Hizi taa za Jokate Mwegelo mbona bei ghali hivyo jamani au zina link na satelites?

Hizi taa za Jokate Mwegelo mbona bei ghali hivyo jamani au zina link na satelites?

Umepiga gharama ya mkandarasi ? Procurement n.k au unadhani hiyo hela ni taa peke yake?
Kwanza eneo lazima ifanyike survey, uandaliwe mchoro, baada ya hapo tender itangazwe au wafanye selective tendering, baada ya kupata mkandarasi kazi inaanza...
Kumbuka kuna kuchimba shimo ili uweke base ya kubeba hizo poles (nguzo) nazo ni gharama pia, Usisahau hiyo base inakua na reinforcement kuipa uimara,

Ongeza hili katika akili yako ni kwamba watu wanaweza kuandaa michoro lakini specification za material siyo locally yaan inabidi uagize nje, piga gharama ya shipping, clearing & forwarding...
Pamoja na kufanya mchanganuo mzuri lakini je ilikua na umuhimu gani wa kuweka taa za ghalama kubwa kiasi hicho?ofsi ya mkuu wa wilaya inayolindwa masaa 24 taa za ghalama kubwa kiasi hicho kwa nchi masikini kama Tanzania he ni fait what if kila mkuu wa wilaya aige kuweka taa kama za mkuu wa wilaya ya temeke pesa za walipa Kofi zitatuika shi ngapi? Naona huyo jipu lake limeiva linasubiliwa kutumbuliwa
 
Umeangalia tu taa kama taa kwa maana ya balbu na cover yake au?. Kuna solar system hapo, kuna sensing system ya kujua kama ni mchana au jioni, kuna mlingoti wa chuma na zege la kuweka, gharama za vibarua. Umewaza yote hayo? Pia nilitegemea ungeleta estimation ya gharama ambazo unadhani zingekuwa sahihi. Kusema m 3 ni nyingi bila kuwa reference point inakuwa haieleweki, nyingi ukilingalisha na nini? Hiyo ni relative term
Jamaa anajua taa ni zile za kichina tu sebuleni kwake!
 
Au labda ni teknolojia kama ya Mossad , CIA? isije ikawa zina satellite ndani, taa 32 kwa milioni 102 ukipiga hesabu ni kama vile taa moja ni tshs 3,187,000.

View attachment 1835927View attachment 1836188
Mjuu unajua bei ya nguzo moja ya chuma ya hizo taa? Hii sio taa wanayoenda kufunga kwenye socket nyumbani. Na si kila kitu ulichoona Alibaba bei rahisi kina ubora wa kununuliwa au ndio bei elekezi. Waacheni watu wafanye kazi.
 
Sawa wahusika watasikia ila sijajua ni bei brand gani hasa wanatumia serikali.

Kuna contractor amefanya project huku niliko , Serikalini imemlipa solar system moja kwa 2.5 mil , inashangaza kama kwa staili hii kumbe zinauzwa 600k?,na walivyo wapuuzi ziko aina tofauti tofauti kwenye barabara za mradi huo huo.

Zingine zina Waka vizuri zingine zina mwanga hafifu zingine zina milingoti mirefu zingine mifupi yaani ni vurugu tupu,no uniformity kabisa,na inaonyesha wanamwambia supplier alete bila hata kumpa specs zozote ndio maana wanaweka hizo bei.

Kwa taarifa tuu ni kwamba hizo bei sio Dar tuu bali ni kote ndio bei ya Serikali hiyo kwa taa moja.

Nitafuatilia kujiridhisha kwa nini bei inakuwa kubwa wakati kumbe haizidi hata mil.1 kwa nguzo 1 hadi kuisimamisha.
 
Siwezi shangaa, watu utoa udongo Kenya hadi tz kwa ajili ya greenhouse, unaweza kujiuliza ila si kila udongo ni sawa!
 
