Ni sahihi kabisa. Nimefanya kazi taasisi ya Serikali, Mshahara wangu wa kwanza ulikuwa 1.5K. Take home ilikuwa laki 9. Miaka 3 baadae nikaenda kwenye NGO, nikawa nalipwa 3.8Mil kwa mwezi na safari kila wakati.
Baada ya miaka 3 wazungu hao hao wakatoa Post kwa wanaotaka kufanya kazi nchi za nje. Tukafanya interview tukapita wachache sana mwishowe tukabaki 3 tu.
Wakatupa shavu kufanya internship Uholanzi mwaka mmoja, baada ya hapo tukapelekwa kwenye vituo vya kazi, mimi nikapangiwa Nambia. Salary yangu niliyoanza nayo ilikuwa ni USD 9, 400 plus house and transport allowance.
Je kuna Afisa anayelipwa hivo serikalini ?
Wakurugenzi (DG)wa taasisi tajwa wengi wanacheza kati ya 15M hadi 20 M plus risk ya kutumbuliwa muda wowote kama Nehemia.
Wenzangu niliowaacha Serikali I am sure mpaka leo bado hawajafika salary ya 4M, tena sidhani kabisa maana sijasikia kupanda kwa madaraja wala salary.
Kibaya zaidi taasisi zote kwa sasa wanatakiwa kufuata sheria za Utumishi wa Umma Kwenye kupandisha salary na madaraja.
Tofauti na mwanzo; taasisi kama MSD, NHIF, TPA zilikuwa zinaajiri wenyewe na wanaviwango vyao vya mishahara na madaraja na ndio maana ukienda hizo taasisi unakuta Mkurugenzi, Manager, Afisa Wote wana Masters yaaani wapo sawa; tofauti yao ni aliyekaa muda mwingi ofisini na mwenye performance nzur.
Yaani hupaswi kuwa jeuri maana inawezekana leo nina report kwako but in few years Wewe uta report kwangu na utakuwa chini yangu.
Hakuna watu wana njaa kama watumishi wa umma; na ndio maana wakurugenzi wa hizo taasisi wanaishi kwa ku deal fake na rushwa. Unashangaa Yaani unakamatwa na Takukuru; ili akuachie Wanakuomba Rushwa lol [emoji23] .
Mk54