Hizi ni ziara za Rais au ni kampeni za uchaguzi?

Sema ukweli kuwa amekuwa Rais kwa sababu ya ubovu wa katiba yetu. Hakuna aliyemchagua, Bali amekuwa Rais by default. Huo ndio ukweli.
kiri kwanza amekua rais kulingana na katiba na sheria za nchi, mbona una kosa ungwana😀

kama hizo cheria au katiba ni mbovu ama vinginevyo sasa hilo ni suala jingine na ofcoz ni mjadala mwingine.
 
Mkuu

CCM yetu hii ni dudu!

Dr samiah hajafikia HATA robo ya uungwaji mkono alioupata jpm wakati wa MIAKA yake sita ya uongozi wake!

Walimfananisha HADI na kristo,Musa lakini leo hayupo!!


Kati ya kosa kubwa alilofanya mama ni kuingia mkenge wa machawa HAO!yaani machawa wanakusifu ili uharibu kazi ukose uhalali KWA wenye mamlaka ya nchi yetu!!

Kama kaanza kampeni mapema kabla ya 2025 anajuaje kuwa atafika huyo 2025 akiwa bado ni amiri jeshi Mkuu!!?

Kwanini asiuheshimu wakati na kunyenyekea!!?

Mi nadhani hata kama inakula vizuri KIASI GANI ,hata kama KITI ni kitamu KIASI huwezi sahau nguvu ya nyakati I asi hicho,labda uwe unalishwa madawa ya kulevya ambayo yatakupa over confidence ili uharibu!!

"NI DHAHIRI KUWA MAMA ANA HOFU KUU NDIO MAANA ANAPIGA KAMPENI KABLA YA WAKATI,NI WENYE MASHAKA TU NDIO HUONYESHA MASHAKA YAO KWA KUFANYA VITENDO KABLA YA WAKATI"

WALIO KARIBU MWAMBIENI KUWA AACHE HOFU YA KUKOSA AU KUPATA URAIS,URAIS NI MPANGO WA MUNGU SIO WA BINADAMU HIVYO AKIUPATA NI SAWA NA AKIUKOSA NI SAWA YEYE ATIMIZE MALENGO ALIOWEKEWA NA CHAMA NA WENYE DOLA TU!!!

JAPO NAONA KACHELEWA SANA YAANI TOO LATE KABISA KWA KUTIMIZA MALENGO YALIYOWEKWA!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
 
Sera ya Chama ni kuhakikisha Chama linakuwa madarakani hivyo kikishinda uchaguzi mmoja miaka minne inayofuata focus ni kwenye uchaguzi unaofuata
 
Mshaanza kugwayagwaya mapema. Ulitaka Rais asikaguwe kazi anazozitolea mabilioni?
Dah! Mbona unanipa mashtaka sio ya kwangu. Mimi natoa ushauri kwamba ziara za rais zitofautishwe na mikutano ya CCM na kampeni zake. Mfano mzuri angalia ziara za Waziri mkuu, hakunaga uchawa Wala uccm ni watu kuwajibishwa na kuchukuliwa hatua.
 
Umeongea ukweli kabisa mkuu.
 
Sera ya Chama ni kuhakikisha Chama linakuwa madarakani hivyo kikishinda uchaguzi mmoja miaka minne inayofuata focus ni kwenye uchaguzi unaofuata
Ni kweli sikatai, lakini mikutano ya hadhara ya CCM itofautishwe na ziara za serikali. Mimi namkumbuka Mkurugenzi wa Tanroads Engineer Mfugale, yeye kabla ya kuongea kwenye ziara ya Rais alikuwa anaanza kwa kusema yeye sio mwanasiasa. Kwa hivyo alikuwa haweki uchawa wowote, Bali alikuwa anasoma ripoti yake anaenda kukaa.
 
kiri kwanza amekua rais kulingana na katiba na sheria za nchi, mbona una kosa ungwana😀

kama hizo cheria au katiba ni mbovu ama vinginevyo sasa hilo ni suala jingine na ofcoz ni mjadala mwingine.
Sawa nakiri amekuwa Rais kwa mujibu wa katiba na sio kwa ridhaa ya wananchi. Hapo vipi.
 
Nchi yetu bwana inachangamoto kweli. Kiukweli huwa hakuna ziara Bali huwa ni kampeni tu. Hapa ndipo utawaona wanafiki na wachumia Tumbo wenye kutoa sifa hata ambazo Rais hana
 
Dah! Mbona unanipa mashtaka sio ya kwangu. Mimi natoa ushauri kwamba ziara za rais zitofautishwe na mikutano ya CCM na kampeni zake. Mfano mzuri angalia ziara za Waziri mkuu, hakunaga uchawa Wala uccm ni watu kuwajibishwa na kuchukuliwa hatua.
Labda huelewi kuwa CCM ndiyo chama tawala na Rais anatokea CCM.

Singapore ili kutofautisha kazi za vyama na serikali waliamuwa kurekebisha katiba yao na kuweka kifungu kuwa mgombea urais hawezi kutokea chama cha siasa chochote. Yaani awe ni mgombea huru.

Hapo hata vyama haviruhusiwi kufanya kampeni. Vyama viienda kwenye ziara za Raisa vinakuwa vimealikwa tu.

Tanzania tufanye hivyo.
 
Upinzani unatakiwa upiganie sheria ya kuruhusu kampeni za kisiasa muda wowote.
Mambo ya kusubiria mwezi mmoja au mitatu kabla ya uchaguzi yamepitwa na wakati.
Sio kupigania Kodi zetu na rasilimali muda ya wananchi isitumiwe vibaya badala ya kufanya vitu kutumia muda kutoa ahadi na ngonjera za nini kimefanyika na kitafanyika ? Yaani huu upuuzi uendelee ili na wao wakichukua nchi iwe muendelezo wa huu upuuzi ?
 
Waache waendelee kuwadhalilisha Wazee katika Nchi ili laana iwaangukie kweli kweli !!
 
Kabisa kabisa kabisa hiyo ndio dawa ya Nchi hii ili ipate maendeleo ya kweli !
Kutakuwa hakuna kubebana bebana kwa kisingizio cha huyu ni mwenzetu !
 
Hata CHADEMA wanazunguka nchi nzima wakipiga kampeni watu kuikataa CCM na Serikali ya Rais Samia. Kuna shida gani naye akitumia jukwaa lake kuinadi Serikali yake? Si tuliomba haki ya kufanya siasa kila siku na kila saa? Ndio siasa hizo sasa!!
 
Wewe unadhani Operesheni +255 Katiba Mpya siyo Kampeni za 2024 na 2025?

Kampeni zilishaanza kitambo jimbo la Kawe kwa mfano Askofu Gwajima kaanza kitambo tu sasa Tuko kwenye Gwajima Cup
Sidhani kama watu wanapinga yeye kufanya kampeni.

Watu wanahoji yeye kufanya kampeni wakati ilisemekana anakwenda mikoa ya kusini kwa ziara ya kiserikali.

Angekwenda kwa ziara ya kuimarisha chama chake wala hakuna ambaye angehoji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…