Kasimba G
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 3,428
- 2,612
Umeandika huku hujafanya research yako vizuri, waulize wazee wako 1964 kulitokea nini Tanganyika, Jeshi la wananchi lilianzishwaje?Habari za wakati wanajamvi,
Leo nimekuja kwenu na orodha ya nchi 10 Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya serikali ya aina yoyote. Nchi nyingi za kiafrika baada ya uhuru ziliangukia katika wimbi kubwa la mapinduzi ya serikali zilizoachwa na wakoloni, kwa kipindi hicho sababu kuu za mapinduzi hayo ilikua ni uchu na tamaa za madaraka walizokua nazo viongozi wa mapinduzi au wadau wa mapinduzi, tuliona viongozi wengi waliofanya mapinduzi na mwishowe kuharibu utaratibu na kuhujumu uchumi na mali za nchi mfano Idd Amin na Mobutu, nchi karibu zote za Africa zilikumbwa na hili tatizo isipokua zifuatazo:-
Swali: Je unadhani kutokua na mapinduzi ya kiserikali ni alama ya ukomavu wa kisiasa, au kukosa watu wenye maono tofauti yenye ushawishi, au woga?
- Botswana
- Cape Verde
- Eritrea
- Mauritius
- Mozambique
- Namibia
- Sao Tome and Principe
- Senegal
- South Africa
- Tanzania
BONUS: Kenya ndio nchi pekee Afrika yenye jina linaloanza na K.
NAWASILISHA.
Hujawahi kusikia hadithi za JK Nyerere kuvaa baibui na kutoroka? Unafikiri alipenda tuu kuvaa baibui? Au alipinduliwa!
Unaujua ugomvi kati ya Kwame Nkrumah na JK Nyerere source ilikuwa nini? Simple hint; Nyerere baada ya kupinduliwa aliwaalika wanajeshi 100 wa uingereza, lililokuwa koloni la Tanganyika kuwadhibiti wanajeshi wa KEA waliompindua Mwalimu.Kwame alichukia mualiko wa wazungu badala ya waafrika, akamdharau Mwalimu.
Last question, kwanini Kukawa na swahilization na kuminimise matumizi ya kiingereza Tanganyika? Nakushauri kasome machapisho ya kutosha harafu uje na hoja au la uliza swali upewe majibu.
No research no right to speak!!!