Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Uongo mtupu,kuna jamaa namjua aliacha Tanesco alikuwa analipwa kilo 8 per month ,na kuna jamaa niliona slip yake kwa mwezi anakula 35m kampuni binafsi na pia kuna mabwana wadogo kibao wanalamba 6m mpaka 15m kwa mwezi kwenye makampuni binafsi na haujayataja kabisa.
😋😋
 
Wakuu huu ndo mtiririko wa taasisi za serikali zinazolipa unono na zenye maslahi makubwa kwa watumishi wake

1. TPDC
2. TCRA
4. Ngorongoro
3. Ewura
4. WCF
5. TBS
5. TANAPA
5. Tume ya madini
6. Mamlaka ya chakula na dawa
7. SSRA
8. NSSF/PSSSF
9. BOT
9. Bunge
9. Ofisi ya mkemia mkuu wa serikali
10. TASAC
10. TRA
11. MSD
11. TAKUKURU
11. EGA
12. NHIF
13. TPA
13. TIC
14. KADCO
15. TANESCO
16. TANROAD
17. TAA
Hakuna wizara hata moja hapo, inamaana wizarani ni njaa tu 😅
 
Kuna baadhi ya sehem umepatia ila kwingine umekosea ndo maana nikatoa mfano kuwa mfano kuwa kama wewe umesomea bsc pharmacy na mm nikasoma Md na tukaajiriwa sehem moja md atakuwa na mshahara mkubwa kuliko pharmacist

But mfano huyu pharmacist akaajiriwa kwenye parastatal organization ie TFDA ataanza na mshahara mkubwa kuliko pharmacist ambae kaajiriwa na serikali kuu(halmashauri)
Mfano Md akiajiriwa halmashauri huwa ana mshahara wa kati ya 1.4-1.5
Ila Md huyu huyu kama angeajiriwa Kwenye parastatal organization kama muhimbili angekuwa na mshahara zaid ya 1.5m


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu halimashauri sio serikali kuu
 
Mkuu, sometimes Ni lazima kuachana na fantasies na kuishi kwenye uhalisia.

Hata mbunge wa Tanzania analipwa Tsh 15,000,000 tunalalamika. Je, hiyo 15M kwa mwezi Ni pesa kubwa?

Hivi unajua hiyo Tsh 15M Ni $6,000 tu!!

Mkuu wa Idara Halmashauri analipwa That 3M. Unajua hii Ni USD 1,300.

Maisha hayajawahi kulingana hata siku moja. Ukitaka uone Maisha magumu,.kuwa my wa kukosa shukurani au kuona kama dunia haikutendei haki JILINGANISHE na walio juu yako.

Mbona hujilinganishi na unaowazidi??

Kwa mishahara ya serikali kuu, MD ndio anaanza na mshahara mkubwa na hiyo Ni FACT.

Achana na stori zaashirika sijui Nani anapata Milioni 30 kwa mwezi. Hata kama wapo ni watu wangapi.wanalipwa hivyo?

Ndio maana hata wabunge wetu wakijilinganisha na Kenya wanaona wanalipwa pesa ndogo sana na wao wanadai kuongezewa mishahara.
Kwann figure unaweka kwa usd??
 
I wish mgejua kuwa Hela imelala kwa biashara ,Nina mkaka nliimpa line mwaka uliopita alikuwa anaslave kwa halmashauri na vichenchi visivyo na maana Leo hii ana range 2022 edition
Kuna mdada pia najuana naye ,siyo mwajiriwa Ila ukitaka services zozote serikalini atakufanyia mind you hajasoma chuo kikuu ,mwana biashara tu .
Hela wanazokunja hawa sio mchezo .
Naijua hiyo .... watu wa kalynda na Q net
 
Kama unafanya kazi kwenye taasisi ambayo haiingizi pesa serikalini kazi yake inategemea kupewa pesa kutoka serikalini kamwe haiwezi lipa wafanyakazi wake mshahara mnono ,mfano angalia
TRA
TPA
TANAPA
DAWASA
Hawa wote wanaiingizia mapato serikali ndio maana mtaani wanavimba kwa kulipwa mishahara mikubwa,sasa wewe kajichanganye ufanye kazi kwenye taasisi za kutegemea mpaka wapewe fungu kutoka serikali kuu kudadadek utabaki kulia njaa hivyo hivyo na mikopo ya kausha damu juu kama
Temesa
Halimashauri
Sido
 
Back
Top Bottom