Hizi ni Aina nne za ugali ninazokula maisha yangu yote , na mboga zake nakuwekea

Ugali na uheshimiwe
 
Mla ugali namba moja humu ni mimi. Nabadilisha aina zote za ugali mlaini na mgumu. Kuna ugali wa mahindi dona na sembe, kuna ugali wa mtama, uwele, ulezi na muhogo. Zaidi napendelea ugali wa uwele nikila ni pasi ndefu sisikii njaa kuanzia asubuhi mpaka jioni. Ugali wa uwele unakupa nguvu nyingi mpaka nguvu za kiume shoo unapiga vema muda mrefu unafurahia penzi taratibu mashine inasoma mnara kisawasawa
 
Wameanza kuusingizia kwenye Akili ..japokuwa hawana kabisa hizo akili.

Wakaja Kujenga mwili ingali mtu ana body Kama mbuni...... tumbo, kifua na mgongo vimerundikana eneo Moja
Wakaenda mbali Zaid wakausingizia ndio chanzo Cha kuwa na sura ya Suma Jkt and yes, huo ndio uanaume Sasa.
 
Twende mbele na kurudi nyuma,ugali sio chakula
Nenda na urudi peke yako,
Umeona ugali tu,na kwanini si chakula
Nyoka na samaki jamii ya nyoka,majani,ndege nani alikuambia hivi ni vyakula na ugali si chakula?
Usiaminishwe ujinga,asiekula ugali kwa maamuzi yake ni hvyo hivyo kwa asiekula ng'ombe kwa imani ama maamuzi yake
 
Niwe mkweli...
Unakuta mtu anaponda ugali halafu anakula mihogo ya kukaanga..

Sasa anayekula ugali na mihogo ya kukaanga upi utofauti? tena hapo mla mihogo anakula na mafuta mengi...

Unakuta unaponda ugali halafu ni mlevi/mnywa pombe, sasa si bora mla ugali kuliko hayo madhara ya pombe?

Uakuta unaponda ugali halafu unakula chips na mayai ya kisasa, tomato za makopo na mayonnaise, halafu unasema ugali ni chakula cha wanyama... hapo mara mia mla ugali..

unaponda ugali halafu unakunywa vinywaji vya kusindikwa... soda, juisi za makopo, n.k

Huu ni unafiki... waacheni wala ugali.
 
Loh ugali wa ulezi na muhogo?

Nije kujaribu ugali wa uwele ...unaweka na nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…