Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

-Hata Kama hawawezi kukusanya kila siku hiyo 150,000/- lakini hela ya magumashi wanayo nyingi kuliko watumishi wanaotegemea mishahara,
--By the way, mbona hujasema siku wanayovuka hiyo 150,000/-? let say wamepiga 400,000/- kwa siku? hata Kama isipokuwa constant 150k per day unakuta automatically kwa mwezi mwenzio ana 4M za magumashi
Kuna traffic huku chanika alifariki bhaana, ile kwenda kwake kabisa watu hawakuamini nyumba alokuwa akiishi. Pale kaweka kama 150,000,000 na unaambiwa ana nyumba 3.
 
Hizo Taasisi zilizotajwa ni salary hiyo bwashee, TRA unakuta Ni 2.7 M hiyo ni salary bado posho bado overtime ukijumlisha unajikuta ww unapokea posho mwenzio wa TRA anapokea mshahara

Wenzio hela za magumashi ndio zinawafanya wajenge magorofa
Hii nakubali kabisa yaani.
 
--unataka kulazimisha ulingane na TRA wenzako wako juu 2.7M ndiyo salary ukiwa na CPA unalipwa 3.2 M (bado posho) ambao ni mishahara ya maluteni wawili
-Unataka matrafiki wakuonyeshe mali zako ukawasemee TAKUKURU kwamba wanamiliki mali zaidi ya kipato?
-Wanaojenga magorofa labda majenerali lakini lakini siyo junior officers
-
Unayoyasema ni kweli kabisa mkuu
 
--Kamishna wa Forodha unajua kicheo ni yeye ndiye kiongozi wa kitengo cha Forodha nchi nzima?
-Conclusion ni kwamba hauko TRA uko kwenye kazi nyingine ungekuwa TRA ungejua stahiki za kamishna wa Forodha, na ungejua kwamba Makamishna Wana pesa nyingi kupindukia, Meja labda umlinganishe na Meneja wa TRA Wilaya ndiyo level zao zinalingana na sio kamishna, na infact nimekuuliza swali la mtego na ww ukanasa, kimuundo Kamishna wa Forodha ni mtu wa tatu kwa cheo TRA (Kama sikosei) i.e Kamishna Mkuu,Naibu Kamishna Mkuu, Makamishna wa vitengo eg.Forodha na ushuru wa bidhaa, domestic tax etc
Ninachojua mimi, wale makamishna bandarini, pesa zao za pembeni wanapiga saaana. Wale wana ela kuliko hata mabrigedia.
 
Bora TPA, TRA kuliko hapo jeiwii.

Hayo mashirika ya kiserikali, yana pesa nyingi mno mbali na mishahara. Tazama maafisa wengi wa hayo mashirika, tazama na maafisa ya jeshi kimaisha.

Achana na TANAPA, TRA, TPA n.k

Kuna watu kwa mwezi nje ya mshahara wanakunja mpaka 10m.
Wewe jamaa wa wapi unayejaribu kuestimate mishahara ya watu kutokana na maisha wanayoishi wakati hiko kitu tulishakiongelea sana kule juu! Mada inahusu taasisi zinazolipa vizuri na siyo taasisi zinazoongoza kwa pesa za magumashi au rushwa!
 
Jeiwii maafisa wanalipwa hiviii

Ana mshahara wake
Cheo chake/fani yake jeshini (kuna kitu sikumbuki vyem apa)
Elimu yake inalipwa, degree n.k ila kwa diploma sijui
Ela umeme na maji (sio nyingi)
Lation kama laki mbili hivi au tatu

Ukikusanya vipengele hapo kama 6 hivi anagota kwenye 2m na usheee. Huyu ni luteni.

Ukienda TANAPA, TRA, Bandar, EWURA kwa mtu mwenye degree, hawa maafisa hawawanusi hao watu. Sema hayo mashirika watu pesa zao hawajioneshi lakini jeiwii hanusi hapo.

Unachosema ni kweli kabisa, wengi wakienda nje ya nchi ndo walau wanapata pesa na wengi wao hii kazi wanaona inawabana mno.
Hehe unasema hao watu hawajioneshi! Je una uhakika gani kuwa hata taasisi tena yenye usiri kama jeshi ndiyo inajionesha?
 
Kuna mjinga mmoja anasema koplo analipwa eti mpaka 2m, ni kichaa kabisa uyu mtu.

