Hizi ndizo Sababu kuu 4 za Ufisadi Tanzania

Sawa umeongea vyema ila kuhusu elimu duni nakataa maana hao wanaiba wanatumia elimu kubwa kuiba kabla mamlaka za juu kujua ...

Mm ninachoona ni malezi, na jamii ndio shida ...mtu anayeiba million of tsh. Jamii inamchukulia kuwa mjanja na ametoboa na anapata heshima zaidi na zaidi mtaani..tofauti na nchi za nje mwizi wa mali za umma ni fedhea kubwa kwa jamii na unatengwa kabisa...
 
Nchi za africa kunakitu tunacho hubiriwa na wazungu kuhusu democrasia,na haki za binadamu,hii slogan ndio kwanjia moja ama nyingine inaturudisha nyuma sana.

Mtu anapiga ufisadi kwa mabilioni alafu mambo yanaisha juujuutu!!!, daah.
Ufisadi hauwezi kwisha kwa kuwa na sheria za kuchekeana chekeana.
Tutaumizwa mbaka mwisho.

Dawa niku copy na ku pest sheria za nchi kama china ndio heshima itakuwepo kwenye matumizi ya kodi zetu.
 
Mkuu Tamaa kila sehemu zipo ila kuna vitu vinaweza fanya watu wasiibe
 
Ongeza na hoja ya uwepo wa royal families kama za akina Mwinyi, Karume, Kikwete and the likes
 
Hivi ilitumika hoja gani au hekima gani kufanya hawa viongozi wapewe hivyo vitu bure? Yani Mimi mwananchi kipato changu kidogo hata kulipia huduma za matibabu hospitali ni mtihani ila kiongozi huko si tu kwamba ana mshahara mnono wa kumudu kuishi vizuri na familia yake ila yeye anatibiwa bure, usafiri bure, makazi bure na mengineo na bado analipwa mshahara.

Binafsi sijawahi kuelewa tija yake.
 
Tatu
3&4 sio kweli,umaskini sio chanzo Cha Rushwa,sio cause ni effect,ni matokeo ya nchi kuwa na Rushwa,kiasi kwamba huduma za jamii,afya,Elimu ajira,hazipatikani hapo ndio umaskini unatokea
 
Ndio hapo ujue kama serikali inatuchukulia watanzania oya oya saana
 
Watanzania kila mtu akishateuliwa mkuu fulani,kiongozi fulani kitu cha kwanza anataka awe bilionea
Hata umlipe mshahara mln 20 hatotosheka!

Ova
 
Hao Graduates unao Wasema ndio hao wanashinda vijiweni kujadili Simba na Yanga Diamond Harmonize Wanawake Pombe na Bangi hata wakipata Ajira Akili ndio hiyo hiyo
 
Namba 1 itoe, nyingine upo sawa
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hao Graduates unao Wasema ndio hao wanashinda vijiweni kujadili Simba na Yanga Diamond Harmonize Wanawake Pombe na Bangi hata wakipata Ajira Akili ndio hiyo hiyo
Sahihi
 
Sahihi
 
Jambo la kwanza la kuondoa ufisadi nchini ni kubadilisha chama bila kujali kuwa ni mtu gani atakuwa mgombea kwa chama hicho ili kuwe na CHECK AND BALANCE katika utawala,kwa maana chama hiki kinapoondolewa kwa kura halali hujishauri ni wapi tuliwakosea wananchi na kujisahihisha katika mapungufu yale waliokuwa nayo.
 
Nakusikia pia nakubaliana na wewe 100% ! Lakini umeanzia kwenye matawi ya mti; umeacha mizizi ya tatizo ambayo ni AINA na KIWANGO cha ELIMU ambayo MTANZAI wa WASTANI anayo hivi sasa, hasa OPINION MAKERS. Hayo ndiyo msingi wa matatizo au mafanikio ya jamii yo yote tangu wakati wa Socrates na Plato! Kama huamini, sikiliza hoja za Mawaziri na Wabunge wakiwa Bungeni kisha pima wastani wa KIWANGO chake! Safari itakuwa ndefu bila mapinduzi ya aina fulani katika Elimu kuanzia ngazi ya Chekechea!

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Hii point imeingia akilini kweli kweli mwizi katika mitaa yetu ndiyo mjanja na mwenye akili kwa sababu tu ametoboa maisha,hivyo ufisadi kwa jamii zet za kiafrika ni halali na baraka kwa jamii inayokuzunguka.
 
Namba 6 iwe Na. 2 tena wengine walianzishwa maalum kabisa kututetea WANANCHI na maadui wa ndani na nje bila kujali adui wa ndani ni kiongozi au si kiongozi, sina hakika kama hawajui majukumu yao au teuzi hata baada ya kustaafu ndio zinawaondolea uwezo wa kufikiri..mfano Angola Rais wa sasa alikuwa mwanajeshi alipoingia akawabadilikia waliomsaidia kuwa Rais including Rais mstaafu..nchi inahitaji watu wa aina hii.
 
Watanzania wengi pia wana mitazamo ya kale "conservatives" kupita kiasi wasiopenda mabadiliko. Ni vigumu kuendelea ukiwa katika hali kama hiyo hasa kama nchi ina rasilimali ambazo zinahitaji innovation kubwa kuwa na faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…