Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Vunta ni hatari mno, ni moja Kati ya dangerous roads, na hiyo ya Ugara kwenda Mbulu basi haziwezi kupita Kona ni Kali Sana.

Hizi Kona mbili kifo unakiona kileeee
 
kwa kona nilizowahi pita ni nyankoro kona ya dodoma iringa hii kona ukiwa umetoka mtera unaianza na haishi uzuri wa hii kona ina lami afu ni pana barabara pia kuna kingo,

Kona nyingine ni Mwanga kwenda Ugweno kwa mimi izi kona ni funga kazi barabara nyembamba afu kona kama zote,

Kona za kolo kondoa kwenda dodoma aiseee nazo ni shida.

Kona ya kutoka muheza kwenda msitu wa amani nayo ni kali.
 
Magara kwenda Mbulu usha wahi pita ile njia? Hahaaa pira siku moja na hutaomba kurudi na hio njia
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 
Narudia kusisitiza

Mteremko wa kushuka Bondeni Rukwa kutoka Sumbawanga kwenda MUZE ni #1 kwa hatari.

Nimeambatanisha picha ya kutokea angani.

Mteremko gradient yake ni almost 45 degrees, Bus za kawwida ama Fuso za kawaida haziwezi kupita isipokuwa zile fupi fupi. Kuna kona kali almost nyuzi miatatu hamsini hivi.

Bàadhi ya madereva wapo radhi wwzunguke 180km plus kufika Muze kutokea Sumbawanga kuliko kukatisha hapo ambapo ni chini ya km 60.

Kwa madereva walio safiri sehemu mbalimbali Tz na wamepita njia hiyo watakubaliana nami, pia kwa abiria ambao wanaujua mlima huo na wanazijua njia nyingine ikiwemo ile ya Tukuyu, Makete, Lushoto na Manyara watashuhudia kuwa kushuka MUZE ni namba moja.

Ingawaje kwa picha hiyo huwezi kuona vizuri lakini ukipita utajuwa kwa nini nasema ni hatari.

Kitonga, Kigoma, Lukubulu, Gangitoroli kote ni cha mtoto.
 
Hata tungepata ufundi mkubwa kiasi gani, bado tunamhitaji Mungu. Huyo wa NIT/VETA naye anaugua, anapata maruweruwe, anachoka, anasinzia na anaweza akawa amelewa. Madereva wazoefu wanasema mara nyingi wanaona vitu vya ajabu barabarani, ikiwemo kukutana na bwawa ghafla. Kumbe halipo! Mimi ni dereva nayajua mauzauza kama hayo.

Ndio maana namtumaini Mungu katika kutuepusha na ajali zinazotokana na dosari za kibinadamu, kiufundi au hata kimiujiza. Na tukumbuke kuwa si kila dereva anatoka NIT/VETA, na si kila anayetoka NIT/VETA ni mkamilifu. Watu si malaika, tuna upungufu na udhaifu mwingi!

Tunamhitaji Mungu kwa kuwa binadamu hatujakamilika na hata vifaa tunavyotengeneza navyo havikosi hitilafu, hata kama ni vipya!

Si kwamba Mungu anaendesha Yeye badala yetu, la hasha; bali hutuwezesha, hutulinda na hutuongoza kufanya maamuzi sahihi. Yaani anakuwa Dereva kupitia sisi.
Mungu wa nini? Umeenda Veta ukatoka ukaenda NIT umeaminiwa ukapewa leseni? Mungu wa nini tena?
 
Kuna siku nilipanda premier line kutoka mwanza kwenda mbeya...nakumbuka zile kona za nyang'oro jamaa alikua anapanda huku gari inapiga alarm kuwa yuko speed zaid ya 80...halafu baada ya kona kuna sehem ina mwinuko ukipita unahisi gari inapaa na kupata ajari
 
Kona hatari ni kona za kutoka Mbeya kwenda Chunya. Kona nyingine inaitwa Gangi tololi, kutoka Njombe kwenda Ludewa.
Kuna kona za mkoa na kona za wilaya 😂😂. Unaongelea zipi?
 
Uko sahihi mno .... Nimepita hiyo njia mara kadhaa... Ni hatari sana... Hata Waziri Jaffo akiwa Tamisemi aliipita hiyo njia kwenda kukagua kituo cha afya kule bondeni.... Anasimulia hadi kesho jinsi alivyopata changamoto....
 
Hizi zote nimepita isipokuwa Mwanga - Ugweno.

Muheza - Amani Game Reserve ikiwekewa mkeka itakuwa rahisi tu kupita
 
zile hata anayesema nyankoro ni kali hana lolote zile ni kona
Kona za kupandisha mlima kutokea mwanga kilimanjaro unaelelekea kijiji kinaitwa ugweno baba ile naifananisha na death road ilioko Bolivia lakini haina ajali za ovyo oanayesema

Hizi zote nimepita isipokuwa Mwanga - Ugweno.

Muheza - Amani Game Reserve ikiwekewa mkeka itakuwa rahisi tu kupita
kona ya mwanga ugweno haina wapitaji sana lakini ni kona kali kuliko zote yaani ni funga kazi mkuu afu haziishi sasa bora iyo nyankoro, nyankoro inatisha kutokana na zile landscape zake na misitu minene.
 
Ivi hamna njia mkato kupitia Tabora hadi Mbeya ukitokea Mwanza?
 
I wish siku moja nipite hiyo kona kuelekea Ugweno nione yaliyomo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…