Hapa nina salary slip ya Koplo. Ameajiriwa 2008. Ukikusanya takataka zake zooote anagota 1.1m na ameoa.
Wabongo bhana! Iko hivi mishahara na posho ya baadhi ya makoplo na masajenti inacheza kwenye 1M-2M, kwahiyo wewe kumfahamu huyo koplo anayelipwa hiyo haimaanishi hakuna makoplo wanaolipwa hizo nilizokutajia, ukizingatia jeshi ni taasisi ambayo ulipaji wake unazingatia vitu vingi kama elimu nk!!
 
Mkuu kwanza kabisa hakuna sehemu nimesema bajeti ya wizara ya ulinzi ni kubwa kuliko wizara zote nimesema kwamba asilimia kubwa ya bajeti ya nchi hii inaenda jeshini kulinganisha na taasisi nyingine! Wewe unaponiambia sijui wizara ya ujenzi au elimu je hizo wizara zina taasisi ngapi chini yake maana kumbuka wizara ya ulinzi haina taasisi nyingine zaidi ya jeshi tu na hapo bado hiyo bajeti ya ziada!

Pili hakuna sehemu nimesema posho na duty free shops hazipo kwenye budget hebu acha kulazimisha kuweka maneno ambayo hayapo na kunirudisha nyuma kwa mambo ambayo nimekwisha kukufafanulia ila umekosa hoja! Elewa kwamba mishahara, posho, zana za kivita, huduma zote muhimu za wanajeshi vinaandikwa kwenye bajeti ila kuna matumizi mengine hayaandikiwa kwa sababu za usalama!

Elewa kwamba hiyo bajeti nyingine ya ziada yote inakaguliwa na Bunge na CAG na serikali inaitambua ila tu haiwi published kwa raia kama ambavyo bajeti kuu ya matumizi yao ya msingi inakuwa published! Hivi sasa kwa mfano mtu nimekuambia yote hayo halafu wewe kwa hiari yako tu ukaamua kubisha sasa hapo unafikiri nitakusaidieje wakati ukweli niliokupa umeamua kuubishia kana kwamba ukibisha ndiyo itabadilika?
- Mkuu kwa heshima na taadhima, unaposema asilimia kubwa ya Bajeti maana yake wao ndiyo wenye bajeti kubwa kuliko wote, na nilishakwambia kuwa 14.4% ya Bajeti (ambayo ndiyo asilimia kubwa kuliko zote) inaenda Wizara ya Ujenzi,hivyo 14% ndiyo asilimia kubwa kuliko zote mkuu
  • Wizara ya Ulinzi ina mafungu matatu mosi Fungu la Wizara, Ngome na Jkt, hoja ya kutokuwa na Taasisi nyingi Haina nguvu unachotakiwa kujua Jeshi lina ukubwa gani (military personnel), gharama ya kuendesha Mafunzo ni kiasi gani? Zana za kivita (ambazo ni Siri) Ni zana kiasi gani?
  • umekubali kwamba duty free shops ni miongoni mwa privilege zinazopitishwa bungeni/ kujadiliwa bungeni, hoja ya kusema Mambo ya Siri inaenda Kwenye sehemu ya Bajeti tunaita jina la jumla ambalo ni zana za kivita na huwa zinawekewa Makadirio yake.
  • bajeti ya Ziada inachapishwa Kama bajeti nyingine kwa sababu inapelekwa bungeni kwenda kuombewa Fedha za Ziada hivyo inakuwa public document,
  • Mkuu umetoa hoja gani hapa ambazo Mimi sijazipinga kwa hoja mujarabu? Tafadhali naomba uorodheshe hizo hoja moja baada ya nyingine halafu tuone nani alikuwa anayumba / kutoa hoja za Uongo.

 
Wakuu huu ndo mtiririko wa taasisi za serikali zinazolipa unono na zenye maslahi makubwa kwa watumishi wake

1. TPDC
2. TCRA
4. Ngorongoro
3. Ewura
4. WCF
5. TBS
5. TANAPA
5. Tume ya madini
6. Mamlaka ya chakula na dawa
7. SSRA
8. NSSF/PSSSF
9. BOT
9. Bunge
9. Ofisi ya mkemia mkuu wa serikali
10. TASAC
10. TRA
11. MSD
11. TAKUKURU
11. EGA
12. NHIF
13. TPA
13. TIC
14. KADCO
15. TANESCO
16. TANROAD
17. TAA

Kuna mtu alikua Bunge akasema mishahara yao ya kawaida tu sio mikubwa sasa sijui alikua anatuzuga ili wana wasipambane kuhamia sielewi.
 
