covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 6,967
- 17,452
Sawa umeongea vyema ila kuhusu elimu duni nakataa maana hao wanaiba wanatumia elimu kubwa kuiba kabla mamlaka za juu kujua ...Habari Wana JF,
Ufisadi Tanzania sio kitu kigeni nimekaa kwa kipindi kirefu, nimefanya Utafiti usio rasmi nimegundua kuna vitu vinne ambavyo vinafanya uendelee kuwepo kama Ifuatavyo:
1. KATIBA, kwanza haina makali pili viongozi wengi hawawajibiki kwa Wananchi, wanafanya kazi kwa ajili ya mamlaka ya Uteuzi sio wananchi. Hivyo tunahitaji katiba mpya.
2. CCM, chama hiki kina watu wengi ambao wako kwa ajili ya maslahi yao tu kibaya zaidi wana mizizi mikubwa sana suluhisho ni kukitoa kwa namna yoyote ile .tatizo ni nani wa kumpa
3. UMASKINI, wananchi wengi ni maskini sana hivyo moja wako bize kutafuta kula yao kuliko mambo ya Taifa pili wanapoteza ujasiri na uthubutu wa kuweza kuhoji mambo yanayoendelea, kikubwa wanajawa hofu.
4. UDUMAVU WA AKILI, nimefuatilia nimegundua Watanzania wengi walipata shida ya afya ya akili sababu kubwa nikapata ni lishe duni wakiwa watoto ,Ndio maana watu wanapiga pesa watu
Hivyo kuna haja ya kutafuta suluhisho la hivi vitu ili Nchi iwe kuendelea.
Mm ninachoona ni malezi, na jamii ndio shida ...mtu anayeiba million of tsh. Jamii inamchukulia kuwa mjanja na ametoboa na anapata heshima zaidi na zaidi mtaani..tofauti na nchi za nje mwizi wa mali za umma ni fedhea kubwa kwa jamii na unatengwa kabisa...