Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Hahaha inabidi atembee akaone maajabu huko nyanda za juu kusini magharibi na nyanda za juu kaskazini mashariki, kwanza atambue maana ya neno nyanda za juu Kisha mumueleweshe kwanini wapaite nyanda za juu na so nyanda za chini kama dasilamu
 
Kona na milima ya Usambara (Mombo - Lushoto). Mara ya kwanza kabisa nilipita usiku kuelekea Lushoto, sikuona. Kimbembe ilikuwa siku narudi kuelekea Mombo, ilikuwa mchana tena nilikaa siti ya mbele kabisa kwenye Land Rover. Pale Soni tokea Lushoto huoni kabisa kona mpaka ukaribie. Basi nilijua sasa tunakwenda kutumbukia. Barabara nzima nilikuwa nafunga breki as if naendesha mimi. Kufika Mombo mguu wa kulia ilikuwa unauma hatari.
 
Ile barabara Mombo to Soni inahitaji umakini wa hali ya juu kabisa as if unafanya operation ya moyo. A slightly mistake, you are gone.
 
Zile kona hazionekani vizuri na siyo kali sana kama unatoka Lushoto ila ukiwa unaenda Lushoto mtihani
 
Wakati naenda huko nilikaa dirishani kuna fala moja likasema hapo gari ikidumbukia hakuna wakupona sikulijibu chochote [emoji23]
 
Ukipanda New Force ya yule mchina mshenzi mvuta fegi lazma ushike roho mkononi🤓🤓🤓
 
Mlima Nyoka🐍
 
Zile ni shida kona75 za kutisha ,mpaka Gari la juu utosi wa kichwa unaliona
Kabla sijapita njia ile nilikuwa nadhani kona za nyang'olo ndio nyingi na zinashtua,aisee nchi hii Kuna kona zinatisha kupindukia,njia chimala-matamba ukipita hutamani kupita tena na kama una gari halieleweki utaishia makorongoni.
 
Kabla sijapita njia ile nilikuwa nadhani kona za nyang'olo ndio nyingi na zinashtua,aisee nchi hii Kuna kona zinatisha kupindukia,njia chimala-matamba ukipita hutamani kupita tena na kama una gari halieleweki utaishia makorongoni.
Katikati ya mlima kuna sehemu panaitwa mwadangala ,hapo kuna kona kama sita hivi zipo karibu karibu na bonge la bonde kushoto na kulia kwako ,mlima una nyuzi 75. Gari likiachia huko chini watu hawakufati chini wanafanya ibada juu kama kwenye meli ya titanic
 
Aisee sijapita hii njia na wala siwish kuipita[emoji3] mambo ya kuminya breki kama mimi ndiye dereva sitaki[emoji3]
Mimi ilikuwa najiwahia siti ya dirishani nachapa zangu usingizi,hata sijali yaani [emoji23]
Yaani pale hata kula huwezi maana chakula chako chote kitakumwagikia[emoji1787]

Ukikaa siti ya pembeni yaani wewe utapambana kushikilia kiti hadi ukome maana gari inalala mno,kushoto kulia imagine saa nzima [emoji1787]

Mara ya kwanza napita kule Mtera nilitamani nilie[emoji23]ila ndio kulikuwa hakuna namna, nimesoma Dom hadi nimemaliza napita ile barabara,safari za kutosha.

Ila hizo Kona za Nyang'olo Zina balaa[emoji119]
It's funny sometimes,mimi nilikuwa naburudika sana ila naomba tu Mungu gari isitumbukie korongoni[emoji23].

Ukisema ushike breki za miguu basi utashika hadi miguu iume maana Kona haziishi zile[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hatari sana na kujishikilia kwenye kiti kwa nguvu huku ukiminya breki[emoji3][emoji3][emoji3] maisha ni matamu haya jamani ijapokua tunalalamika hamna pesa maisha magumu ila when it comes to uhai mmh full mabreki kama dereva[emoji3][emoji119]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119]
Haka kamtindo nilikuwa nako zamani aisee..
Siku nimepata ajali nilikaachaga,maana ajali ikija hata ujishike vipi[emoji23][emoji23][emoji23],siku hizi huwa nasafiri tu bila kujali,lolote na liwe..kwanza huwa naamini nitafika salama na Mungu ni mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…