Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Nyagoro( Iringa- dodoma ) , ni shida, kile kipande kina kilometers kaa 28 toka unapozianza zile kona hadi unapozimaliza , na inasemekana zile kona zipo kaa 300. Nanikona za bampa to bampa kweli .

Basi kuna jamaa anaitwa ustadhi ( dereva fuso tandam ) huyu mjomba huwa inazila zile kona speed ikisoma 60 km / h kwenye dash board mi hupaki tu nimeshikilia roho yangu .
Hiyo sehemu ni hatari mno, ukimaliza Kona unasali na kushukuru Mungu
 
Hata mimi niliuliza kuwa hapa ajari zitakuwa nyingi wakasema ni nadra sana kutokea maana wakimbiaji wa ile barabara ni wenye private wazoefu na mabasi kama kina side, burdan, maning nice n.k ule mlima ukiwa mgeni unaweza kuogopa hata ushuke upande kwa mguu, na bondeni kule ni mbali sana na barabara ni nyembamba gari kubwa zinasubiriana zipishane, halafu kuna vile vikaravati na kona papo kwa papo dah
Unakutana na Chakito Longway au Shambalai Apache zinashuka speed ziwahi abiria Mombo. Hiyo Chakito ni Fuso body za kuchonga anavyoshuka unajiuliza mwamba anajihamini nini?
 
Zile Kona za mtera ni kufuru[emoji23]
Halafu haziishi haraka tofauti na kitonga dk chache tu pameisha.
Zile nusu saa inaisha bado hazijaisha na hapo gari ipo speed Sana.

Zile Kona ilifika mahala nikazizoea,,Kama hujakaa siti ya dirishani unaweza kudondoka aisee[emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Nazo ziko kama kitonga,pembeni korongo.
Aisee sijapita hii njia na wala siwish kuipita😀 mambo ya kuminya breki kama mimi ndiye dereva sitaki😀
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Hizi breki za miguu kumbe tupo wengi [emoji1787][emoji1787]
Hatari sana na kujishikilia kwenye kiti kwa nguvu huku ukiminya breki😀😀😀 maisha ni matamu haya jamani ijapokua tunalalamika hamna pesa maisha magumu ila when it comes to uhai mmh full mabreki kama dereva😀🙌
 
Morogoro kuna Njia ya kutoka Mlali kwenda Mgeta Kibaoni kuna mlima hatari kuna Kona kali na miinuko mikali pia wameweka kalavati za kupitisha maji kwa juu na njia ni nyembamba. Kama dereva mgeni akipita na gari manual atapata tabu Sana.Ukienda mbele zaidi utakutana na vilima huko Nyandira.
 
Kuna milima na kona za hatari huku goba...
Jamaa yangu alikuwa hajawahi kupita Goba road. Siku katoka na Washkaji wakapita njia hii pale kwenye kilima Cha Mount Kibo Primary mpaka Kayuni gari yake Nissan March ilikosa nguvu akapanda kibishi.

Sasa akawa anasimulia amekutana na kilima Kikali Sana Dar, watu wakawa wanamcheka Sana wanamwambia kapanda Kitonga ya Dar na yeye ni Mwanadarisalama hajawahi kwenda Mkoa maisha yake yote.
 
Mi nashangaa watu wanafananisha eti na mburu kusiko hata na maporomoko,

Burdani anapitaga na mpaka 90kmph usiku, Madereva Wageni wengine wakifika Mombo wanaomba Mwenyeji awasaidie kupandisha, No chance for mistakes juu kuna jabali, chini kuna falls kati hapatoshi.

Cha kushangaza Sijawahi sikia ajali njia ilee.
Sababu ile ni njia ya pembezoni hivyo magari ni machache tofauti na Kitonga ambayo nikm geti la kuingilia nyanda za juu kusini na nchi jirani

Unaweza toka Mombo hadi Lishoto usipishana na lori
 
Back
Top Bottom