Hizi Software 3 hazitokuja kupata mshindani wa kuzipindua kizazi hiki

Nakubali kabisa kuna kozi yake nliidownload aloo mambo ni mengi nilitoka kapa, ila kichwa ikitulia ntajifunza hiyo kitu inaweza kuwa msaada mbeleni kwenye ulimwengu wa kidijitali
Tatizo la Excel ili uweze kua master Ni lazima uwe unaitumia Mara kwa mara Kwny shughuli za kila Siku,lkn mtu ukiisoma Kama Noval/notes hivi ukajaribu kui-apply kidogo Baada ya muda unasahau kabisa Kama uliwahi kujifunza Excel.

 
Excel ni program kubwa sana. Ina application kama million hivi sema wabongo wengi tunatumia 0.005 ya uwezo wake.
 
MS Excel? Kuna kitu kinaitwa LibreOffice, unakijua?
 
Kuna programmer mmoja niliona documentary alikuwa anatengeneza game, alitengeneza ile game miaka mi 3 yupo ndani ana code tu.
imagine mtu anakaa 3 yrs amefocus na kitu kimoja, kula, coding kulala ratiba inajirudia, hivi mtu wa aina hio unategemea atatengeneza kitu gani? game yake ilivunja rekodi kwenye mauzo, huyo ni mmoja hebu ongeza kama 1000 watengeneze programu moja kwa miaka mi 3. Vitu vingine si uchawi, tusi underestimate uwezo wa akili ya mwanadamu, sisi tunatumia akili zetu kwa level ya basic tu ila wenzetu wanajua kutumia akili zao kwa level ya advance tunabaki kusema uchawi.

Heshima sana kwa hao waliobuni hizo software.
 
Excel imefanyiwa development kubwa sana na ndiyo sababu inaendelea kua program kubwa zaidi.
Wanafunzi na watafiti wengi wanafanya tafiti zao kwa kutumia excel hivyo wanaendelea kuidevelop zaidi ili kurahisisha mambo
Kila anayetumia kwa matumizi yake anatafuta namna ya kurahisisha shughuli zake zaidi hivyo anadevelop zaidi
Imegusa kila nyanja
 
I concur
 
muhindi wangu Vinod anaigonga excel sheet kwenye pc ya ram 8gb mpaka pc inachanginyikiwa inaanza kulia, kwa mimi najua kutafuta totals na average ya sums tu.. yeye anajua kufanyia funtions nyingi na kwa wakati mchache mno kwa kutumia excel shortcuts na anacross chek kwa excel tena. wahindi wengi wahasibu ni diploma level, wanaongezea kusoma tally, sap na adv. excel huwapati kwenye market ya uhasibu wa viwanda si kama sisi degrees, cpa's masters ila bado unaogopa kushika pc ukukotoe uhasibu.
 
Mnapotaja maajabu ya excel muwe mnaorodhesha kabisa maana sisi wengine miaka yote huwa tunaipita kama hatuioni. Yaani mimi hata budget nilikuwa natengenezea kwenye ms word kwa kuchora jedwali na kukaa na kikokotoo pembeni.

Juzi tu ndio nimejua kumbe ukiwa na excel inamaliza kila kitu yenyewe.
 
Kama hutojali tafadhali shuka hizo firm 6 mkuu...... ili tuziingilie chimbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…