Hizi protokali za kila mtu kutaja wageni eti ni protokali nu ujinga na inachosha sana.

Hizi protokali za kila mtu kutaja wageni eti ni protokali nu ujinga na inachosha sana.

hii kitu hata mimi sielewi maana yake, nilifikiria kuwauliza wadau humu ambao wamewahi kuishi nchi za nje kuwa je, huko kuna utaratibu kama huu?!!!
Huu utaratibu wenzetu walishauacha siku nyingi,ni ushamba tu. Huwa tunaona wenzetu wanapokuja hapa kwenye hutuba zao sanasana Wana mtaja Raisi ..My Raisi Mabibi na Mabwana, itfaki imezingatiwa,anaendelea na hotuba.
 
Ni ujinga mtu anataja wageni hadi 30. Tuangalie namna ya kuliweka ili sawa. Utasikia mh fulani, mh naibu spika, mh spika, katibu, katibu kiongozi.
 
Halafu huu utaratibu wa kukusanyana uwanjani naona kama vile umepitwa na wakati.

Hatuba ingesomwa ikulu mbele ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi na ingekua live kwa anayetaka kuangalia.

Wengine waendelee na mambo yao.
 
nani wa kupeleka hilo pendekezo kwa viongozi kuwa tunapendekeza tusiwe tunawataja kwa majina wakati ikitokea mmoja tu karukwa inakuwa nongwa hadi NEC kuwa anadharauliwa na kuchonganishwa na wapiga kura wake
 
hii kitu hata mimi sielewi maana yake, nilifikiria kuwauliza wadau humu ambao wamewahi kuishi nchi za nje kuwa je, huko kuna utaratibu kama huu?!!!
Uliasisiwa kwa staili ya mfumo wa zidumu fikra za Mwenyekiti,kwa sasa unaboa.Hata kuchora mapicha ya Mgeni rasmi wakati atakuja namtamuona ni ushamba na upotevu wa rasilimali
 
Ahaa gonga tano! Ni ujinga uliokubuhu. Nchi yetu imelaaniwa sijui. Hakuna kazi za kufanya kwa viongozi ndiyo maana. Hotuba inakuwa nusu ni kutambua ''uwepo'' wa fulani. Ujinga mtupu.
Kuna vitu tz lazima vibadilike ili kuendana na muda, muda ni mali sana katika uzalishaji kwa namna yoyote ile kutambua uwepo wa mtu fulan haina tija hata kidogo kama mgen rasmi aje kutoa speech yake watu wakafanye kazi na ikipendeza yeye ndio aseme kwamba nashukuru labda mtu fulani au taasisi fulan kwa kazi zao
 
Back
Top Bottom