Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Walimu wanalipwa vizuri balaa hapa Tz
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muongo huyo!
Anatuuzia chai

We jamaa Mshamba kweli; Milioni 21 kwa mwezi kwako ni hela ? Unajua kazi ninazofanya?

Mkurugenzi wa MSD Aliyetumbuliwa anapokea 20 M kwa mwezi ; Mbona mishahara ya 20 M ni kawaida hata bongo!

Unajua Range za mishahara ya WHO?

Punguzeni ushamba basi kwa yale msiyoyajua. Unaweza kusikia nalipwa Dola hizo lakini do you know work permit nalipia kiasi gani kila mwaka ?

Yaani katika East Africa Tz ndio taifa Lina watu washamba na wasiokuwa na exposure ya maisha.


Mk54
 
CEO wa MSD anakula 20s M kumbe! Yaani anamzidi JAJI kweli?
Tatizo sio ushamba, Kenya kuna maCEO wanalipwa million 100+ za Tanzania, unasema million 20 sio hela uko nyuma ya keyboard ha ha sasa ukitaka kujua milioni 20 ni hela au sio hela kwa nchi yetu hii Fanya study ujue ni watumishi wangapi wa umma na binafsi wanapokea 20M kwa mwezi, kwa nchi kama Kenya ni kweli milioni 20 sio hela kubwa sana kwa sababu kuna watu wanakula hadi milioni 500 (including bonus) kwa mwezi,
UN agencies zina hela haina ubishi issue ni je wewe unafanya kazi huko? Au unatuuzia Chai muda upite, na kama uko huko WHO au taasisi yenye maslahi (kwa maana wewe mwenzetu una exposure) unaonaje ukatoa mbinu kwa vijana wenzio ili wafike huko kwenye 'exposure' ?
 

Sawa. Majibu yote yapo kwenye maandiko yako. Ni wewe kuchagua utatumia Jibu gani kk.

Thanks


Mk54
 
Kuna kitu wengi hamkijui bado humu ndani.
Mishahara kwa kada zinazofanana Tanzania haipishani sana but utofauti unakuja kwenye syringe benefits. Wengine wanalipa posho ya pango ya nyumba, usafiri, vocha na lunch bila kusahau overtime.
Sasa hapa ndipo magape yanapojitokeza.
Dereva anayeanza kazi kuna sehemu akikusanyiwa anaondoka na 2.1 as take home. Sehemu nyingine take home ya dereva ni 3.5 hapo hana cha ziada zaidi ya kusubiri safari.
 
Niliajiriwa kampuni moja, nilikuwa nalipwa hela kiduchu tu na degree yangu(600k) take home plus accommodation (nyumba,chakula,umeme, maji)

Hiyo sio story wadau!!

Aisee nilikuta kuna jamaa wanavuta mpunga mrefu sana na wengi wabongo tu....Nilibahatika kuwa rafiki na human resources manager alikuwa ananihamasisha sana... Alivunja maadili ya kazi yake na kuniambia mishahara ya wadau nilichoka kuna mbongo tulikuwa naye alikuwa anavuta dola elfu 10.

Huyu boss wangu mwenyewe alikuwa anavuta 8m alikuw na Masters by then na akawa ameomba kupiga PhD. Na hiyo 8m sio kwamba ni mkongwe kazini hapana alikuwa na kama mwaka tu alikuja pale kwenye kampuni akitokea Barrick.

Hatimaye mkataba ulipoisha niliamua kutembea. Kikubwa nilichojifunza kwa boss wangu ili ulipwe vizuri inabidi uwe na qualifications konki, wakati naondoka alinisisitiza sana sana nisome [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TISS IKO WAPI????
 
Kama bajeti yao tu bungeni haijadiliwi, je mshahara ambao hata teacher wa primary anavyopewa barua ya mkataba wa mshahara huandikiwa ni siri ilhali sote tunajua salary ya mwalimu?
Kule utaambulia posho ya suit au kombati tu
unajua unachokisemaaaaa???/
 
Mshahara wa 8 M ni mkubwa lakini hapo kodi ni 30% (kama sikosei)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…