Kwanza kabisa kuhusu mimi kuwa TRA kitengo gani na nina cheo gani hilo siwezi kukujibu wala kukupa uthibitisho wowote siwezi kukuonesha salary slip wala job description ili uamini! Na nilishakuambia tangu mwanzo sikukuambia ili wewe uamini bali nilikuwa nakupa taarifa tu sasa kama unafikiri nisipokujibu ndiyo itabadili ukweli kuwa niko TRA basi sawa!
Pili kuhusu sheria ya jeshi kupewa bajeti ya ziada ambayo haichapishwi hiyo sheria haipo kwenye katiba wala wapi na haitakaa iandikwe popote pale ndiyo maana nikakuambia fanya utafiti kwa wahusika! Hata hiyo bajeti unayosema jeshi litaongezea tena nayo ni bajeti kuu na siyo hiyo bajeti ya ziada ninayokuambia ambayo inakaguliwa vizuri tu ila HAICHAPISHWI!
Hii nchi usifikiri kila kitu kinawekwa kwenye katiba yaani unafikiri wewe unaijua katiba kuliko wenyewe walioitunga na hata hawaifuati kila siku wanavunja sheria ndiyo watashindwa kuvunja sheria kwa kuliongezea jeshi bajeti ya siri! Ndiyo maana nikakuambia hii serikali siyo ya kuiamini nikakutolea mfano wa namna tunavyofichwa hata kwenye mapato ya utalii!
Kuhusu ugumu wa interviews za TRA na mitihani ya jeshi huna hoja mzee mitihani ya jeshi ni migumu na hata hao wanaochukuliwa na division 1 na 2 za form six waliosoma PCB na PCM nao wapo wanaofeli! Kuhusu kina 'baba kanituma' kwani unafikiri huku TRA hawapo au kwa vile mmedanganywa kuwa ajira zikipitia PSRS ndiyo hakuna kina 'kamlete?
Kuhusu takwimu za utalii hujaniburuza mkuu bali ni kwamba inaonesha hujui mapato ya utalii ya nchi hii huwa yanaandikwa kwa currency ipi kwenye takwimu za benki kuu! Wala sijakosea na nilimaanisha nilichokiandika kwamba serikali inasema mapato ni 2B ila maafisa wa TANAPA wanasema mapato halisi ni 6B mengine tunafichwa na wala sikusema ni TZS ulikurupuka!
Kuhusu kuwepo na maluteni walioishia form six jeshini nimekuwekea screenshot ya comment yangu ya kwanza kabisa kuhusu huo mjadala hiyo hapo uone nilivyokuburuza! Tena nimeweka uliyoniquote ili usije ukasema labda niliedit so tangu mwanzo nilishasema "miaka hii" na nilikuwa na uhakika na nilichokisema sababu najua zamani walikuwepo tena wengi tu!
View attachment 2118983