uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,657
- 2,406
Siwezi kubisha ila natambua mamlaka zote za serikali watumishi wake wanalipwa vizuri,ila mimi hiyo double standard inanipa shida,Wakuu huu ndo mtiririko wa taasisi za serikali zinazolipa unono na zenye maslahi makubwa kwa watumishi wake
1. TPDC
2. TCRA
4. Ngorongoro
3. Ewura
4. WCF
5. TBS
5. TANAPA
5. Tume ya madini
6. Mamlaka ya chakula na dawa
7. SSRA
8. NSSF/PSSSF
9. BOT
9. Bunge
9. Ofisi ya mkemia mkuu wa serikali
10. TASAC
10. TRA
11. MSD
11. TAKUKURU
11. EGA
12. NHIF
13. TPA
13. TIC
14. KADCO
Lkn pia mfumuko wa mamlaka
16. TANROAD
17. TAA
kwanini watumishi wote wa serikali wasilipwe angalau mishahara inayowiana? sisemi walingane lakini kuwepo uwiano.
Nikimaanisha ngazi fulani ya kiwango cha elimu ipate malipo yanayofanana.
Lakini pia mfumko wa mamlaka unaoongezeka kila kukicha unatuongezea mzigo sisi wananchi ili kuwalipa mafao mazuri watumishi wa mamlaka hizo.
Mfano: Kulikuwa kuna haja gani ya kutenganisha LATRA kutoka SUMATRA Kuigawa EWURA na kupata PURA
kwa maoni yangu hivi vilitakiwa kuwa vitengo chini ya mkurugenzi mkuu wa mamlaka husika.Lkn kwa sababu nisizozijua
mamlaka zinaendelea kuanzishwa na mzigo unaongezwa kwenye maji,umeme,mafuta,Mitandao n.k ambavyo mwisho wa siku mlipaji ni mwananchi wa kawaida. Nafikiri hii siyo sawa.