Hizi ni baadhi ya fursa za ajira upande wa Soka ukiachana na uwezo wa kucheza mpira

Hizi ni baadhi ya fursa za ajira upande wa Soka ukiachana na uwezo wa kucheza mpira

Hapa tuna JK youth park pekee labda na Don Bosco ambapo hadi upate nafasi ya kucheza ukiwa unatokea chanika basi ni muujiza utajiuliza fungu la michezo halmashauri huwa linafanya Nini!?
Hakuna sport center yoyote ya kisasa tena kama hizo basketball court netball court volleyball handball ni muhimu sana kwa mapumziko ya jioni
Asa Kila KIWANJA zimejengwa frame palipobaki maji yanajaa ndio Faiza anauliza pale chuo Cha Mipango watu walienda kusomea ujinga!?
Sasa lubumbashi wana sports center hiyo ina michezo yote hadi kuogelea na walimu wapo....halmashauri zina kula tu hela wkt wange promote michezo ingetoa sana ajira kwa vijana na fursa ndogo na kubwa
 
Siyo kwamba hawajui faida zake, wanazijua sana jinsi sanaa na michezo vinaweza kuwainua wangapi. Shida ni wanaogopa maendeleo ya haraka yatakayoibua vijana wasioambilika, wasioamini wanahitaji kulipa fadhila kwa yeyote ambao watakataa kuwa machawa.

Ndiyo maana kuna sekta kuanzia elimu hadi huku kwenye michezo tunaenda kwa kujikongoja, hii inawasaidia watawala kuchukua watu wawili watatu wawaweke pale juu au wale wawili watatu watakaopenya kwa nguvu zao wenyewe, waweze kusema kinafki "mnaona hawa wamefanikiwa, nyie wengine mnakwama wapi?"
Yes huu ni mkakati kabisa wa wakubwa wanajua ktk michezo kuna familia nyingi sana za kimaskini wakiwezesha michezo family za kimaskini zitapata fursa

Ni km vile hawawezi lazimisha copyright ktk Muziki ili vijana sanaa iwalipe kwa asilimia 100 ,wanajua huo ujinga na umasikini wa vijana na family zao ndio mtaji wao
 
Sasa lubumbashi wana sports center hiyo ina michezo yote hadi kuogelea na walimu wapo....halmashauri zina kula tu hela wkt wange promote michezo ingetoa sana ajira kwa vijana na fursa ndogo na kubwa
Brother mdudu anaitwa halmashauri kwenye hii nchi ameiua kwa muda mrefu sana
Asante kwa wakurugenzi makada kitu pekee wanajua ni kutangaza matokeo ya uchaguzi
 
Brother mdudu anaitwa halmashauri kwenye hii nchi ameiua kwa muda mrefu sana
Asante kwa wakurugenzi makada kitu pekee wanajua ni kutangaza matokeo ya uchaguzi
Hahahahaha na hayo matokeo yenyewe sio ya kweli kivile ..

Halmashauri za Tanzania , kujenga vituo vya bus shida, kujenga masoko shida

Leo kila Halmashauri inagawa viwanja lkn husikiii wametenga sports center kwa ajiri ya vijana ila utasikia wakisifia Tanzania tuna vipaji..
 
Kimsingi hakuna hata mpango wanao mkurugenzi akitangaza matokeo akampa tale tale ushindi yani anaandika kwenye diary yake kama Moja ya mafanikio hakuna stand hakuna soko hakuna sports center basi tufanye ni ngumu sport center agiza basi Kila shule ya msingi na Sekondari iwe na uwanja wa basketball na netball kwenye eneo lako ambayo ni 20 ml in total tena kwa international standard how!?
 
Dah kweli kabisa ..tena court ya basketball inaeza ingiliana na court ya netball na hata volleyball..yaani court moja inabeba michezo mitatu
 
Ina maana maafisa michezo huko halmashauri huwa wana kazi gani haswa ?
Dah hapa nakosa Cha kuandika labda kuhudhuria washa na tamasha mbalimbali na jogging clubs
Anyway ni kama tulivyosema mwanzo neno "michezo"kwa nchi yetu ni sawa na kusema "huna Cha kufanya umeamua kupoteza muda"
Kwa hiyo serikali inaona hiyo hela ni kheri iliwe kuliko kupelekwa kwenye michezo
 
Habari za uzima,

Tukiwa kama wadau wa michezo, naomba tuoneshe fursa mbalimbali ambazo zipo zinazoweza kuwasaidia Vijana kupata ajira au kutengeneza pesa kupitia michezo. Moja ya changamoto wanazozipitia Vijana wengi ni uchaguzi wa nini wafanye katika khari ya kujikwamua ki maisha, pamoja na baadhi Yao kupitia kwenda shuleni, mfano kusoma mpaka elimu ya kidato Cha nne au zaidi, ukimuuliza aseme anapanga kuwa nani baada ya masomo yake, utasikia akitaja fursa zinazoendana na taaluma tu, mfano, kuwa mwalimu, daktari, nesi, injinia, rubani nk nk. Wachache sana wanaoiona michezo kama fursa nje ya taaluma (academic).

