Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona ni pa kawaida sana pale...Ni Tukuyu ile ukiwa waitafuta Kiwira kama unatoka MbeyaKuna kona moja matata kutoka Mbeya kuelekea Malawi imepewa jina Uwanja wa ndege ni balaa,R.I.P nyingi zilipatikana pale hasa kwa wageni enzi hizo hadi kuna kibao cha onyokali,punguza mwendo,tembea taratibu[emoji591][emoji591][emoji591][emoji591]
1. Kona za Iyovu - ukitoka tu mikumi kuelekea iringa utaziona Kona hizi, ni Tamu Sana
Hiyo barabara(uyole-Tukuyu- kyela). Nimeipita, ila huwa sioni Kona za kuogopesha au kwasabb huwa niko na uchovu.Kweli mkuu ile barabara pia haiko vizuri , uwanjwa wa ndege gari zilikua zinapaa kuelekea porini aisee[emoji848] sasa mkiwa mmetoka Dar kufika Mbeya mjini kuanza kuitafuta Tukuyu madereva wanahisi wameshafika sijui wanatoka speed balaa basi huku abiria mapigo ya moyo yanaenda mbio. Sitosahau dereva na konda wanatuambia hatujawahi kufika mbeya kyela ndiyo mara ya kwanza afu wanatoka speed balaa nikasema hivi wanaijua uwanja wa ndege hawa[emoji19][emoji19]
madereva wa mabasi hata hawaogopi hii sehemu. Kuna siku nilikuwa ninasafiri kutoka Dodoma kwenda Iringa nilijuta hii sehemu ni hatari🙌🙌Mkuu funga safari utoke iringa kwenda dodoma au dodoma kwenda iringa via Mtera utakuja kuelezea hiyo kitonga ni cha mtoto
Mi nashangaa watu wanafananisha eti na mburu kusiko hata na maporomoko,
hii ni hatari sana yaani bora uzungukie Rungwe[emoji23][emoji23][emoji23] ile ya chimala ni hatari kwa afya yako unaweza kufa kwa presha
Hizi kona nilipita na shambalai bus 2009 sio mchezo kabisa na madereva vichaa wanalaza gari kana kwamba hajali kuwa lolote linaweza kutokea, Na mambo yaende Sawa angalau usichungulie upande wa bonde .Mombo-Soni-Lushoto,
Mara ya kwanza waweza useme huku sirudi tena.View attachment 1764642
Umenikumbusha mbali...tuliopitia Kwiro sec tunazitambua kona za Ndololo.Kona za mlima Ndololo, Mlima nyani njia ya Ifakara-Mahenge. Kona za kuitafuta Mkamba/Sanje na Soni ukitoka Mikumi kwenda Ifakara.
Naunga mkono hoja.Kona namba moja ilipaswa kuwa nyang'oro , kutoka mtera kwenda iringa.
Na namba mbili ilipaswa kuwa lipumburu, kutoka njombe kwenda songea
Na namba 3 ilipaswa kuwa kawetere
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Mi kona za kitonga aah sijawahi kuzioea kabisa, hasa nikiwa natoka Iringa to Moro (kushuka) huwa nahisi moyo unahama mahali pake huku maini kama yanatoka hivi, aah na madereva sijui ndiyo wamezoea hiyo speed yake sasa[emoji848] huwa nabaki nasali tu na kuminya breki za miguu[emoji3]
Kona za kutoka Njombe - Madaba - SongeaHabari jamvi?, kwa wale wazurulaji nchini
Ukizunguka nchini utakutana na sehemu maarufu , kimandhari na kimuonekano.
Leo naongelea sehemu za barabara nchini ambazo Zina Kona Kali na sehemu ya milima, nataja chache nyingine ongeza
1. Kona za Iyovu - ukitoka tu mikumi kuelekea iringa utaziona Kona hizi, ni Tamu Sana
2. Kona za kitonga - hizi zinapatikana kutoka Moro kwenda iringa.
3. Kona za Kolo- hizi zinapatikana kutoka kondoa kuelekea babati
4.kona za Nyang'olo - hizi zinapatikana unapokaribia kufika iringa kutokea dodoma
5. Kona za Lukumbulu songea huko
6. Kona za msambiazi, korogwe kuelekea mombo
7. Kona za Mombo kuelekea Soni - Lushoto
8.Kona za Mbeya kwenda Chunya
9. Kona za Ugara - Babati kwenda Mbulu - hapa kitonga chamtoto Cha ngedele
Ni Kona hatari lakini Tamu Sana, na mabasi huwa wanalala na Kona hizi kwa speed ya 120 yaani shaa.
Ongeza Kona Kali nyingine
Zile Kona za mtera ni kufuru[emoji23]Duh aki sitaki kupita njia hiyo nimeskia ni kona mno, ile kitonga tu mimi naskia kulia huko sijui itakuaje, kuna siku tunatoka Mbeya kufika kitonga pale naona watu wanalia wameumia kuuliza ni ajali na gari imedumbukia kule chini ingawa si kule bondeni sanaa na hao watu wametolewa huko na kuletwa huku juu kwa ajili ya kuwaishwa hospital duh[emoji25][emoji25]nilitetemeka maana dereva wetu alikua anaenda speed na hizo kona hajali.
Miaka hiyoooo kabla ya barabara kuchongwa ilikuwa balaaa Tumelala sana kwenye hii njia. Maporomoko ya mawe mvua zikinyesha balaa. Ukifika Soni unapumua kidogo kuanzia pale kuitafuta Mombo mmh ni Mungu tu. Tulikuwa tunawacheka sana wasambaa eti miguu imekomaa sababu ya milima. Kwenda Gare usipime lakini all in all kuna ardhi yenye rutuba sana.Kona za Lushoto Mombo