo Ilogi au ni nani?

Msaada mwingine, naomba kufahamu kama unajua tofauti ya Mapunduzi ya Kijeshi na Uasi wa Jeshi.
 
Kenya umeicha wapi au ilishawahi kupinduliwa na nani tangu 1963??? Malawi ilishapinduliwa lini na nani? Zambia, Namibia!
Nchi kama Namibia sioni kama inatakiwa kuwa kwenye taarifa za kupinduliwa ama la kwa sababu hii nchi imepata uhuru miaka ya 1990 wakati huo vita baridi ilikuwa imekuwa baridi haswaa hivyo mambo ya mapinduzi nayo yakawa hayana mvuto/support.
 
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar haipo kiongozi! Siku ya Muungano Jamhuri hiyo (Republic) ilizikwa na hivyo dola ya Zanzibar ikafa, halikadhalika dola ya Tanganyika nayo ikafa. Sote kwa pamoja tukapata Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamuhuri wa Mungano wa Tanzania ni mungano wa nchi mbili Zanzibar na Tanganyika..

Katika Jamuhuri ya Tanzania kuna Wizara za mungano na zisizokuwa za Mungano.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina Wizara zake zisizoingiliwa aidha na Serikali ya Tanganyika vile vile..

Tanganyika imejifanya kuuwa jina lake, ili ikumbatie mamlaka ya serikali kuu ya Jamuhuri ya Tanzania, utapeli wa kisiasa

Zanzibar ina serikali yake, Katiba yake, Baraza la wawakilishi(Bunge)lake,.Bendera yake,..

Zanzibar Lakini bado hawajitambui,ukosefu wa kuwa na "self esteem", "self confidence", ugonjwa ambao tuko nao Waafrika wote,

Nadhani kama SMZ inaongonzwa na mtu ambae sio Mwafrika, Zanzibar ingekuwa na maamuzi Mengine..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…