Hizi ndizo sababu kuu 3 kwanini mfuko wa NHIF unapitia changamoto nyingi katika kuhudumia wananchi

Halafu unakuta mume akatwa, mke akatwa, mkwe akatwa lakini member akienda kupata huduma aambiwa dawa hizo hazipo kwenye NHIF [emoji2356][emoji2356]

Inakera nyie!

Yaani mtu atoe Hela yake bank akanunue dawa wakati anachangia Hela chungu nzima yeye na mkewe/mumewe achilia mbali mkwewe?!

Ufalme wenu utafitinika tu kwa namna hiyo.

You will not be established.
 
Halafu vipimo vingi na dawa za uzazi havimo kwenye package ya NHIF , Kwanini?
 
Hiyo inategemea na aina ya package



Ni package ipi au vigezo gani vitamfanya mwanachama kuwa anapata ful service hadi vipimo na dawa za uzazi?

Kuna watu nawajua wako taasisi ambazo mshahara wao si haba Yaani wachangia mfuko Hela nyingi kila mwezi kila Mwaka na mume wake lakini wakienda hospital wanaambiwa vipimo hivyo havilipiwi na NHIF wala dawa [emoji848][emoji848]

Wanakereka mpaka basi.

Na inawabidi wakachukue Hela bank walipie wakati wameshakatwa Hela nyingi na NHIF!
 
Mbona matumizi ya fedha ya mfuko ni ya holela sana hilo halisemwi
 
Hii pointi ya 3 ni mzigo sana mfano ofisi moja unakuta inahidumia wilaya 2 ama 3 hapo gharama za kila siku lazima zitakuwa kubwa
 
ukiwa na standard package na supplementary packages unapima . Vifurushi kam NAJARI ,WEKEZA na TIMIZA hapo utalazimika kulipia .
 
.
Kati ya watu waliiongea point, ni wewe. Tatizo kubwa la waafrika ni UBINAFSI. Hakuna tatizo kubwa zaidi ya hili, HAKUNA. Matatizo yote yanatokana na tatizo hili. Imagine hata vijana ambao hawajapata kazi serikalini tayati wana mentality za kupiga, sasa wakipata nafasi unategemea nn?!
.
Dawa ya ubinafsi: Zitungwe sheria kali kwa wanaofanya ubadhirifu wa mali za umma mfano kunyongwa, vifungo vya maisha, kufilisiwa, n.k.
.
Afrika isipofanya hayo, hatutakaa tuendelee...never ever ever!
 
Dawa ya ubinafsi: Zitungwe sheria kali kwa wanaofanya ubadhirifu wa mali za umma mfano kunyongwa, vifungo vya maisha, kufilisiwa, n.k.
.
Afrika isipofanya hayo, hatutakaa tuendelee...never ever ever!
Tukifanikiwa kutunga sheria hizi hakika tutaenda mbali sana.
 
Nadhani katiba mpya ni muhimu sana
 
Magufuli ndio alivuruga mfuko wa hifadhi ya jamii kwa kuchota hela huko na kupeleka kwenye ujenzi wa madaraja. Kinachofanyika sasa ni kufidia fedha zilizochukuliwa kibabe na awamu ya 4 na mama ni mhusika pia.
 
Mifuko imechotwa na Kikwete pia. Ujenzi wa Hospitali Dodoma fedha zilitoka NHIF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…