-mantiki ya hoja yako ya kusema bajeti ya Jeshi haijadiliwi (hapo awali) ilikuwa inataka kuonesha kwamba JESHI lina Siri Sana, nikakupinga kwa hoja kwamba Bajeti ya Jeshi ni Bajeti tu Kama ya Tamisemi
- nilipoleta Hoja usiri wa IKULU na Tiss (Usalama) ilikuwa ni kukuonesha kwamba hizo Taasisi zina Siri nzito lakini bajeti yao inajadiliwa Bungeni, ila tofaut ni tu pale ambapo kwenye ukaguzi wa CAG taarifa zao hazichapishwi, na nilitaka kuondoa dhana ya kwamba JESHI ndiyo wenye nchi na kwamba wao hawasemeshwi kwenye masuala ya fedha
-Kuhusu kukwapua Pesa, ww kwenye bandiko lako hapo juu umesema kwamba zile trilioni 2.3 ambazo ndiyo bajeti ya Wizara ya Ulinzi ukasema kwamba siyo trilioni 2.3 Mimi nikakujibu kuwa bajeti ndiyo hiyo ikitokea matumizi ya Ziada itabidi Waziri wa Ulinzi aandae bajeti ya Ziada apeleke Bungeni, na siyo tu kwamba atakwapua tu pesa, na haiondoi ukweli kwamba trilioni 2.3 ndiyo bajeti yenu hayo mengine mnadanganyana tu huko kambini
-Privileges zote, matumizi yote yapo kwenye vitabu vya bajeti, ndiyo maana ikaitwa Bajeti (Mpango wa Mapato na matumizi)
-kuhusu shule ya msingi na bajeti, ww ndiye uliyesema kwamba hata huo mchanganuo kufundishwa shuleni (msingi), swali la msingi ni kwamba kwa mitaala ya hesabu Tanzania mtoto wa shule za msingi anaweza kufundishwa hesabu Hadi Trilioni?, Kalete huo muongozo unaosema watoto wa primary wanafundishwa Hadi Trilioni, na je mtoto wa msingi anajua Sheria za Kodi? Kwa maana Bajeti ni kutoza (kwa kuongeza au kupunguza) Kodi,tozo,ushuru nk
Kwenye taarifa ya cag jwtz ipo? Naomba kuuliza cheif?
 
Kuna mjinga mmoja anasema koplo analipwa eti mpaka 2m, ni kichaa kabisa uyu mtu.

Hapa nina salary slip ya Koplo. Ameajiriwa 2008. Ukikusanya takataka zake zooote anagota 1.1m na ameoa.
Lation hapo bado mkuu
 
Hahaaa young man basi tufanye hivi wewe baki na imani yako kwamba matumizi yote ya jeshi yanawekwa kwenye bajeti hiyo unayoijua wewe! Ila wanaoujua ukweli hawawezi kubisha hili hata kama hawafurahii!

Kwa sababu sioni mantiki ya kukaa kujadili jambo ambalo jibu lake ni abcd! Ila wewe ukataka tuzunguke tuanze kuliwekea maelezo mengi kana kwamba hayo maelezo mengi ndiyo yatahalalisha ukweli wa hilo jambo!

Wakati mimi najadili vitu ambavyo vipo kiuhalisia wewe unataka tujadili kutegemeana na ufahamu! Wakati hivi vitu havihitaji na wala havitegemei ufahamu wa mtu bali ni swala la kusema tu hii ni nyeupe na hii ni nyeusi basi hata kama usipoamini!
- Mkuu Mimi Kwanza sijakulazimisha ukubali hoja zangu, na kuhusu bajeti nilishakwambia kuwa zinakuwaje
- by the way hujajibu hoja yangu ya kwamba tuainishe hoja zetu zote tuone nani alikuwa anayumba/ anaandika Uongo, au unaogopa afande?
 
Kwenye taarifa ya cag jwtz ipo? Naomba kuuliza cheif?
- wapo ndiyo na wanakaguliwa na ripoti inatoka ikiwana opinion za CAG
- hata PPRA (mamlaka ya kudhibiti manunuzi ya umma) huwa waakagua manunuzi ya Jeshi.
 
