Niko hapa kituo flan cha daladala
Basi pembeni yangu Amekaa mkaka nadhifu sanaaa anaonekana mwenye sura ya HeLa na hata hapo kituoni sijui hata anafanya nini.... Ila anaonekana mwenye stress Sana hadi anaongea kama mtu anayekaribia kutoa machozi.
Kaka huyu mrefu maji ya kunde nzuri, mwenye sura na maongezi ya upolee yuko busy anaongea na simu....
Anaonekana anaongea na mshkaj wake anamuelezea Mambo ya familia yake.... Yaani anasema hapo alipo hajui hata anaenda wapii Ila hawezi Kurudi nyumbani kwa Yule mwanamke maana anaweza kumpasua akamuua akapata kesii. Bora akae kituo cha daladala.
Badae nkamsikia anasema ".....basi ngoja nichukue daladala nikufwate Nije huko Mara Mia ....". Akadandia daladala huyooooo akatokomea na gari ya bunju.
Sasa jamani mnaishi na Simba ndani kwamba Bora ukae kituo cha daladala kuliko nyumba ambayo mkeo mpendwa uliyemlipia mahari huenda kubwa anaishi?? Ilikuwaje ukamuoa mtu wa hivi? Ni mhemko au?
A see ndoa zimegeuka ndoano kwa wengi Ila ishini humo Hadi mfe tuwazike.
Asanten.