Hizi ni baadhi ya fursa za ajira upande wa Soka ukiachana na uwezo wa kucheza mpira

Uzuri wa hizo fani soko lake ni Pana unaweza pata KAZI hadi nje ya nchi ilimradi uwe competent tu!
 
Everton ni Moja ya club zenye sera nzuri ya pesa na matumizi way back na Chelsea Abramovich ndie alijenga utaratibu mzuri wa uendeshaji
Sasa si tuwekeze kwenye maarifa halafu hayo masuala ya kupigania haki za wafanyakazi tuachie vyama vyao
Ni kama hapa bado hatuwekeza kwa wachezaji wa ndani kuinua viwango vyao na hapohapo tunataka waanze kulipwa mishahara Mikubwa inakuwa sio poa
 
Msingi wa kozi zote hizo ni kozi za awali za ukocha..km grassroots coaching na zingine zinahusu field ...ila kuna courses za management hizi huwa zinanza na diploma
 
Urefarii na ukocha unaratibiwa na vyama husika kwa kushirikiana na tff.

Mfn juzi zimeanza kozi za ukocha zilizoandaliwa na chama cha soka cha mkoa wa morogoro..hivyo kwa marefa
Yah nadhani kwa dar Chama Cha soka ubungo huwa wako active sana kwenye programme hizo
 
Point yangu ni kwamba kuwekeza kwenye michezo hata kama tusipopata hata sumni faida yake ni maradufu...., mambo ya afya..., nchi kama Brazil Timu yao ya Mpira na watu kama Pele wameweza kuitambulisha dunia nzima..., sasa hivi maisha magumu wana-siasa walaghai watu wanakwenda kwenye michezo kujiliwaza... kwahio mambo yanayoleta tija kwenye michezo ni makubwa..., lakini ndio hivyo kuna shule inapewa kibali haina hata kiwanja..., open space zinageuzwa kuwa sehemu za machinga.....

Kwahio hata mtu akitaka kuingia kwenye hizi sekta za michezo anaweza akawa na skills nyingine ambazo anaweza kufanya kazi popote hata kwenye mpira sababu unaweza ukawa nurse au MD na Dietitian vilevile Mario Sarri alikuwa Banker ila kwa upenzi wake wa mpira alikuwa anafundisha mpira part time.....

Sarri did not play football professionally, taking part as an amateur centre back and coach while working as a banker. In 2005, he had his first Serie B job at Pescara.[4] In 2014, Sarri won promotion to Serie A with Empoli, and after preserving their place in the top flight he was hired by Napoli. He won several individual awards while managing the Naples-based club; after finishing as league runners-up in 2017–18, Sarri moved to English club Chelsea, where he won the UEFA Europa League in his only season with the club. He returned to Italy to coach Juventus in 2019, with whom he went on to win the Serie A title in his first season, becoming the oldest manager to ever win the Serie
 
Karume zilizopo ofisi za tff pameshageuzwa soko utulivu WA kufundisha watoto Mpira hakuna tena ni vurugu mechi Tu hii nchi
 
Karume zilizopo ofisi za tff pameshageuzwa soko utulivu WA kufundisha watoto Mpira hakuna tena ni vurugu mechi Tu hii nchi
Watu hawajui kwamba kuna nguzo tatu katika maendeleo; Environmental, Social na Economical...

Hatuwezi tukaangalia tu kupata faranga bila sehemu za ku-enjoy hizo faranga.., na open spaces na viwanja vya michezo angalau kila wilaya ni muhimu sana..., matokeo ya kutokufanya hivyo tunaweza kulipia kwa gharama ya afya kwa wana-jamii kwa kutunza vitambi na short life span
 
Kwa dar Tu pekee yake zinatakiwa open space zaidi ya Mia mbili na sidhani kama hat 20 zimefika! Mikoani ndio kabiisa unazitafuta kwa tochi
 
Kwa dar Tu pekee yake zinatakiwa open space zaidi ya Mia mbili na sidhani kama hat 20 zimefika! Mikoani ndio kabiisa unazitafuta kwa tochi
Ajabu kuna mpaka shule eti haina hata uwanja.., yaani shule (tena primary) unatoka ghorofani unaingia mtaani - sasa hapo unajiuliza huyu dogo mwenye kipaji atakuza vipi kipaji chake ? Labda kwenye corridor za shule au kwa nadharia.....

