Habari jamvi?, kwa wale wazurulaji nchini
Ukizunguka nchini utakutana na sehemu maarufu , kimandhari na kimuonekano.
Leo naongelea sehemu za barabara nchini ambazo Zina Kona Kali na sehemu ya milima, nataja chache nyingine ongeza
1. Kona za Iyovu - ukitoka tu mikumi kuelekea iringa utaziona Kona hizi, ni Tamu Sana
2. Kona za kitonga - hizi zinapatikana kutoka Moro kwenda iringa.
3. Kona za Kolo- hizi zinapatikana kutoka kondoa kuelekea babati
4.kona za Nyang'olo - hizi zinapatikana unapokaribia kufika iringa kutokea dodoma
5. Kona za Lukumbulu songea huko
6. Kona za msambiazi, korogwe kuelekea mombo
7. Kona za Mombo kuelekea Soni - Lushoto
8.Kona za Mbeya kwenda Chunya
9. Kona za Ugara - Babati kwenda Mbulu - hapa kitonga chamtoto Cha ngedele
Ni Kona hatari lakini Tamu Sana, na mabasi huwa wanalala na Kona hizi kwa speed ya 120 yaani shaa.
Ongeza Kona Kali nyingine