Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Umeweka matango pori
 
... citing ... actually neno "citing/citation" sikumbuki kukutana nalo sekondari. Kama primary za siku hizi ni common word basi kuna mabadiliko makubwa!
 
Kuna watu wanacomment upuuzi ila mleta mada yupo sahihi sana,private nyingi wanakimbia majukumu yao kila kitu wanawasakizia wazazi,jambo ni la kutumia skills za kufundishia na yeye mwalimu ndio naamini anazo hizo skills lakini wanataka ubwete watafuniwe na wazazi,bora mwanao umpeleke hizi hizi za Serikali zenye kujielewa kuliko huko unatoa pesa nyingi halafu majukumu ya ufundishaji mnakuwa walimu wote
 
Acha kabisa mkuu,inakera mnoo.
Wanachokifanya si sahihi, kwani wazazi wengine ni darasa la saba tu unampelekea hesabu za form three? na kila siku inakuwa too much, mimi na kaelimu kangu huwa inabidi nigoogle sana na maswali ya hesabu huwa siwezi kumsaidia. Mtoto atalia kuwa ataenda kuchapwa. Hili jambo lanishangaza sana. Wanapaswa kuwafundisha waelewe then wawape homework.
 
Permanent cultivation

Shifting cultivation
 
Hahaha,pole sana mzee mwenzangu.
Halafu watoto wenyewe ni wadogo na maswali yako advanced mnoo,mtoto haelewi chochote.mtoto yuko standard two,lakini maswali ukiyacheki ni ya secondary kabisa.
 
Partispatory method si kwa waalimu tu na mwanafunzi hata mzazi unahusika. Kama unampa mtoto kiporo cha wali au ugali aende shule au hukumnyonyesha miez 6 ukamkimbia ukamwacha kwa bibi sasa pambana. Elimu sio kulipa ada tu hata mazngra ya nyumbani ni part of learning.
 
Hahaha,pole sana mzee mwenzangu.
Halafu watoto wenyewe ni wadogo na maswali yako advanced mnoo,mtoto haelewi chochote.mtoto yuko standard two,lakini maswali ukiyacheki ni ya secondary kabisa.
Wakuza mitaala wanajimwambafai sana siku hizi, wanaamini mifupa siyo haramu kwa kibogoyo.
 
Kabisa mkuu.
Ualimu ni profession ya watu.
Wamesomea na wanalipwa!!
Kwa Nini mtoto asielewe wanapomfundisha?
Mbona mambo ya kawaida nyumbani anaelewa?
Nadhani kuna haja serikali kufanya ukaguzi wa hizi shule kuona kama walimu ambao ni trained kwa watoto wadogo na pia kuona kama zinatoa elimu inayoendana na hadhi ya kuitwa 'English medium school'. Yaani siku hizi nikion kibao kimeandikwa 'English medium school' naanza kusikia 'kichefuchefu'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…