Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

-ukisoma bajeti Mambo muhimu lazima yawepo, usiri unaotawala Sana ni kwenye baadhi ya Sehemu/vitengo mfano Ofisi ya Rais (IKULU) hapa Kuna Siri nyingi Sana na hata hesabu zake hazichapishwi, Usalama nao pia Mambo yao ni Siri Sana ndiyo manaa hesabu zao zinakaguliwa lakini hazichapishwi, hoja yangu ni kwamba Kuna maeneo yenye Siri nzito kuliko Jeshi ambayo ni IKULU na Tiss (Usalama).
-Shule gani ya msingi hapa Tanzania wanafundisha masuala ya Bajeti na utaratibu wa matumizi ya fedha za umma hebu itaje
- Kuhusu kusema raia tunaambiwa Yale yunayostahili, tunayostahili ndiyo hayo masuala ya matumizi ambayo nimekutajia hapo juu na kimsingi nimekuchambulia vizur Sana rudia kasome
--Inaonekana hujui bajeti na dhana nzima ya Bajeti yaani ww unadhani JESHI linaweza kukwapua tu pesa na lisihojiwe na kisikaguliwe kitu ambacho siyo kweli na ndiyo maana CAG anakagua na PPRA wanawakagua, ndiyo maana kwenye Post zangu za just huko nilisema kuwa hata ikatokea matumizi ya JESHI yamezidi waziri wa ulinzi itabidi apeleke bajeti ya Ziada bungeni kwa hayo matumizi ambayo yamezidi.
-Kuhusu Magari yao kupita Sehemu sio Mimi nilikupinga kutokana na ni hatari na ww ulivyoandika hapa uliandika kiushabaki kwamba hawafanywi lolote, Kuhusu pesa za magumashi Mimi hoja yangu ilikuwa ni kwamba wenye mishahara mikubwa wanaweza kuzidiwa na wenye mishahara midogo ambao wana magumashi Mengi,
 
-mantiki ya hoja yako ya kusema bajeti ya Jeshi haijadiliwi (hapo awali) ilikuwa inataka kuonesha kwamba JESHI lina Siri Sana, nikakupinga kwa hoja kwamba Bajeti ya Jeshi ni Bajeti tu Kama ya Tamisemi
- nilipoleta Hoja usiri wa IKULU na Tiss (Usalama) ilikuwa ni kukuonesha kwamba hizo Taasisi zina Siri nzito lakini bajeti yao inajadiliwa Bungeni, ila tofaut ni tu pale ambapo kwenye ukaguzi wa CAG taarifa zao hazichapishwi, na nilitaka kuondoa dhana ya kwamba JESHI ndiyo wenye nchi na kwamba wao hawasemeshwi kwenye masuala ya fedha
-Kuhusu kukwapua Pesa, ww kwenye bandiko lako hapo juu umesema kwamba zile trilioni 2.3 ambazo ndiyo bajeti ya Wizara ya Ulinzi ukasema kwamba siyo trilioni 2.3 Mimi nikakujibu kuwa bajeti ndiyo hiyo ikitokea matumizi ya Ziada itabidi Waziri wa Ulinzi aandae bajeti ya Ziada apeleke Bungeni, na siyo tu kwamba atakwapua tu pesa, na haiondoi ukweli kwamba trilioni 2.3 ndiyo bajeti yenu hayo mengine mnadanganyana tu huko kambini
-Privileges zote, matumizi yote yapo kwenye vitabu vya bajeti, ndiyo maana ikaitwa Bajeti (Mpango wa Mapato na matumizi)
-kuhusu shule ya msingi na bajeti, ww ndiye uliyesema kwamba hata huo mchanganuo kufundishwa shuleni (msingi), swali la msingi ni kwamba kwa mitaala ya hesabu Tanzania mtoto wa shule za msingi anaweza kufundishwa hesabu Hadi Trilioni?, Kalete huo muongozo unaosema watoto wa primary wanafundishwa Hadi Trilioni, na je mtoto wa msingi anajua Sheria za Kodi? Kwa maana Bajeti ni kutoza (kwa kuongeza au kupunguza) Kodi,tozo,ushuru nk
 
- Mkuu unasema nimeishiwa hoja wakati hakuna hata hoja yako hata moja sijaijibu, mfano tu unazungumzia primary school na hesabu za bajeti wapi na wapi? Hilo hujaliona?
  • mnadanganyana ndiyo huko kambini kuamini kwamba fedha zenu hazijadiliwi bungeni, fedha za JESHI ni fedha za umma, Bajeti inabeba kila kitu kinahohusu Jeshi including zana za kivita,
  • hesabu za Jeshi kupelekwa bungeni hakuondoi unyeti wa Taasisi ya Jeshi.
-
 
Mi nina huzunishwa na mfumuko huu wa bei za vitu sijui kama unazingatia mishahara ya wafanyakazi wote kwani bei zimepanda zaidi ya 30% na zaidi ya hapo bado najiuliza hivi Tz kuna vyama vya wafanyakazi kweli? Hata hao watu wa T.R.A wanaolipwa mamilioni bado hawaioni real value ya hela zao kwa mazingira haya ya mfumuko.
 