- Mkuu Mimi Kwanza sijakulazimisha ukubali hoja zangu, na kuhusu bajeti nilishakwambia kuwa zinakuwaje
- by the way hujajibu hoja yangu ya kwamba tuainishe hoja zetu zote tuone nani alikuwa anayumba/ anaandika Uongo, au unaogopa afande?
Unapata wapi nguvu za kubishana na mwanamke kiasi hiki?
 
Kuhusu bajeti ni kwamba ulihisi siyajui uliyoyaandika? Mimi nimekushangaa kubishia kitu ambacho nimekuelekeza nje ya hayo unayoyajua wewe ila unabisha umebaki unakomaa na hayo unayoyajua wewe sasa unataka kuweka hoja ipi kwenye mambo ambayo ni straight tu wala hayahitaji kuzunguka!

By the way nashukuru ulishakubali ukweli kwamba afisa mwenye degree anayeanza kazi TRA anapokea 2.3M nje ya marupurupu na afisa mwenye degree anayeanza kazi TPDF yaani luteni usu mwenye nyota moja anapokea 2.3M nje ya marupurupu! Labda uniambie unataka tujadili nini hapo wakati hilo liko straight!

Ulichonishangaza ni kuzunguka kwa jambo ambalo liko wazi na wala halihitaji mjadala kana kwamba tumepewa mtihani wa general studies ambao maswali yake mengi yanahitaji ufahamu kuyajibu! Kwa kukusaidia fanya utafiti wako binafsi usisubiri taarifa kutoka kwa wanasiasa ambao mengi wanayaficha!
-- ww umenielekeza Mimi? Hoja gani wakati nilikuwa nakuburuza ninavyotaka au umesahau unakumbuka nilikuwa nakupa hoja za mitego kupima uelewa wako Mfano. Meja vs Kamishna wa Forodha ukakubali ukaanza kuleta ulinganisho wa Kanali na Kamishna wa Forodha, nyingine unakumbuka ulisema kwamba asilimia kubwa ya bajeti inaenda Jeshini nikakwambia siyo kweli bajeti kubwa inaenda Wizara ya Ujenzi ambayo ni trilioni 4.3 huku Ulinzi ni Trilioni 2.3 umesahau hili?, Unakumbuka mwanzoni ulisema bajeti ya Jeshi haijadiliwi bungeni nikakuburuza ukakubali kuwa inajadiliwa ukaanza kusema haipingwi nikakuuliza swali kuwa tangu lini bunge letu hili limewahi kukataa bajeti?, Nyingine nilikwambia Kuna maluteni Wana elimu wa form6 ukabisha nikakuburuza hadi ukakubali
-kuhusu Luteni nilikwambia Ni 1.5 M na sijawahi kusema 2.3 M,
- kwa hiyo Kama wanasiasa Mambo Mengi wanayaficha ww ndiye mwenye taarifa sahihi,halisia na za kweli? hebu taja Sehemu hizo taarifa zilipo.
 
Kuhusu meja vs kamishna wa forodha uliuliza ni nani ana mshahara mkubwa nikakuambia meja ana mshahara mkubwa, ukasema kwamba ulikuwa unanipima kwamba eti kamishna ni cheo cha tatu kutoka juu kwa TRA! Nikakuambia mtu fulani kuwa na cheo kikubwa kwenye taasisi moja siyo hoja ya kumzidi mshahara mtu mwingine kwenye taasisi nyingine ambaye naye ana cheo kikubwa ila tu hamfikii huyo wa taasisi nyingine, ndiyo sasa nikakuambia kuwa kwanini pia usimlingaishe na wenzie mameja jenerali ambayo ndiyo wanalingana kicheo?

Kuhusu bajeti nilimaanisha nilichokisema kwamba asilimia kubwa ya bajeti ya nchi hii inaenda jeshini ukijumlisha na zile privileges za ziada ambazo haziwi published, ukasema wizara inayoongoza kwa bajeti kubwa ni ujenzi nikakuambia je hiyo wizara ya ujenzi ina taasisi ngapi kumbuka wizara ya ulinzi ina taasisi moja tu ambalo ni jeshi! Ukasema kwamba hiyo bajeti kuna mafungu matatu ambayo ni wizara ngome na jkt, kitu ambacho hakibadilishi ukweli kwa sababu ngome ni sehemu ya jeshi na jkt ni sehemu ya jeshi so bajeti inaenda sehemu moja!

