Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 9,397
- 12,415
Unafikiri atakujibu nini mkuuNaomba kujua,. Kabla ya dhambi, simba alikula nini? Achana na fisi, mamba, chui n.k
Soma hapa mwanzo mpaka mwisho utapata jibu kwenye mstari wa 29 hadi wa 31.Naomba kujua,. Kabla ya dhambi, simba alikula nini? Achana na fisi, mamba, chui n.k
Nilisha mjibu biblia ina majibu yote.Unafikiri atakujibu nini mkuu
HaiwezekaniNilisha mjibu biblia ina majibu yote.
Kila jambo linawezekana ni kujenga uwezo wa kuelewa na kuamini.Haiwezekani
Alikula Yanga😅Naomba kujua,. Kabla ya dhambi, simba alikula nini? Achana na fisi, mamba, chui n.k
Sawa mkuuKila jambo linawezekana ni kujenga uwezo wa kuelewa na kuamini.
Ukitumia milango mitano ya fahamu hakuna jambo lolote ambalo halionekani litaweza kuwezekana katika maisha.
Ukiongeza mlango wa sita wa fahamu (imani) ndipo sasa utaweza kuelewa kila jambo na mambo yote yatawezekana.
Kwahiyo tunakubaliana kwamba kifo kilikuwepo hata kabla hawajatenda dhambiSoma hapa mwanzo mpaka mwisho utapata jibu kwenye mstari wa 29 hadi wa 31.
Mwanzo 1:
19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.
20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
Ni wapi wameandika kifo kilikuwepo? Biblia ni kitabu kikubwa sana kina majibu yote unayo hitaji. Unapokisoma. Tumia principle of context utakielewa vizuri.Kwahiyo tunakubaliana kwamba kifo kilikuwepo hata kabla hawajatenda dhambi
Simba alikuwa anakula nini? Umejibu kwa andiko refu ilhali jibu ni dogo.Ni wapi wameandika kifo kilikuwepo? Biblia ni kitabu kikubwa sana kina majibu yote unayo hitaji. Unapokisoma. Tumia principle of context utakielewa vizuri.
Sasa kama unashindwa kusoma mistari michache hivyo miepesi utaweza kusoma vitu vigumu mkuu?Simba alikuwa anakula nini? Umejibu kwa andiko refu ilhali jibu ni dogo.
1. Alikula matunda?
2. Alikula nyasi
3. Alikula magome ya miti?
4. Alikula nyama?
Hivi ndivyo tumelelewa kwenye dini. Mtu akihoji swali inabidi kumpoteza iwapo jibu lina mkanganyikoSasa kama unashindwa kusoma mistari michache hivyo miepesi utaweza kusoma vitu vigumu mkuu?
Mkuu mbona husemi alikuwa anakula nini? Tafadhali jibu kwa kifupi tu chakula cha simba /wanyama walao nyama kilikuwa nini?Sasa kama unashindwa kusoma mistari michache hivyo miepesi utaweza kusoma vitu vigumu mkuu?
Soma lile andiko pale limeeleza walikua wanakula nini. Andiko linaeleweka.Mkuu mbona husemi alikuwa anakula nini? Tafadhali jibu kwa kifupi tu chakula cha simba /wanyama walao nyama kilikuwa nini?
Simba alikuwa anakula nini? Umejibu kwa andiko refu ilhali jibu ni dogo.
1. Alikula matunda?
2. Alikula nyasi
3. Alikula magome ya miti?
4. Alikula nyama?