Hizi ndizo sababu za kutopokea simu za baba yangu mzazi

Hizi ndizo sababu za kutopokea simu za baba yangu mzazi

Kwanini usipokee tu? Kama huna mueleze tu ukweli kuwa huna, kuwa muwazi.

Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani. Heri ndyo baraka. Ukijiweka mbali nao utajiweka mbali na baraka na mafanikio.
Mkuu kuna maneno unaweza ukaambiwa unajikuta weww mwenyewe unaenda kukukopa.pesa ili uwape hom

After that unaanza ishi maisha ya ajabu ajabu
 
We bwana mdogo churaa,, na ukiendekeza kumkwepa mzee wako nakwambia hutoboi walah na utazid kuhangaika mpaka utajinyongo dogo ngoja nikwambie kitu mwenyewe nishawah pitia hilo jambo tena niliwah kumzaba na makofi na baba yangu huez amin niliteseka sanaa siku niliporudisha moyo na kuomb msamaha mzee akanisameh na ndipo mambo yakaanza kufunguka oya churaa elewa neno kwamba wazaz ni miungu wa pili mbona simpo tu kwann unafanya moyo kuwa mgumu kama wa farao churaa
 
We bwana mdogo churaa,, na ukiendekeza kumkwepa mzee wako nakwambia hutoboi walah na utazid kuhangaika mpaka utajinyongo dogo ngoja nikwambie kitu mwenyewe nishawah pitia hilo jambo tena niliwah kumzaba na makofi na baba yangu huez amin niliteseka sanaa siku niliporudisha moyo na kuomb msamaha mzee akanisameh na ndipo mambo yakaanza kufunguka oya churaa elewa neno kwamba wazaz ni miungu wa pili mbona simpo tu kwann unafanya moyo kuwa mgumu kama wa farao churaa
😂😂😂😂😂😂
Mwanangu mi sio chura bob..

We jamaa ulimpiga baba ako vibao we jamaaa shaitwani kabisa
 
Ulimwengu una jinsi au namba ambayo huitumia kuwasiliana na mtu. Na moja ya njia hizo nikupitia ndogo, kila unachota kina maana katika maisha yako ya kawaida

Na hakuna mtu anayeweza kukufumbulia fumbo la ndoto uliyoota wakati wewe mwenyewe majibu unayo....

Majibu ya ndogo yako, yako katika maeneno uliyoyaandika hapa.
Sijaelewa kabisa mkuu nielekeze
 
Kukaa mwezi mzima bila kupokea simu ya baba kutazidi kukutengenezea deni la Nafsi, kila simu yake anayo piga na hauipokei, inakuongezea uzito wa hatia kichwani mwako.

Wazazi wengi age go wanakuwaga kama watoto, akikipigia simu, mara nyingi utakuta anahitaji tu kusikia sauti yako mtoto wake ili ajue upo salama na unaendelea vizuri, pesa ni ziada, ingawa kwa mazingira yetu ya kitanzania ni hitaji.


Usisubiri mpaka upate pesa au mpaka uonane na mtu wa kukwambia fanya moja mbili tatu ndo umtafute, vunja Ukimya kwa kumtumia hata meseji kama huwezi kuongea naye kwa sababu ya hofu uliyo nayo labda atakulaumu, itampunguzia yeye wasiwasi (kwamba labda umekufa au umemkataa) na itakupunguzia wewe pia hali ya kuhisi hatia.



Ndugu yangu maisha ya sasa ni magumu kwa kila mtu, na kusoma sio tiketi ya kupata kazi hapo hapo, kuwa mkweli kwa mzee wako ukiwa hauna mwambie mzee leo sina hata mia ukweli humuweka mtu huru kuliko kuwa kimya ukizidi kujiumiza mkuu.


Kwa sasa kwa kuwa hauna permanent source of income, punguza kamari au achana nayo kwanza kwa sababu itazidi kukuongezea msongo wa mawazo, kwa sababu unacheza ukiwa na presha ya kutaka kutatua matatizo ya nyumbani, hii inakufanya upoteze umakini wa kutafuta fursa za kudumu.

Pole sana kwa changamoto mkuu, Mwenyezi Mungu azidi kukukitia nguvu katika wakati huu mgumu unaopitia.
Amen ameeen ameeen mkuu
Shukurani sana mkuu kwa ushauri wako.

Kuhusu kupunguza kubet ntajitahidi kabisa ila daaaah aiseee
 
Ifike nyakati mue na ustaha wa kauli zenu mtu anaomba tumpe heads up wew unaanza kuponda uandishi wake rubbish 🗑
Jamaa ana mambo ya ajabu sana.
Hadi me nimemshanga why kaanza kusema vile
 
Bro, unakosea sana kufanya hvy kwa baba ako.

Ongea nae, muweke wazi yale unayopitia lkn sio kumpuuzia.
Mwambie ukiwa nayo utampa, usipowa nayo bc awe mpole.
Takbir...
Mkuu hapa nimetoka ongea nae leo jioni daaah mkuu acha kabisa kikubwa kasema ananiombea dua
 
Naumia sana, umeongea kwa hisia
1. Naomba usije jiongezea majukumu kwa sasa kwa kuoa
2. Nenda nyumbani muone babako mwamby ukweli kuwa haujapata chochote
3. Mambo yako mengi yamejifunga kwa sababu umejitenga na mzazi wako, rudi nyumbani hata mara moja, muone, akutemee mate, akupe mkono wa baraka, ongea naye kiundani..hakafu rudi ukapambane
4. Jitahd kuongea na wazazi wako, unavyowafungia mlango ndivyo na baraka zako zinajifunga
5. Sali kwa imani yako na kwa roho na kweli maana mzaliwa kwanza kuna changamoto

NENDA KWENU ULIKOZALIWA KAFANYE IBADA ZENU, KAAGE NYUMBANI HALAFU RUDI NAKUAMBIA MAMBO MENGI YATANYOOKA

achana na uanaharakati wa ki gen z, miaka inasogea..kaage kwanza home
Mkuu kusema kurudi mbeya uwongo..
Ila upande wa mama nipo nae vizuri sana kabisa huyu mama kila siku naongea nae..

Nilichogundua pia kutengana kwa wazazi inaweza kuwa ni chanzo cha mtoto ku base upande mmoja
 
Pole mkuu...
Me nmeingia mbeya leo kama bado upo southern,njoo pm nikupe contact tuonane kesho pengine tutapata pa kuanzia kwa pamoja
 
Back
Top Bottom