Hizi ni ziara za Rais au ni kampeni za uchaguzi?

Kuna shida mahali mkuu. Labda katiba mpya italeta mabadiliko.
 
Wewe unadhani Operesheni +255 Katiba Mpya siyo Kampeni za 2024 na 2025?

Kampeni zilishaanza kitambo jimbo la Kawe kwa mfano Askofu Gwajima kaanza kitambo tu sasa Tuko kwenye Gwajima Cup
Hujanielewa wewe. Nimeuliza zile ni ziara au kampeni?. Halafu ni lini 255 walianza kutaja jina la Fulani kuwa watampigia kura kuingia ikulu?. Tofautisha mikutano ya CHADEMA ya kisiasa na ziara za kikazi za rais.
 
Alichaguliwa lini na watanzania kuwa Rais?. Halafu Kama anapendwa mbona anatumia nguvu nyingi kukubalika.
 
Upinzani unatakiwa upiganie sheria ya kuruhusu kampeni za kisiasa muda wowote.
Mambo ya kusubiria mwezi mmoja au mitatu kabla ya uchaguzi yamepitwa na wakati.
Hii itakuwa ngumu kutekelezeka. Nadhani wapambanie ile ya coalition hata miezi mitatu kabla ya uchaguzi Kama Kenya.
 
Samia bila kufanya fujo kama Magufuli hapati kura na hataweza toboa.
Kweli kabisa. Hana ushawishi kwa Sasa. Hata hotuba zake haizina ushawishi kwa wale wanaomsikiliza.
 
Umeelewa swali langu?. Tofautisha ziara ya Rais na mkutano wa kampeni au chama Cha siasa. Unapochaguliwa kuwa Rais wewe ni kiongozi wa wote. Unapofanya ziara unakuwa unafanya ziara ya wananchi wote na kwaajili ya kusikiliza kero na matatizo yao, sio kwaajili ya kusifiwa na kuahidiwa kura na Wana CCM.


CHADEMA wanafanya mikutano ya hadhara na sio kampeni. Ndio maana huwezi kuona mabango ya mgombea wa CHADEMA, Wala husikii Mbowe au Lissu akinadiwa kuwa atapewa kura nyingi 2025.
 
Wewe unakiitaje? Si umemuona tundulissu ziara ya Ngorongoro au utasema inaitwa ziara ya Ngorongoro? Saga wembe ule, endelea na pipoooooz yako.
Tatizo huelewi hata maana ya ziara ya Rais. Ziara ya Rais utalinganisha na mikutano ya hadhara ya CHADEMA?. Mikutano ya CHADEMA hakuna kunadi Fulani atakuwa Rais zaidi ya kujadili katiba, bandari etc. Ila kwenye ziara ya Rais ni kumsifu na kumwabudu Rais mpaka mwisho na kumpigia debe basi.
 
Mungu awaponye Sana majeruhi. Tatizo CCM wanalazimisha kukubalika.
 
Kwa ushauri hizi ziara ziwe za kikazi, Rais aondokane na haya makampeni. Afike kwa wananchi aulize shida zao na Kama wahusika wapo wajibu tuhuma zao.
Mkuu 'econonist', kidogo mimi ninakushangaa wewe, pamoja na kuwasilisha mada liyojitosheleza kabisa; kwamba wewe ndio kwanza unaiona hali hii ya Samia kuwa kwenye Kampeni.
Huyu Kampeni zake zilianza mara tu aliposhika kiti cha urais, na hata siku moja hajafanya tofauti na kujiuza achaguliwe kuendelea kwenye nafasi hiyo.
Alipoingia, wewe hukuona alivyokimbilia harakaharaka kujiuza kwa wasanii? Hukuona matukio aliyofanya ili awaweke wasanii wamuuze katika kazi zao?

Wewe unadhani hayo mabango yaliyotapakaa mijini ya "Nani kama mama" yapo huko kufanya kazi gani?

Wakati akijaribu kuwanunua CHADEMA, unadhani aliwapenda sana hao jamaa, huoni sasa anavyowanyanyapaa baada ya kuona kuwa mtego wake haukuwanasa?

