Hizi ni Aina nne za ugali ninazokula maisha yangu yote , na mboga zake nakuwekea

Hizi ni Aina nne za ugali ninazokula maisha yangu yote , na mboga zake nakuwekea

gwanseri

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2024
Posts
632
Reaction score
1,831
Ugali ni Tanzania
Sima ni Zambia
Shima ni Zimbabwe
Fufu ni nchi za afrika magharibi
Bugali ni kwa wakongoman

Twende moja kwa moja ugali ni chakula Changu pendwa kama ifuatavo
Dona ambayo mahindi yameoshwa vyema , yakaenda kusagwa na muhogo uliokaushwa hapa naweza Kula na dagaa , nyanya chungu, ambayo imeungwa na karanga .

Ugali wa mtama mwekundu huu huchanganywa na muhogo kidogo au udaga mweupe hapa mboga pendwa hua ni nyama choma na kichuri na hapa pembeni mboga ya majani
Ugali wa mtama mweupe uliowekewa ngano kidogo hapa hua napenda na samamki choma au samaki mbichi aliyeokwa na vitunguu maji vingi

Ugali wa muhogo huu UWE ni muhogo uliolowekwa au udaga unasagwa wenyewe Tu huu naupiga na rost ya nyama au rost maini , au mchemsho wa kuku au mchemsho wa Ng"ombe ,
 
Back
Top Bottom