Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Hehehehehee mtoe hapo mpeleke kayumba aje awe kama wewe...asiweze kufikiri zaidi
Nani Kakudanganya kayumba hawawezi kufikiri?
English medium ni kiingereza tu anaongeza sio maarifa, Kama mwanao ni kiazi English medium haiwezi kumfanya genius, Na Kama ni genius Hata akisoma kayumba atatamba tu.

Hebu tafakari, kuna mtoto A anasoma primary na secondary Kwa gharama ya mil 20+,na kuna mtoto B anasona kayumba primary, Kata secondary halafu wanakutana chuo kikuu wote wanagraduate degree ile ile.

Wakishagraduate wote wanakuwa jobless, yule aliyesoma akiwa anaenda Kwa school bus anajikalia zake Nyumbani Mara Kwa uncle, hawezi kujiongeza kwasababu amezoea kulishwa kila kitu, aliyesoma kayumba anajiongeza kwasababu ni mpambanaji tangu mwanzo.

Huo ndio uhalisia uliopo mtaani, sasa Nani mwenye akili hapo?
Na Kwa Mzazi mwenye akili kuliko kupeleka mwanao akajifunze kiingereza,kuchora na kuimba Kwa mamilioni huko English medium ni bora Kama unaona ana uwezo mzr ukampekeka kayumba ukamfungulia fixed account, hiyo pesa ya ada ukawa unamuwekea Kwa uaminifu, akifika chuo atakuwa Na mtaji mkubwa sana wa kujiajiri.
 
Mkuu umeenda chaka mnoo

Sent from my vivo 1820 using JamiiForums mobile app
 
Hovyo sana hii kitu,
Umeongea kitu cha maana sana ila kuna wajinga wachache watakuona umeongea pumba
 
Mwaka jana Kipindi Cha Covid-19 shule zilipofunga walimu wa private school walianza utaratibu wa kwenda kuchukua maswali ya mitihani unalipia watoto watafanya nyumbani.

Kuna mzee alikuwa mtata Sana, nimeenda kuchukua mitihani ya binamu yangu, mzee anataka asahishiwe ndio atoke ilikuwa kabakiza English maswali aliyomsaidia mwanae yote kakosa walimu wakasema huyu mtoto michezo mingi. Baba mtu ikabidi aseme hizo homework nafanya nae mimi siendi kazini muda mwingi nipo na familia, ikabidi walimu wampooze kuwa wamejaza najibu sio sahihi.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Baba na mtoto michezo mingi
 
Ahsante sana mkuu.
 
Kama nakumbuka vema
1-Sedentary farming
2-Normadic farming
 
Ni vizuri kumfungulia fixed account na kumpeleka English medium au International school ya uhakika kuliko kayumba kama uwezo unaruhusu.Kwa sababu kuna asilimia 99% mtaji ukapuputika akarudi nyumbani kula pensheni yako wakati kuna asilimia 55% ya yeye kupata scholarship na koneksheni za nje ya mipaka,koneksheni za shule na vyuo vyetu local ukifanikiwa umeishia kufanya TRA,Ardhi,TPA unakuwa na akili za upigaji tu.
 
Ukitaka mkeo akuelewe lazima umpeleke mtoto English medium Tena yenye jina Kali Kama
DECEIVINGSHITBASE ENGLISH MEDIUM LEARNING INSTITUTION.
Siku ukitaka mlale mzungu wa nne mrudishe Shule ya Msingi Mwongozo inayomilikiwa na TAMISEMI
 
Walimu wengi wa shule za inglish midiam hasa mikoani Ni wakenya wasio na taaluma ya ualimu.
Huku Dar kidogo tunawadhibiti walimu feki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…