Hizi ndizo shughuli zinazowapeleka Wachagga Kilimanjaro kila mwaka

Hizi ndizo shughuli zinazowapeleka Wachagga Kilimanjaro kila mwaka

Natumai wote wazima.
Huu ni mwezi wa mwisho wa mwaka
Mwezi ambao unapilika nyingi sana za kumalizia dk za mwisho.

Kuna makabila mengi sana yanayopenda kuumalizia mwezi huu kwa kwenda makwao yaani sehemu walikozaliwa.
Nitazungumzia Wachagga sababu mi mwenyewe natokea huko.

Sababu za kwenda makwao December.
1. Kupumzika,hii ni baada ya kufanya kazi kwa mwaka mzima,bila kwenda.
2. Kuchinja mbuzi, hapa kuna za matambiko na za kawaida. Matambiko haya ni kushukuru wazee wao kwa baraka walizopata kwa kipindi chote.
3. Sherehe mbalimbali. Komunuo, kipaimara, ubatizo,Xmas na mwaka mpya wenyewe.
4. Utambulisho mbalimbali kama mke, mchumba,gari jipya,nyumba mpya n.k
5. Kukutana na watu mbalimbali ambao hamuonani baada ya kipindi hicho kama, classmates, majirani,ndugu na jamaa.
6. Utekelezaji wa miradi mbalimbali kama ujenzi wa nyumba, ukarabati wa nyumba,njia mashamba n.k

Kutokana na sababu hizo wanaokwenda ni watu wote wa dini zote

Ukienda tofauti na kipindi hiki huwez kukuta watu wengi sana. Kipindi hiki hakuna kaya utakayokuta haina furaha.

CHANGAMOTO
Kama umeenda na huna chochote kitu,utakumbana na ubaguzi na manyanyaso makubwa sana labda usiwe mzawa wa hapo.
Vijana wenzako wanawajengea wazazi wao nyumba ww huna kitu,wameenda na magari ww huna kitu. Umeshindwa hata kujenga choo hapo nyumbani!!!???

Maswali fikirishi
Utaulizwa mjini ulifata nini??bora ungelima hata huku shambani tu tujue kabisa kweli huna kazi?
Kama ni Dar, utaulizwa kwani Daslama unayokaa wewe ni hiyo hiyo anakaa mtoto wa Massawe?[emoji23][emoji23] Utajibu nini hapo?
Kipindi hicho wenye vitu,mali pesa ndio wenye akili na maamuzi. Una vyeti vyako,una elimu kubwa lakini kama hujafanya chochote au hauko vizuri na wazazi wewe ni takataka tu.

Kwa sababu tajwa hapo juu kumbuka sio wote wanakwenda kwa sababu zote bali lazma sababu mojawapo ihusike.
Ni kipindi chenye shangwe na furaha sana.

Karibuni watu wa maeneo mengine mtupe sababu za kwenda na changamoto zake. Ruksa kujazia pia hapo.
Twendeni tu kwetu, hawa wa mikoa mingine waacheni waendelee kushangaa sio utamaduni wao mangiii

NB
Kama hujajipanga usiende maana hutakua na majibu ya maswali tajwa hapo juu
 
Kuna yule mchaga wa Arusha tena mzee wa Kanisa KKKT alikuwa analala na chatu chumbani kwake.

Siku alipojisahau akasafiri bila kufunga mlango chatu likatoka nje wananchi wakaliua na utajiri wa bwashee yule ukaishia pale pale.

Wachagga, Wakinga na Waha utajiri wenu mnauweza wenyewe!
Wewe kama unawasema wakinga kupitia Wachagga utajua mwenyewe
 
Naomba niwaite maswahiba zangu hapa tuanze kuria mbege...

Le Big Sam Babu Asprin aka mzee wa without [emoji28]

Brudha wa Verossa Mentor aka baba naniliu .....[emoji12]

Sukari ya warembo Watu8 aka Msafiri wa Nissan nyeupe [emoji2957]

Niko Lushoto huku hadi tarehe 18, tarehe 19 nateremka atayekuwa anaelekea kaskazini zaidi atoe taarifa mapemaaaa niongeze chupa za wine [emoji485] [emoji39]
Upo Lushoto sehemu gani madam? Maana nami nipo Lushoto kwa kazi fulani kabla ya kurejea mjini Daslam January.
 
Back
Top Bottom