Hizi ndizo nguvu na uwezo wa Ajabu aliokua nao Adam baada tu kuumbwa

Hizi ndizo nguvu na uwezo wa Ajabu aliokua nao Adam baada tu kuumbwa

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
9,397
Reaction score
12,415
NGUVU NA UWEZO WA AJABU WA ADAMU

Adamu, akiwa kiumbe wa kwanza kabisa kuumbwa na Mungu, alipewa mamlaka makubwa na uwezo wa kipekee juu ya viumbe wote wa duniani. Tofauti na wanadamu wa leo, Adamu hakuwa na hofu wala upungufu wa nguvu. Biblia inasema:

“Kisha Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na dunia yote pia, na kila chombo chepote kitambaacho juu ya nchi.” (Mwanzo 1:26)

1. Uwezo wa Kuwa Karibu na Viumbe Vyote Adamu aliishi bustanini Edeni akiwa rafiki wa wanyama wote. Kwa mluzi tu au ishara ndogo, aliweza kuwaita wanyama wote na wakamtii bila upinzani. Alikuwa na lugha ya kipekee ya mawasiliano na viumbe wote hii ni nguvu ambayo sasa imepotea kwa wanadamu. Adamu hakuwa na hofu ya simba, chui, au mnyama yeyote; wote walimtii.

2. Alikuwa na Nguvu za Ajabu Adamu aliumbwa akiwa mkamilifu kimwili na kiakili. Aliweza kushika hata tembo au mnyama mkubwa bila tatizo, na nguvu zake zilitokana na kutokuwepo kwa dhambi na mauti. Hakuwa na magonjwa, uchovu, au udhaifu kama walivyo wanadamu wa sasa. Kila kiungo cha mwili wake kilifanya kazi kikamilifu na kwa ufanisi mkubwa.

3. Uwezo wa Kumwona Kila Kiumbe (Wakiwemo wa kiroho) Adamu alikuwa na macho ya rohoni na ya kimwili yaliyoweza kuona hata viumbe wa kiroho. Ndiyo maana alipomwona nyoka (ambaye shetani alikuwa amejificha ndani yake), aliweza kuzungumza naye bila kushangaa. Kabla ya dhambi, kulikuwa hakuna kizuizi kati ya ulimwengu wa kiroho na wa mwili. Adamu alikuwa na ufahamu mpana wa mambo yote aliona na kuelewa vilivyo mambo ya rohoni na kimwili.

4. Uwezo wa Kuwapa Majina Viumbe Wote Mungu alimleta kila mnyama mbele ya Adamu ili ampe jina. Hii ni ishara kwamba alikuwa na hekima na akili ya ajabu. Majina aliyoyatoa yalilingana na asili ya kila mnyama (Mwanzo 2:19-20).

Nguvu na uwezo huu vilitokana na ushirika wa moja kwa moja na Mungu na kutokuwepo kwa dhambi. Baada ya anguko la dhambi, nguvu hizi zilipungua na hatimaye mwanadamu akawa dhaifu, mwenye hofu, na asiye na mamlaka kama zamani. Lakini hadithi ya Adamu inatufundisha kwamba mwanadamu aliumbwa kuwa juu ya viumbe vyote na anaweza kurejeshewa nguvu za rohoni na mamlaka kupitia uhusiano wa karibu na Mungu.

Fahamu kwamba mwanadamu wa kwanza alikuwa na uwezo mkubwa kuliko tunavyoweza kufikiri. Hivyo, kila mmoja wetu anapaswa kutamani kurejesha ule ushirika na Mungu ili kurudishiwa hekima, ujasiri na mamlaka katika maisha yetu ya sasa.
 
Naomba kujua,. Kabla ya dhambi, simba alikula nini? Achana na fisi, mamba, chui n.k
Soma hapa mwanzo mpaka mwisho utapata jibu kwenye mstari wa 29 hadi wa 31.

Mwanzo 1:
19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.

20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.

21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.

23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.

24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.

25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;

30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.

31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
 
Haiwezekani
Kila jambo linawezekana ni kujenga uwezo wa kuelewa na kuamini.
Ukitumia milango mitano ya fahamu hakuna jambo lolote ambalo halionekani litaweza kuwezekana katika maisha.

Ukiongeza mlango wa sita wa fahamu (imani) ndipo sasa utaweza kuelewa kila jambo na mambo yote yatawezekana.
 
Sawa mkuu
 
Soma hapa mwanzo mpaka mwisho utapata jibu kwenye mstari wa 29 hadi wa 31.

Mwanzo 1:
19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.

20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.

21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.

23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.

24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.

25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;

30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.

31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
Kwahiyo tunakubaliana kwamba kifo kilikuwepo hata kabla hawajatenda dhambi
 
Kwahiyo tunakubaliana kwamba kifo kilikuwepo hata kabla hawajatenda dhambi
Ni wapi wameandika kifo kilikuwepo? Biblia ni kitabu kikubwa sana kina majibu yote unayo hitaji. Unapokisoma. Tumia principle of context utakielewa vizuri.
 
Ni wapi wameandika kifo kilikuwepo? Biblia ni kitabu kikubwa sana kina majibu yote unayo hitaji. Unapokisoma. Tumia principle of context utakielewa vizuri.
Simba alikuwa anakula nini? Umejibu kwa andiko refu ilhali jibu ni dogo.

1. Alikula matunda?
2. Alikula nyasi
3. Alikula magome ya miti?
4. Alikula nyama?
 
Kuna wajanja wajanja wanasema binadamu wa kwanza alikuwa sokwe🤔🤔
 
Simba alikuwa anakula nini? Umejibu kwa andiko refu ilhali jibu ni dogo.

1. Alikula matunda?
2. Alikula nyasi
3. Alikula magome ya miti?
4. Alikula nyama?
Sasa kama unashindwa kusoma mistari michache hivyo miepesi utaweza kusoma vitu vigumu mkuu?
 
Walimuumba Adam kwa mfano wao, Adamu ni mwanaume.

Hivyo kuna Mungu zaidi ya mmoja?

Na wote wanaume?

Hii Idea ya Eva ilitoka wapi au kati hao Miungu kulikuwa na mwanamke?

Iluwachukua siku ngapi kuamua kumuumba Eva?

Na kwanini hawakumuumba Eva kama walivyomuumba Adamu, badala yake wakamlaza Adam na kumtoa nyama ubavu wa kushoto na kumuumba Eva?

Au walipungukiwa material za uumbaji?
 
Back
Top Bottom