Kuhusu bajeti ya jeshi kujadiliwa nilichomaanisha ni kwamba bajeti ya jeshi kama jeshi haina mjadala sijui kama unajua maana ya kukijadili kitu kwa scenario kama hiyo, kwa sababu nilichomaanisha ni kwamba bajeti ya jeshi haipingwi wala hairekebishwi either bajeti kuu au bajeti ya ziada bali inakaguliwa tu kama bajeti nyingine tofauti na taasisi nyingine ambazo bajeti zake zinaweza kurekebishwa! Kuhusu kuwepo na maluteni wa form six, sijakubali kwa sababu jeshini HAKUNA maluteni walioishia form six mkuu labda kwenye jeshi lako!

Sasa mkuu kama uhalisia ni kwamba mshahara wa luteni usu wa jeshi ni 2.3M ila wewe ukaamua kubisha ukasema ni 1.5M unataka mtu asemeje tena wakati umeshaamua kuukataa ukweli kwa hiari yako, yaani ni sawa na mimi niamue tu kusema TMO wa TRA analipwa 1.3M unafikiri itabadili ukweli kwamba wanalipwa 2.3M kwa sababu tu mimi nimeleta ubishi hapo? Taarifa kamili na sahihi kuhusu bajeti ya ziada ya jeshi huwezi kuipata bungeni wala kwenye maandishi mkuu, ndiyo maana nikakuambia fanya utafiti wako binafsi labda unaweza ukaokoteza machache!

Yaani we jamaa bhana nimegundua kumbe hayo unayosema umeniburuza ni yale ambayo niliamua kuyaacha kwa sababu ukweli wake nilishakupa ila kwa makusudi kabisa ukaamua kuyakataa na kupinga, sasa hapo unataka mtu aendelee kukuambia nini au aendelee kubishana na wewe ili iweje? Sasa mfano kama hapo unaposema kuna maluteni walioishia form six na kwamba mshahara wa luteni ni 1.5M, siwezi kuendelea kubishana na wewe tena kuhusu hilo itakuwa ni kupoteza muda tu maana ukweli uko pale pale sasa napo utasema umeniburuza?
-meja ana mshahara mkubwa Kama ulisema hivyo mbona baadae ukaja ukabadili msimamo wako ukaanza kusema alinganishwe na Kanali au majenerali,? Kwa nini ubadili kauli yako ya awali? Maana yake huna taarifa za uhakika hivyo una badili badili kutokana na ukweli wa hoja,
  • Umesema kwamba mtu kuwa na cheo kikubwa kwenye Taasisi fulani siyo Kigezo cha kumzidi mtu mwingine mwenye cheo wa Taasisi nyingine, hivi unadhani tujadili Wakuu wa idara wa halmashauri? Hapa tujadili Wakuu wa idara wa TRA i.e Forodha na ushuru wa bidhaa, na ndiyo ujue kwamba Kamishna wa Forodha ana pesa nyingi kuliko meja, Meja level zake ni Mameneja wa TRA wilayani
  • hoja ya asilimia kubwa ya bajeti kwenda Jeshini ilishafeli bajeti yenu Ni 2.3 trilioni, Ujenzi ni Trilioni 4.3, hata Kama Kuna matumizi ya kificho (Kama manunuzi ya Zana)hayo unayosema yatakuwa ndani ya trilioni 2.3, fedha za umma hazitoki kizembe matumizi ya fedha za umma ni lazima yawe yameidhinishwa, kuhusu uwingi/ ukubwa wa Taasisi kwamba Bajeti ya 2.3 trilioni inatumika na Jeshi tu, nilikujibu kwamba matumizi hayo yanategemea ukubwa wa Jeshi, manunuzi ya Zana, Mafunzo kwa askari,
  • Kuhusu kupingwa kwa bajeti, nimekuuliza swali ww hapa Tanzania hili bunge letu ni lini umewahi kuona Bunge limekataa kuidhinisha bajeti ya Wizara yoyote? Kama umewahi kuona hebu itaje hiyo Wizara, tatizo kila hoja unakosea Mara haijadiliwi bungeni, Mara haipingwi? Inaonekana huna msimamo na hujui taratibu za fedha za umma
  • form six maluteni wako wengi tu Jeshini, ndani ya Jeshi Hilo Hilo ulilopo na Pengine na ww umo ndani ya hao form six (wasio na ujuzi wa chochote)
-luteni hapati 2.3 M ni uongo mshahara wake Ni 1.5 M nimepinga na huo ndio ukweli,usidanganye watu humu kutaka kujilinganisha na TRA
- Ona hata usivyojua kujenga hoja huyo TMO ni wa level gani II, I, senior II, Senior I, PRINCIPAL II, PRINCIPAL I umekuwa general be specific
-ukweli upi ulionipa? Wakati nilikuwa nakuyumbisha Hadi unabadili msimamo, hivi ungekuwa na kesi ya jinai c ungeenda jela? Kwa sabab ya retract na kubadili badili
- Umeamua kuyaacha wakati huyajui? Mara haijadiliwi, Mara haipingwi? Mara asilimia kubwa ya bajeti Ni Jeshi? Huo si uongo mtupu? Labda useme kitu gani unajua mkuu? Kulenga shabaha au
 
