Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Siwezi kubisha ila natambua mamlaka zote za serikali watumishi wake wanalipwa vizuri,ila mimi hiyo double standard inanipa shida,
kwanini watumishi wote wa serikali wasilipwe angalau mishahara inayowiana? sisemi walingane lakini kuwepo uwiano.
Nikimaanisha ngazi fulani ya kiwango cha elimu ipate malipo yanayofanana.

Lakini pia mfumko wa mamlaka unaoongezeka kila kukicha unatuongezea mzigo sisi wananchi ili kuwalipa mafao mazuri watumishi wa mamlaka hizo.
Mfano: Kulikuwa kuna haja gani ya kutenganisha LATRA kutoka SUMATRA Kuigawa EWURA na kupata PURA
kwa maoni yangu hivi vilitakiwa kuwa vitengo chini ya mkurugenzi mkuu wa mamlaka husika.Lkn kwa sababu nisizozijua
mamlaka zinaendelea kuanzishwa na mzigo unaongezwa kwenye maji,umeme,mafuta,Mitandao n.k ambavyo mwisho wa siku mlipaji ni mwananchi wa kawaida. Nafikiri hii siyo sawa.
 
6 ndio mpango. Hapo pengine njaa tu tangu waende wale wanajeshi.
Aisee, kuna nafasi 2 za MSD zipo hewani, nimejaribu kutupua ndoano kupitia ajiraportal ila system inagoma. Sijui tatizo nini labda mambo ya nyaya/koneksheni maana ndio habari ya mjini siku hizi
 
SUMATRA imegawanyika kutengeneza LATRA na TASAC
Mmoja ardhini mwingine majini
 
Mfano nimehama kutoka TPA nikaenda wizara inayosimamia TPA, Mshahara wangu utashuka? Maana wizarani sijui kama kuna hizo scale za mishahara ya taasisi hizo.
Kama unapoenda mshahara ni mdogo, haushuki. Kama unapoenda mshahara ni mkubwa, unapanda.
 
tafadhali, hebu ondoa takukuru, tuna wake zetu huko tunajua kila kitu. tafadhali.
 

[emoji17]Tupeni connection jamani ata kujitolea tu jamani wengine hatuna wa kutushika na familia zetu hazijasoma sis ndo tegemezi [emoji1373]
 
TPDF kama haipo hii orodha yako ni batili
 
Kuna uongo mwingine upo wazi kabisa..haihitaji kufahamiana.

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…