Kwenye michezo, Kuna fursa nyingi zaidi na kwasasa ndipo kulipo na pesa zaidi. Kwa kulitambua hili, hebu tuoneshe baadhi ya fursa zilizopo kwenye michezo ili kusaidia Vijana mbalimbali wanaojaribu kujikwamua ki-maisha, fursa hizi watazikuta Kila watakapo google kutafuta habari za fursa za michezo.

1. Referee; hii ni fursa ambayo unaipata hata bila ya kujua kucheza mpira, Vijana waelekezwe ni wapi wanaweza kupata mafunzo ya u-referee.

2. Coaching; unaweza ukajifunza kuwa kocha wa mazoezi tu, goalkeeping, au team yote kwa ujumla, Kuna academy nyingi zinahitaji makocha professional, na hii haihitaji mpaka ujue kucheza mpira kwa asilimia kubwa.

3. Uchambuzi na utangazaji wa michezo, hii pia haihitaji kujua kucheza mpira tu, unaweza kuwa mchambuzi wa michezo mbalimbali ikiwemo ngumi, mpira, riadha nk.

4. Kutengeneza na kuuza bidhaa za michezo

Hizi ni baadhi tu, tuendelee kuonesha fursa nyingi kupitia michezo

You're welcome.
Safi sana Mkuu! Moja kati ya andiko bora sana! Fupi ila limejaa madini sana!
Cha kuongezea hapo tu! Tunaweza kutengeneza kazi au fursa ambayo itajumuisha michezo na utalii! Tunatumia sehemu ya utalii na mpira ili kuongeza uelewa zaidi!
Safi sana Mkuu
 
Ndio maana nimekwambia club ni sawa na kampuni au viwanda si unaona Kila siku vinakufa ila wafanyakazi huenda mahali pengine na kupata kazi na maisha yakaendelea!?
Vijana wakipata hizo taaluma wanaweza kwenda kuajiriwa au kujiajiri maeneo mengi ya soccer
Germany Uk Spain France Italy na US michezo ndio sekta imeajiri watu wengi zaidi kuliko sekta yoyote Ile na ndio high paid ukifanikiwa kutoboa huko basi unaishi tajiri ukiwa bado mtoto eg Mbape Yamal Hao kina Saka n.k
Na mimi ndio maana nanikwambia ingawa industry ya football ina faida kubwa sana hata zaidi ya monetary na kuna shughuli nyingi za pembeni zinafaidika kutokana na hizo pesa ila wafanyakazi / wanaofanyia kazi hivyo vilabu, wachezaji wengi ambao sio top names wanachopata ni kidogo sana na cha kinyonyaji katika kila Mbappe mmoja kuna kina John Doe wa kutosha ambao maisha yao yanategemea hisani ya wadau.....

Sisemi kwamba kama nchi tusi-invest kwenye vitu kama hivi la hasha tufanye hivyo sababu faida yake ni kubwa zaidi ya pesa za moja kwa moja..., ndio maana hata timu kama Real Madrid na mapesa mengi inayoingia ni Halmashauri yao ndio mara kwa mara inawasaidia wasiende under.....; Unaweza ukawa na kiwanja tu ambacho kukimanage kwa mwezi ni milioni kadhaa sasa kama unaingia watu robo kwenye uwanja unaweza kuona hizo ni money down the drain... Angalia hio article na hapo siongelei timu za mitaani bali creme de la creme la football clubs

Natafuta vijana wenzangu 100 kazi yetu itakua timu yoyote inatukodisha na kutuvalisha jezi kisha tunaingia uwanjani kazi yetu ni kushabikia full vibe mwanzo mpaka mwisho.
Training yetu itakua ya kujifunza namna ya kushangilia na kutoa sauti kubwa
wewe unakuwa kapteni wa mashabiki unapanda juu ya viti unaongoza ushangiliaji kama yule jamaa wa Al hilal mnaweza kupiga hela sana mtakuwa mnakodiwa na timu zenye mashabiki wachache,siku ya mechi mnaambiana mje mmevaa jezi za rangi ya timu husika ili kupunguza gharama za uendeshaji wa kampuni.
 
Mbona inakua serious sasa😅
 
Video analysts inakuaje
Ni kama wachambuzi wao hufatilia mechi na kuangalia ubora wa team pinzani au udhaifu kabla wakati na baada ya mechi,hii husaidia team kuja na mpango mzuri wa mechi hiyo au mechi ijayo
Nadhani huwa unaona hasa mechi kubwa za Ulaya watu Wa ka ipad pembeni wakati mechi inaendelea ndio hao
 
Back
Top Bottom