Poleni sana mkuu! Wenzenu Wanajeshi mahitaji yao mengi wananunua kwa nusu bei huko makambini kwao na bado wanalipwa mishahara mizuri kama TRA tu halafu mtu anakuja kulinganisha mambo kwa kutumia mihemko tu bila uhakika!
 
Hehe mkuu vipi bado tu hujapataga kazi kwenye chombo chochote cha mambo ya ndani? Tuambie basi wewe unayejua maana kwenda jkt uzalendo tu tayari unajionaga mwanajeshi na unajua kila kitu kuhusu majeshi na wengine wote hawajui kitu!
Umebishana imetosha. Nakuja pm kwako tuyajenge.
 
Rudi shule
 
Pesa ya kawaida wakati mtu mwenye diploma tu anakula 2M+ we unaiita hela ya kawaida hio kwa level ya mishahara ya kibongo?
Bora TPA, TRA kuliko hapo jeiwii.

Hayo mashirika ya kiserikali, yana pesa nyingi mno mbali na mishahara. Tazama maafisa wengi wa hayo mashirika, tazama na maafisa ya jeshi kimaisha.

Achana na TANAPA, TRA, TPA n.k

Kuna watu kwa mwezi nje ya mshahara wanakunja mpaka 10m.
 
Jeiwii maafisa wanalipwa hiviii

Ana mshahara wake
Cheo chake/fani yake jeshini (kuna kitu sikumbuki vyem apa)
Elimu yake inalipwa, degree n.k ila kwa diploma sijui
Ela umeme na maji (sio nyingi)
Lation kama laki mbili hivi au tatu

Ukikusanya vipengele hapo kama 6 hivi anagota kwenye 2m na usheee. Huyu ni luteni.

Ukienda TANAPA, TRA, Bandar, EWURA kwa mtu mwenye degree, hawa maafisa hawawanusi hao watu. Sema hayo mashirika watu pesa zao hawajioneshi lakini jeiwii hanusi hapo.

Unachosema ni kweli kabisa, wengi wakienda nje ya nchi ndo walau wanapata pesa na wengi wao hii kazi wanaona inawabana mno.
 
-Mkuu Kama ni ukayumba kati ya Mimi na ww Nani ameonyesha ukayumba? We ndiyo umeonesha ukayumba kwa sababu Kama hizi mosi ulisema kwamba Bajeti ya Jeshi haijadiliwi bungeni nikakwambia sio kweli na nikakufundisha jinsi fedha zinavyotolewa,pili ulisema Bajeti ya JESHI ni kubwa kuliko Wizara zote nikakwambia kwa takwimu kwamba Bajeti kubwa ni ya Wizara ya Ujenzi ambayo ni Trilioni 4, Bajeti ya pili Ni ya Wizara ya Elimu, tatu ukasema kwamba ukasema privilege zenu Kama Posho, duty free shops hazipo kwenye Bajeti kitu ambacho ni cha Uongo kwa sababu hayo yote sehemu ya Sheria na Bajeti, nne ukasema kwamba shule za msingi wanaweza ku-compute mahesabu ya matrilioni nikakupinga kwa hoja Sasa mpaka hapo Mimi na ww Nani Ni kayumba?
- privilege za Wanajeshi ziko kwenye Bajeti na Sheria za Kodi eg Mambo ya duty free shops etc, nilishakwambia kwamba huwezi kutumia zaidi ya matumizi ambayo umetengewa kwenye Bajeti yako, ikitokea hivyo waziri wa ulinzi anatakiwa apeleke bajeti ya Ziada bungeni kuomba Ziada ya Fedha tatizo unadhani JESHI linakwapua tu Pesa bila utaratibu wanafuata utaratibu na wakikosea wanaambiwa kwenye ukaguzi
-Kuhusu kudanganyana Mambo ya bajeti ndiyo inawezekana mkadanganyana kwa kutokuwa na ufahamu wa kutosha wa Mambo ya fedha za umma na bajeti,
- hata Jeshi likitaka Fedha wanaenda kuomba idhinini kwa CAG na hayo matumizi yanatakiwa yawe kwa mujibu wa Sheria.
 
Umemaliza mjadala.
 
Sasa Luteni wa Jeshi kama anapokea mil 2.3 anatofauti gani na afisa wa TRA anayeanza kazi na mwenye degree??
Ni kweli luteni anakunja 2.3 tena hiyo mimi niliona jamaa akiwa mwaka wa 5 jeshini.

Nina uhakika wa zaidi ya 100% ktk hili sababu niliona salary slip.
 
Kwa mshahara wake anafika hapo 1.3m au haifiki. Ile salary slip sijui niliitupia wapi. Cheo kinalipwa, degree inalipwa, kuna umeme na maji, kuna ration na takataka gani sijui hukoooo

Hapo ukijumlisha ndo anagota 2.3 mpaka 4.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…