Nehemia Kilave
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 1,414
- 3,118
Habari JF ,Binafsi nimefanya kazi na NHIF kwa zaidi ya miaka 5, kumekuwa na Changamoto nyingi ambazo zinapelekea huduma kupitia huu mfuko kudolola.
Mambo haya nimefuatilia ndio chanzo kikubwa ya Changamoto :-
1. ELIMU DUNI KUHUSU MFUKO WA NHIF (hupelekea matumizi yasiyo sahihi na kudhohofisha mfuko ), wanufaika wengi sana hufikiri ukiwa unakatwa hela basi ni lazima utibiwe hivyo kadi zikikaa sana basi atalazimika kuchukua hata familia nzima au kuwapa hata majirani waende hospitalini kupata matibabu .
Ukweli ni kwamba Matibabu ni gharama sana fedha kidogo tunazo katwa hazitoshi kugharamikia hivyo kinachofanyika kwenye mfuko ni COST SHARING - kipindi wewe mwaka mzima hauumwi ujue kuna mtu kila mwezi anapata matibabu ya zaidi ya laki 2 na anakatwa 22,000 tu . Hivyo mfuko ni wa kuulinda sana kuepuka matumizi yasiyo sahihi au yasiyo ya lazima maana hata wewe kuna siku utatibiwa kwa zaidi unachochangia .
2. HELA YA KUMUONA DAKTARI , Katika madai mengi pesa kubwa inakwenda kwenye hii sehemu hivyo kuna haja ya kupitia na kuona itawekwaje ili isimuumize mnufaika na mtoa huduma ,kama itawezekana basi mfuko uchangie matibabu consultations alipie mnufaika (Maamuzi magumu ) .
3.MATUMIZI MAKUBWA YA PESA ZA MFUKO MAOFISINI -NHIF, Mikopo, Mishahara, Posho na safari nyingi zinazofanywa na watumishi wa NHIF ni mzigo kwa mfuko.
NHIF inatakiwa ije na Technologia zitakazo rahisisha kazi na kudhibiti ubadhilifu - watumishi waumize vichwa
Mfano -NHIF ije na mfumo wake yenyewe ambao hospitali zitautumia uonyeshe mgonjwa anatibiwa nini, mara ya mwisho alitibiwa wapi alifanya kipimo kipi na alipewa dawa zipi na Daktari X aone matibabu ya kituo Y kuepuka kurudia madawa .
Nadhani kama NHIF itasolve haya mambo kuna Changamoto zitapotea.