Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Mkuu hao watumishi si tunaishi nao humu humu mitaani na wewe si umesema hapo juu kuwa kuna mmoja umeona hadi salary slip yake? Sasa si uweke hapa hiyo namba na hizo alizozikosea si uzitaje mbona unazunguka sana chief?
Nacheka tu
 
Acha kujipa moyo binti kiziwi, ujue kuna taasisi zinazalisha pesa tena bila kutumia mtaji mfano kama TPA, EWURA, TBS n.k kwanini zisiwamwagie mishahara minono watu wake.

Mkuu
Mkuu mimi Niko sensitive sana na mshahara, kazi yangu ya kwanza nilikua nalipwa laki nane na nusu take home, huku nimepewa nyumba, gharama za umeme plus maji lakini nilifanya kazi mwaka mmoja tu nikaandika barua ya kuacha kazi nikaomba kazi mahali pengine
Aise! Huenda aliyechukua nafasi yako anaamshukuru Mungu usiku kucha kwa wewe kuacha kazi hiyo na yeye akapata.
 
kwa maelezo yako mkuu inaonyesha huna uhakika ulichokiandika!
ulishafanya proff yoyote ukajua kiasi wanacholipwa ngorongoro?
ook hivi hujui Afisa tuu wa TRA mwenye dip anavuta mpunga mrefu!!? Mbali na hayo makando kando uliyoyaorodhesha!?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona hamna sekta ya
Doctors
Nurses
Teachers
?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hizo kazi ni za Wito,hazina mishahara mikubwa! Kule ni mwendo wa CCD tu na kwa taechers ni Tuitions tu.
 
Duuh yaani mimi siku zote wanavyosemaga mishahara minono, huwa nadhani labda hizo taasisi zote ofisa anayeanza kazi anachezea kuanzia 2.5M-3M!

Kumbe wengi hata 2M hawafiki, kama ni hivyo basi TPDF linalipa vizuri asee maana jeshini hizo 1.8M-2M ni mishahara ya makoplo na masajenti ambao wengi wameishia la saba na form four!

Bado hujazungumzia wenye degree maofisa kuanzia maluteni, halafu kuna watu wanadharau eti jeshini hamna kitu eti pesa ziko TRA na BOT kumbe pesa zenyewe ndiyo hizo wabongo bhana!
Pesa zipo jeshi la bakabaka, bado ujaenda dafur au Congo na kurud salama.
 
Kuna captain wa jeshi leo kanikopa elfu 20,sasa sijui huo mshahara wake huwa haumtoshi au vipi?
Wengi huwa mnasema hivyo ila mtambue kuwa kulipwa mshahara ni kitu kimoja na matumizi ya huo mshahara ni kitu kingine! Mara nyingi njaa ya mtu haitegemei na mshahara wa taasisi anayofanyia kazi bali matumizi yake binafsi na namna anavyopangilia kipato chake maana wanajeshi wengi huwa wanasifika kwa kupenda anasa za hapa na pale!

Wakati wewe una mfano wa huyo captain mimi pia nina mfano wa captain ambaye ana nyumba nzuri na magari mazuri na wala hana njaa na ana biashara nzuri tu! Hulazimishwi kuamini kuwa jeshini wana mishahara mizuri na posho nzuri jumlisha mikopo nje nje ukilinganisha na graduates wengi walioajiriwa kwenye taasisi za serikali ambazo zimetajwa hapo juu!

Maana hata hao waajiriwa wa TRA na BOT wapo wenye njaa na wanakopa sana tu pamoja na hiyo mishahara wanayolipwa ambayo kutwa inasifiwa humu lakini hatuwezi kubeza taasisi nzima kwa ajili ya hao baadhi walioshindwa kupangilia vizuri matumizi yao! Na ukumbuke pia tunatofautiana majukumu kuna mtu mshahara wake anahudumia karibu ukoo mzima!
 
Inakopa serikali, wanakopeshwa makazini, na hao watu wa starehe, wakistaafu wanafulia, Ila wanalipwa uliza kwa wanaojua., Mwalimu akasome.
Tatizo watu wakisikia jeshi wanawaza vile vyeo vya chini tu! Kuna jamaa mmoja ni sajenti alikuwa anawaambia raia eti wasiwashadadie sana maofisa na kuwadharau wao maaskari!

Sababu hao maofisa wengi huwa wanapenda starehe na anasa hawajui kutumia pesa zao vizuri! Na wakati mwingine wakifulia wanawakopa maaskari ambao raia wanawadharau!

Akawa anaelezea mafanikio yake kibiashara pamoja na kwamba ni mwanajeshi wa cheo cha chini! So unaona kabisa kwamba tatizo siyo mshahara bali ni matumizi ya mtu binafsi!
 
Tatizo watu wakisikia jeshi wanawaza vile vyeo vya chini tu! Kuna jamaa mmoja ni sajenti alikuwa anawaambia raia eti wasiwashadadie sana maofisa na kuwadharau wao maaskari!

Sababu hao maofisa wengi huwa wanapenda starehe na anasa hawajui kutumia pesa zao vizuri! Na wakati mwingine wakifulia wanawakopa maaskari ambao raia wanawadharau!

Akawa anaelezea mafanikio yake kibiashara pamoja na kwamba ni mwanajeshi wa cheo cha chini! So unaona kabisa kwamba tatizo siyo mshahara bali ni matumizi ya mtu binafsi!
Sajent darasa la Saba au form four ila mishahara yao utafananisha na msomi wa kada nyingine na mwenye ujuzi, bado mwenye nyota kwenda juu.
 
Mashamba uyu kuna watu

fuel allowance tu 1m

mawasiliano 3lk

House 5lk

Basic 1.8

Huyo ni waserikali na ana miaka 4 kazin tunao maofisin
Sasa mbona mnasema serikalini hakulipi kama private ila hamuachi hizo kazi?😅
 
Huo ni mshahara wa afisa wa TRA anayeanza kazi. Kumbuka afisa ni mwenye Digrii. Kwa mateso hayo ni bora uwe TRA
Huko TRA unaingiaje kwa mfano😅 maana kuna mtoto wa Ndugai anatakiwa aingizwe kabla ya nyie akina kajamba nani!
 
Inategemea na hiyo private unayoizungumzia wewe iko vipi..kuliko kuwa kwenye vijikampuni hivi vya wachina au wahindi bora niwe serikalini tu..private ukiwa kwenye NGO za kimataifa na makampuni makubwa kama TBL,serengeti, TCC na mengine ya aina hiyo naweza kushawishika kuwa huko kuna maisha ila sio umeajiriwa kwa kampuni za wachina nawe eti unawavimbia watu walioko government,tunajua mishahara ya wachina huwa haizidi laki 4.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂 wale wahuni wakifuatiwa na wahindi wanaongoza kwa kuua ndoto za vijana!
 
Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
Mwenye degree jwtz anakunja milion 2.7 coz proffessional allowances ni laki 9 kwa mwenye bachelor na laki 8 kwa diploma + maji+ umeme+ vinywaji + meals+ ngome+ pedi ( kwa w
Mwanamke)yaan salary slip za askari wa jwtz imeshiba mnoo Nashangaa hawapo kwenye hiyo chart yakoo ya magumashi
Jei Wii wanakula mipunga mirefu sana basi, ina maana kwa mie mwenye diploma na degree ningekula extra ya 1.7M ama nini? 😅

Kweli jeshini raha aisee dah
 
Back
Top Bottom