Binafsi ni mteja na mpenzi sana wa Samsung.sina hakika huwenda wewe ni muuzaji ila mnakosea sehemu.
jukumu la kumuelimisha mteja juu ya huduma anayokwenda au anayoilipia ni la wewe mfanyabiashara.
ndugu watu wamepata hela,wanakuja kwako hawajui chochote zaidi kukariri simu aliyoiona kwa nduguye huko pembeni.nawewe unampokea uko hai hai,kana kwamba unauza pini za mia mia.
muelimishe kabla hajaamua kulipia ili kueupusha malalamiko mbele ya safari.
kwamba simu unalipa kiasi kadhaa,mkataba unasema itahudimiwa muda gani??kipi na kipi??
sasa dukani unakuta wamejaa wale maboy tunaita wadananda,wako lesi kufukuzia 20k za cha juu,lazima mwisho wa picha yatokee haya.
Ni mpenzi sana wa kusoma kuliko kuambiwa jambo na kulichukulia at face value kijuujuu as long as hela yangu na interest zangu zinaweza kuwa affected.
Hata disclosure za kwenye simu kabla ya kukubali, ingawa ni ndefu, binafsi huwa nazisoma ili kuzielewa.
JF ni shule, kuna watu wenye uzoefu mkubwa sana kama Chief-Mkwawa ambao ni very resourceful kwenye haya mambo ya simu, kwa hiyo tunawatumia kuweza kuelewa aspect za simu kiundani kama binafsi nilivyoomba kupata uelewa kwake juu ya machaguo hapo juu kabla ya kununua.
Kwendana na uzoefu wangu, kuna wateja wana uelewa na product kuliko hata muuzaji, and for the case of Mkwawa and some of you, are very exceptional.
Mteja anawajibu kwa sehemu kubwa kupata taarifa nyingi na sahihi kwa kadiri awezavyo ili aweze kufanya maamuzi sahihi yanayoendana na self interest zake.
Hakuna yeyote anayeweza kusimamia vyema maslahi bora ya mteja, kama si mteja mwenyewe kwa sehemu kubwa.