Nikubaliane na wewe, hizi tabia za kiongozi kufanya kampeni za kisiasa, na kuacha kuhudumu kwa kufuata ratiba za mipango ya kazi ni kuharibu kazi za wananchi.

Hao washangiliaji, wabunge, mawaziri na viongozi wengine wote wateuliwa wa huyu mtu mmoja, kazi zao wote wanazielekeza katika kumpigia kampeni mtu huyo huyo, ili na wao waendelee kujaza matumbo yao, na siyo kuleta maendeleo kwa wananchi.

Lugha zinakuwa ni za huyu mtu mmoja, kaleta hiki na kile, kajenga shule, kaleta barabara, kaleta maji; mwishowe tutaanza kuambiwa hata kwenda chooni tutakuwa tunamtegemea mtu huyu huyu mmoja.

Na kwa baadhi ya watu wetu wajinga ndani ya nchi hii wanauamini upuuzi wote huu!

Hovyo Kabisa.
 
Mungu awaponye Sana majeruhi. Tatizo CCM wanalazimisha kukubalika.
Cha kusikitisha zaidi, hawa waliofariki na waliojeruhiwa,huenda hata sababu iliyokuwa ikiwapeleka huko hawawezi kuieleza kwa ufasaha. Huenda wameahidiwa kutakuwepo na mlo (wali) kwenye hadhara hiyo, au wameahidiwa vijisenti kadhaa ambavyo wangepewa baada ya kuhudhuria hapo!

Inasikitisha sana.
 
Akili yako inafanya kazi kipekee sana.
Laiti kama pangekuwepo na watu kama wanne tu wa aina yako humu JF, pengine pangetokea baadhi ya watu wakaanza kuamini mkisemacho hata kama kinaonekana wazi kuwa kama kituko.

Sina hakika kama kuna kitu chochote kati ya hayo unayorudiarudia humu, hata wewe mwenyewe unakiamini. Bila shaka kila siku unapopata wasaa wa kupumzika na kuwaza, wewe mwenyewe hujishangaa ni jinsi gani unavyoweza kuandika mambo usiyoyaamini hata wewe mwenyewe, ukikusudia wengine wayaamini.

Ndiyo maana nasema, akili yako hufanya kazi kwa njia za kipekee sana.
 
Uzuri watu hawaendi kwa hiari

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kwahiyo unataka Rais asizingumze hadharini na kusifiwa na watu waliomchagua? wanaona anachofanya Rais wao..

kama hupendezwi nae na actually yawezekana hupendezwi nae na unaghadhabu nae sana, sasa si ukae nyumbani utulie gubu liendelee kukutafuna ndani kwa ndani.

Rais ni Rais tu awe kanisani, msikitini, kwenye mikutano ya hadhara au kampeni ya chama chake,upinzani kwenye msiba, sherehe yeyote ile yule ni Rais tu.

Na atasifiwa sana tu.
Kwan Mbowe au Lisu hawasifiwi? Kuna watu wasifia hadi watukana juu ya hawa viongozi.

sasa eti ukae mahali halafu uanze kujiuliza eti huyu anafanya ziara au kampeni, sijui anasifiwa sana,
Hiyo inabaki kua nadharia na tafisiri yako binafsi isiyoathiri sheria wala taratibu za nchi.
Na sio mbaya, ni vizuri kua hivyo, mwisho wa siku unaweza kuibua wazo linaloweza kusaidia kuondoa hali unayokumbana nayo na pengine inawakumba na wengine wengi tu.
 
sio kweli ila uko sahihi kulingana na upeo na matazamo wako na hiyo ni haki yako.

anachofanya Rais samia ni kuwaeleza wananchi waliamchagua mambo waliyoahidi ambayo tayari yamefanyika yanachofanyika hivi sasa, na yanayokusudiwa kufafanyika tuendako.

haiwezekani alipoenda kuomba ridhaa na kura alivaa nguo za ccm na mabango ya ccm eti sasa anapoenda kuwapa mrejesho avae shuka, ndicho unachotaka right?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…