Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Sababu ile ni njia ya pembezoni hivyo magari ni machache tofauti na Kitonga ambayo nikm geti la kuingilia nyanda za juu kusini na nchi jirani

Unaweza toka Mombo hadi Lishoto usipishana na lori
Ni kwelii, fuso ndio zimejaa, na mkikutana lazima mmoja arudi nyuma kutafuta gap ampishe mwenzake, au asimame mwenzake apite taratibu, kwa ufupi hakuna mazingira ya kupishana bila namna hizo mbili.
 
Katikati ya mlima kuna sehemu panaitwa mwadangala ,hapo kuna kona kama sita hivi zipo karibu karibu na bonge la bonde kushoto na kulia kwako ,mlima una nyuzi 75. Gari likiachia huko chini watu hawakufati chini wanafanya ibada juu kama kwenye meli ya titanic
Nasikia hilo jina ni mzee aliishia makorongoni na gari lake katika hizo kona na kona moja ikapewa jina lake kumkumbuka.
 
Watu wengi wanaoenda Mbulu hua wanapitia Karatu ambapo njia hiyo japo ni rough road ila haina shida. Barabara tunayoizungumzia hapa ni shortcut kutoka Mbulu, kupitia Magara kuja kutokezea sehemu inaitwa Mbuyu wa Mjerumani ambapo unakutana na main road ya kutoka Arusha kwenda Babati. Hii barabara niseme kwa Tanzania, Afrika mashariki na nchi za SADEC jumlisha na maziwa makuu kusini mwa jangwa la Sahara ndio inaheshimika kwa kona kali sana kupita maelezo!!! Mbaya zaidi barabara inapita juu ya mlima ambapo PANDE ZOTE ZA BARABARA NI MAPOROMOKO MAKALI!! Kama unaendesha gari, yaani hata ukiwa spidi 10 bado utajiona uko spidi kali sana, na hakuna kabisa uwezekano wa magari mawili kupishana..!!!! Hii ndio barabara pekee ambayo madereva hua wanapaki magari katikati ya barabara ili wapumzike na kufuta jasho kwenye mikono, miguu hadi kwenye meno.

View attachment 1764818

View attachment 1764819

View attachment 1764820

View attachment 1764822
Daahh
 
Zinafanana na kona za barabara za kutoka Sumbawanga au njia kuu ya Sumbawanga Tunduma kuingia bonde la Ziwa Rukwa.

Kuna barabara 3 za kuingia bondeni zote zina kona kali kama hizo
 
Zinafanana na kona za barabara za kutoka Sumbawanga au njia kuu ya Sumbawanga Tunduma kuingia bonde la Ziwa Rukwa.

Kuna barabara 3 za kuingia bondeni zote zina kona kali kama hizo
Kuelekea Mtowisa usipopita Maji Moto kuna mlima mkali sana na korongo panaitwa KABURI WAZI. Nimepita Kitonga,Nyang'olo hadi huko Chunya ila hiyo down ya Kaburi Wazi hakuna mfano sema sio maarufu kwa kuwa sio main.
 
Habari jamvi?, kwa wale wazurulaji nchini

Ukizunguka nchini utakutana na sehemu maarufu , kimandhari na kimuonekano.

Leo naongelea sehemu za barabara nchini ambazo Zina Kona Kali na sehemu ya milima, nataja chache nyingine ongeza
1. Kona za Iyovu - ukitoka tu mikumi kuelekea iringa utaziona Kona hizi, ni Tamu Sana
2. Kona za kitonga - hizi zinapatikana kutoka Moro kwenda iringa.

3. Kona za Kolo- hizi zinapatikana kutoka kondoa kuelekea babati

4.kona za Nyang'olo - hizi zinapatikana unapokaribia kufika iringa kutokea dodoma

5. Kona za Lukumbulu songea huko

6. Kona za msambiazi, korogwe kuelekea mombo
7. Kona za Mombo kuelekea Soni - Lushoto
8.Kona za Mbeya kwenda Chunya
9. Kona za Ugara - Babati kwenda Mbulu - hapa kitonga chamtoto Cha ngedele

Ni Kona hatari lakini Tamu Sana, na mabasi huwa wanalala na Kona hizi kwa speed ya 120 yaani shaa.

Ongeza Kona Kali nyingine
Kuna barabara ni hatari Ila hazujulikani saana..
1.Kuna Barbara kutoka Hedaru kwenda milimsni Kuna Kijiji kinaitwa Vunta...hiyo unaweza omba poo...Heshima kwa watumishi wa Serikal wanaofanya kazi kule !
2.Hiyo no 9 njia ya kwenda Mbulu ukitojea Babati,au Arusha kuingilia Mbuyuni...ni balaa Basi kubwa sijui Kama linapita!
 
Back
Top Bottom