Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Acha uongo unataka kusema huyo wa moshi vijijini anakula 1.8M? Mishahara ya halmashauri ni 900k tena kwa mzoefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uongo unataka kusema huyo wa moshi vijijini anakula 1.8M? Mishahara ya halmashauri ni 900k tena kwa mzoefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaelipwa hivyo labda sio mmbongo kwa asilimia 100%!
Kama ni muhindi au mkaburu ntakubali, ila ngozi nyeusi kulipwa hivyo labda vyeti viwe vinasomeka Cambridge,IST,Wales,Havard n.k!
Mbona wengi tuu hujui
 
Mbona hamna sekta ya
Doctors
Nurses
Teachers
?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hats Mimi nasubiri wenye uzoefu walete kwa fani hizo mipunga yao inakuaje
Mkuu mshahara kwa kiasi kikubwa unakua defined na position na sio elimu.

Daktari (MD) anaefanya kazi Halmashauri analipwa 1.48M kabla ya makato wakati yule anaefanya kwenye hospitali maalum (Muhimbili, Mlonganzila, MOI, Ocean Road) yeye yuko juu kidogo.

Hivyo hivyo kwa manesi, wafamasia na wachunguzi wa maabara.

Ila kwa ujumla fani za afya ni miongoni mwa wanaolipwa pesa ya kawaida sana, sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kimantiki hao wanaolipwa mamilioni ya fedha 10m** wawapite hata doctors ambao kazi yao n kuokoa uhai ambao haununuliwi kW fedha yoyote.....embu tujadili kazi yao Ina tija kiasi gan kwenye nchi/jamii au wanazalisha nini(kiuchumi) mpaka walipwe hvyo???mfano TPA,TRA,NHIF,TANAPA nk
 

Katika degree zote hapa Tanzania degree yenye mshahara mkubwa mkiajiriwa serikalini ni udaktari ndo inaongoza

Kuna Md,Dds,Dvm then wanafuata manesi(bsc nursing) na engineers

Hii ni kwa sabab serikalini scale ya mshahara ya kuanzia huwa wanaangalia degree uliyosoma ni ya miaka mingap
Ndo maana madaktari( Md,Dds na Dvm) ndo huwa wana mshahara Mkubwa kuliko degree zingine kama engineers ambazo ni miaka minne

So kama daktari na engineer wataajiriwa sehem moja kwa wakat mmoja ie halmashauri daktari atakuwa na mshahara mkubwa kidogo kuliko mhandisi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
TRA labda kuibia watu ila slip zao mishahara ya kawaida sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe binafsi unapokea kiasi gani kwa mwezi kama ni mwajiriwa na kama sio mwajiriwa tueleze wastani wa mapato yako kwa mwezi, mana kila mtu ana maoni yake linapokuja swala la kipato cha mtu na mara nyingi wengi tunapenda kulinganisha kile tunachopata na kinachosemwa kwa wengine. Ikiwa wewe kipato chako kwa mwezi ni zaidi ya mil 3 basi una haki ya kusema wana mishahara ya kawaida kwa upande wako, note: mil 3 ni mshahara wa ofisa wa kawaida ambaye ndio ana anaanza kazi au ana mwaka mmoja kazini. Alaf tujiulize the general life standard kwa watumishi hapa Tanzania either wa umma au sekta binafsi mtumishi anae pokea mil 3 kwa mwezi tunamweka ktk income standard ipi?! Mana the fact is ata huko sekta binafsi taasisi au mashirika yanayolipa kuanzia mil 3 kwa mwajiriwa mpya zipo chache sana
 

Nani amekudanganya ofisa wa kawaida tra analipwa milion 3... net ya ofisa anaeanza kazi Tra hata milioni moja haifiki.. peleleza vizuri.. nimefanya kazi saccos ya tra .. nimecheza sana na salary slips zao.. milioni 3 na zaidi ya milion 3 wapo wanaolipwa ila ni wachache sana maana ni wale mabosi
 
😂😂Kumbe ulifanya kazi Tra saccos, kibarua chako pale Tra saccos kilikoma mwaka gani? nianzie hapo kwanza mana kwa majibu wa maelezo yako bila shaka kwa sasa sio mtumishi wa Tra saccos, ila tu kwa kukusaidia waulize wale maofisa wa Tra saccos kama bado una connection nao scale ya Tras 3/1, Tras 3/2, Tras 4/1 after lawson wanapokea kiasi gani hao ni maofisa wa kawaida sana na highest scale inagotea 12 huko usifike. Na none officers wote naamanisha ma office attendants na nk net salary yao not less than 800k.
 
Usiendelee kubishana nae.

Unaweza ukawa nurse amana hospital ila ukalipwa tofauti sana na taasisi kama ya saratani ocean road.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufikia mwaka 2018,mshahara wa officer anaeanza kazi Tra mwenye degree ulikua 960,000/=. kwa sasa sijui wanalipwaje
 
Wakati muhasibu anakula 700,000/-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…