We jamaa bhana halafu ulivyo huelewi unachosimamia mwanzo ulisema siko TRA kwa sababu kuna vitu sijui kuhusu TRA! Ila hadi sasa bado umekomaa kuwa mimi ni mwanajeshi na wakati unasema sijui lolote kuhusu jeshi!

Mbona kwenye jeshi husemi kuwa "wewe hauko TPDF kwa sababu kuna vitu hujui kuhusu TPDF" ili tuone kama kweli uko serious na unachosimamia! Mkuu kukata mzizi wa fitina hebu naomba niambie hizo taarifa zote ulikozipata!

Kuanzia kuwepo kwa maluteni walioishia form six na kulipwa 1.5M hadi hayo mambo ya bajeti ambapo mwanzo ulisema kwamba kuna wizara ambazo bajeti zao zinarekebishwa! Mimi nikakuambia ya wizara ya ulinzi hairekebishwi ukaja ukabadilisha!
-kwani ukiwa mwanajeshi ni kwamba utaelewa kila kitu including public finance? ww hujui huko Jeshini wanaingia hadi form four wenye ufaulu wa chini/ form six wenye ufaulu wa chini? unatarajia hao wenye form4/6/ Degree (wenye uwezo mdogo) wataweza kupambanua Mambo ya kuhusu fedha za umma? Si wanachojua wao wapokee mishahara na posho tu,
-Kuwa tpdf haimaanishi kwamba unajua/ uelewa wa Mambo ya fedha, ndiyo maana ww ukaropoka kuwa Bajeti haijadiliwi bungeni, nikakurekebisha kwamba inajadiliwa, ukabadili ukaanza kusema haipingwi nikakuuliza swali kwamba lini kwenye Bunge letu limekataa kupitisha Bajeti? hili swali ulijibu? Halafu ndiyo maofisa nyie mna mawazo haya je wale mnaowaongoza watakuwaje?
- Kuhusu taarifa zinapatikana tu kirahisi Tena kutoka Primary source, ikiwa mishahara ya Kitengo (usalama) inajulikana sembuse ya Jeshi )
-maluteni wa form six wapo jeshini,
- kuhusu kurekebishwa kwa bajeti maana yake unarekebisha aidha numerical error za shilingi mfano unakuta wameandika bilioni 230 badala ya bilioni 23 hapo lazima Bunge litarekebisha hawawezi kupitisha kitu chenye kasoro, hivyo hivyo kwenye Bajeti ya Ulinzi ikitokea wameandika mfano trilioni 23 badala ya trilioni 2.3 patarekebishwa Bunge haliwezi kupitisha kitu chenye kasoro umenipata?
 
Hehe ila TRA ulipodai kuwa sijui mshahara wa kamishna wa forodha hukutaka maneno mengi, hapo hapo ukaona useme siko TRA siyo? Kwa taarifa yako hao unaosema wa la saba sijui form four failures wote huwa wanaishia kuwa maaskari tu hakuna anayekuwa afisa sasa ulivyotoa hayo maelekezo sijui ulihisi kwamba sijui kuwa wenye level hiyo ya elimu wapo, mimi nimekupinga kuwepo kwa maafisa walioishia forma six hiyo ilikuwepo zamani ila miaka hii haipo tena ni lazima kwanza wakasomeshwe wawe na degree kulingana na walichosomea a level kisha ndiyo wanavalishwa nyota!