Yaani hata ile mipango miji waliyoacha wakoloni tunazidi kuharibu na uharibifu huu utali-cost taifa kwa miaka mingi sana ijayo....
 
Ni kweli mkuu
 
Watakwambia hizo hatua za kuzingatia "quality of life" bado hatujazifikia. Watakwambia bado tuko hatua ya kusurvive na kuongeza mlo kutoka mmoja hadi miwili. Ndiyo maana mambo mengi yanayoharibu ustawi na quality ya maisha ya kila siku ya Watanzania yanafumbiwa macho kwa sababu kuna watu ambao ukiingilia ukawazuia utaambiwa bado wanapigania kusurvive. Na ndiyo angle wanayotumia kujenga miundombinu ya hali ya chini kwa kisingizio kuwa wengine nao wana mahitaji.

Hili jambo nilitaka nije niliandikie kwa upana na urefu, tatizo muda.
 
Umeniwahi kwenye jambo moja muhimu ulilosema hapa. Nadhani kabla ya yote, ili tutoke hapa tulipo neno "michezo" libadilishwe au litafutwe neno la ziada kutofautisha michezo ya kujiliwaza na michezo ya kulipwa, kama zamani walivyokuwa wanasema mpira wa ridhaa na mpira wa kulipwa, ingawa sasa hivi mstari wa kutofautisha hivi viwili umekuwa mwembamba sana. Itawasaidia wale ambao bado wanapata wakati mgumu kuelewa faida pana za kiuchumi za "michezo"

Kuna watu tena wengine wamesoma kabisa bado wakisikia mtu "anacheza" anaona anafanya jambo ambalo halina maana kiasi cha serikali au watu makini kuwekeza kwake au kumtilia maanani.
 
Ni mada zuri lakini sasa mimi, nitakua nje kidogo na mada, kwenye soka letu mfumo wetu sio mzuri pamoja na ligi yetu, kwanza niseme athira ya usimba na uyanga, imeathiri pakubwa sana, vilab vingine kukua, na ligi kuleta sura ya mabadiriko haipo, mfumo umeathiri sana kwa nchi nzima kwa mashabiki kua wapenzi wa simba na yanga tu. Mikoa na majiji, imejikuta yameshidwa kukuza club za soka vikubwa viwe kama simba na yanga. Kwa mfano majiji kama mwanza, arusha na mbeya kukosa timu asiria zenye nguvu, tofauti na nchi zingine zenye mwananchi wake wengi mashabiki soka 70%. Kama tanzania, tunataka ligi yetu soka letu na liwe na sura ya utofauti. Sisi tuwe na ligi kama za mataifa haya Morocco, england, germany, italy, argentina na brazil.
 
Mimi nimechezesha sana Ndondo back in the days. Niliitwa master ndondo.
Ukocha nililetewa gozigozi nikaacha.
Idea nyingine ni ukipata connection za Uarabuni nako kuna Ndondo huwa zinachezwa. Matajiri hutaka wachezaji.
 
Karume pamekuwaje? Sijafika pale siku nyingi. Machinga wameingia hadi pale uwanjani? Inawezekana TFF wako mbioni kuhamia Kigamboni mazima
 
Hapo si unaona alicheza kidogo na pia asingeweza
Karume pamekuwaje? Sijafika pale siku nyingi. Machinga wameingia hadi pale uwanjani? Inawezekana TFF wako mbioni kuhamia Kigamboni mazima
Uwanja umeharibika sana tena sana
 
Hapo si unaona alicheza kidogo na pia asingeweza
Kuwa kocha sio mpaka ucheze mpira na point hapo ni kwamba sababu alikuwa na passion ukocha ulikuwa part time..., hata wewe hapo unaweza ukawa na kazi yako machinga au hata daktari ukitoka kazini au weekend unawafundisha madogo mtaani ukifanya vizuri watu watakuelewa...

Moral of the story: dunia ya sasa ni ya watu multi-skilled na unahitaji adaptability kuna makocha kibao wanajitolea bila kulipwa hata senti na wengine wengi zaidi ni jobless...; Waambie madogo just follow your dreams na passion ila sio uende kusomea kuwa kocha au pundit; unaweza ukaanza kufanya ukocha na ukitaka kupata FIFA badge unachukua vijikozi vichache tena vingine online
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…