Yes nilimaanisha na nilikuwa nina uhakika asilimia mia niliposema bajeti ya jeshi haijadiliwa bungeni kwa sababu hiyo bajeti inayokuwa published ambayo mnaijua ninyi siyo yote kulingana na inayopelekwa jeshini, kuna nyingine ya ziada ambayo inapitishwa lakini haiwi published kama hiyo bajeti kuu! Bado ukabisha umekazana eti inaandikwa kama zana za kivita nani kakudanganya kwamba zana za kivita ni bajeti ya ziada hizo ziko kwenye bajeti kuu na zinajulikana, wewe umebaki tu kuzunguka na kucheza na kiswahili nilichotumia ili ionekane unajenga hoja kumbe hujui unachozungumza!

Watu kibao huko juu wamekuambia mshahara wa luteni usu ni 2.3M hakuna hata mmoja aliyesema 1.5M, wewe ndiyo wa kwanza nakusikia unasema hivyo na yule mwenzio aliyesema ni 1.1M watu wakamshushua akakimbia uzi! Pia kuna jamaa alileta hapa salary scales za position mbalimbali za TRA naye akasema kuwa yuko huko ukaanza kumbishia kwa kucheza na statement yake aliyosema "i stand to be corrected" wakati kiuhalisia alikuwa sahihi, ila wewe mwanzoni kabisa mwa huu mjadala ulisema afisa wa TRA anayeanza kazi anapokea 2.7M kitu ambacho ni uongo sasa unataka tuendelee kubishana nini tena?
-ni kweli hujui mshahara wa Kamishna wa Forodha ndiyo maana ukasema anazidiwa, na Meja,
-Wapi Mimi nimesema kwamba form4 wanakuwa maofisa (onyesha) hoja ya form four failure imekuja baada ya kusema Askari wanajua vizur Mambo ya kijeshi yahusuyo Bajeti ndiyo nikakupinga hapo
  • umeona Sasa unavyojichanganya mwanzon ulisema Hakuna maofisa wa form six nikakwambia wapo, sasa umekubali kuwa wapo ila utaratibu wa Sasa ni Hadi uwe na degree/ diploma? Umekubali kwamba maofisa wa form six wapo, ndiyo maana Mimi nakwambia Nina kuburuza nnavyotaka na ukaburuzika Hadi unabadili kauli yako
  • Bajeti ya Jeshi inajadiliwa Bungeni,Kama Bajeti ya Tamisemi nothing special kwa Jeshi, Sasa hiyo Bajeti unayosema ya ziada itapitishwaje bungeni bila kuingia kwenye Hansard? Document yoyote ile ikishafika bungeni ni Public document, Sasa Bajeti itapitishwaje na bunge bila kujadiliwa? inaonekana hujui hata parliamentary business zinavyofanyika, bajeti inasomwa na waziri husika na Wabunge wanachangia hoja kuhusu hiyo bajeti, Sasa unaposema inapitishwa na haiwi published ni Uongo shughuli za bunge zote zinaendeshwa kwa Uwazi na kwa njia ya mijadala, na document yoyote ikishaingia bungeni ni public document, Sasa itapitishwaje bungeni bila kuingizwa kwenye Hansard? Unajua maana ya Hansard na Kazi ya Hansard?
  • Kuhusu suala la Zana za kivita ni wapi nimesema haiko kwenye Bajeti kuu? Mimi nikichosema ni kwamba ikitokea bajeti ya Jeshi haitoshi waziri anapeleka 'Bajeti ya ziada' bungeni kwa ajili ya Hilo Jambo na Kama ni Mambo ya Siri Kama silaha waziri hatataja hizo silaha atajaja tu 'zana za kivita'
  • Kwa hiyo watu wengi wakiunga mkono Jambo fulani inamaanisha Hilo Jambo ni la kweli? hao wengi unawajua personally uelewa wao? Mshahara ni 1.5 M huo ndiyo ukweli na sijawahi kubadilisha
  • Kuhusu kuleta salary scales za TRA, huyo aliyeleta hizo scale una uhakika naye? Na unaamini alichokisema ni kweli?
  • unataka kujilinganisha Na TRA ? Hivi Ugumu wa interview za TRA unazilinganisha na za huko kwenu?

 
Back
Top Bottom