Unakubali kabisa tena na kusema safi sana nchi maskini kama Tanzania zitumike sh milioni 100 kwa ajili tu ya taa tena mbele ya ofisi ya DC?
Hapo Temeke hospital mita 300 tu toka hapo ofisini kwake hakuna vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa na tumeambiwa tujiandae kwa Wave no 3 ya Covid 19 so yeye ameona hizo taa ni muhimu kuliko afya za wanaTmk? Hiyo budget ya kijinga hivyo madiwani wameipitisha lini? Mheshimiwa DC kwa temeke kama hii ndiyo style then unaanza vibaya.
 
hilo ndilo swali langu haswa, milioni 100 inaweza saidia kupunguza hata kero ya takataka au kitu kifaidisha hata kata nzima
Mnako elekea mtataka hata viti visinunuliwena majengo ta ofisi yasijengwe fedha ipelekwe kwenye hayo mnayo ita maendeleo ingawa hata sielewi mnapo sema maendeleo kwenye vichwa vyenu mnamaanisha nini
 
Hapo Temeke hospital mita 300 tu toka hapo ofisini kwake hakuna vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa na tumeambiwa tujiandae kwa Wave no 3 ya Covid 19 so yeye ameona hizo taa ni muhimu kuliko afya za wanaTmk? Hiyo budget ya kijinga hivyo madiwani wameipitisha lini? Mheshimiwa DC kwa temeke kama hii ndiyo style then unaanza vibaya.
Huwezi kumaliza matatizo ya watanzania wote na hasa kwa nchi masikin kama tanzania, hayo unayo yasema wewe yana mipango yake na budget zake, kwa sababu badae mtaanza aooh! Watanzania wanakula kutwa mara moja halafu Dc anapanda gari! Yaan mawazo ya maskini yapo kimaskini maskini mda wote

Sasa wewe nyumban kwako umenunua li TV tena liflat smart LED 42" la nini wakati huko kijijini kwenu una ndugu zako tena wa damu wanatembea peku au hawana hata viatu na nguo nzuri za kubadilisha?
 
hebu piga picha kwamba jiji la daresalaam lingekuwa giza na hakuna taa kuongozea magari barabarani, unafikiri changamoto ya vyoo ingemalizwa kwa kulinyima taa jiji la daresalaam?!? wakati tunanunua ndege ya rais mramba nadhani alituambia watz tutakula hata manyasi lakini ndege lazima inunuliwe, je, tulikula hayo manyasi!?! kwa mtazamo wako nini kilipungua kwenye maisha ya watz?!? mabilioni mangapi yanatumika kuwalipa posho waheshimiwa hilo kwako ni sawa tu, lakini 102mn za dc wa temeke zinataka kukunyima usingizi. those things are peanuts kwa watz nenda kwenye mambo ya msingi ambayo yatabadilisha maisha ya watz, acha kulalamikia vijisenti hivyo, hata vilivyo vilivyopelekwa newjersey hukuenda kushtaki mahakamani kumdai jamaa avilete visaidie kujenga vyoo vya watoto wetu mashuleni. Mwlm. Nyerere aliwahi kutuasa watz tuwe tunaongelea masuala sio kahawa
Wewe inaonekana hujui umuhimu wa kidogo ulichonacho.hakuna kikubwa bila kidogo.hayo ya mramba sijui matakataka gani bado ilikua ni ujinga kama ujinga mwingine.inawezekana usione impact yake moja kwa moja kwasababu huwezi kujua ni mambo gani muhimu yalishindwa kutekelezwa kwa wakati kwa sababu ya ukosefu wa fedha baada ya maamuzi yale.Hadi leo tunaongelea vitanda mahospitalini kwasababu kuna maamuzi ya ovyo yakutoa vipaumbele kwenye mambo ya ovyo yanayofuja kodi za nchi badala ya mambo ya msingi.Sasa wewe unatetea la jokate kununua taa moja kwa bei hiyo unadhani kila mkuu wa wilaya nchini naye akifanya yanayofanana na ilo itakua ni fedha kiasi gani imepotea kwa mambo ya ovyo.au unataka hadi CAG aje aseme ndo ujue halikua sawa.jifunze kufikiria mbali zaidi na ujue kamwe hatuwezi kupiga hatua bila kuanza kua na nidhamu ya muda na fedha ata katika vitu vidogo.
 
Kwahio nyie wapuuzi mnahisi Jokate ndie mratibu wa wizi? Kama ni Deal kuna mtu ameseti ila sio Jokate
 
Kwahio nyie wapuuzi mnahisi Jokate ndie mratibu wa wizi? Kama ni Deal kuna mtu ameseti ila sio Jokate
Ila maduka mawili mpaka mataa ya pale machinjioni wamewekaa mataa usiku full kuwakaa...isje kuwa mi mpango wa Dmdp
 
duuh, na cc watz kwa kweli!?! tunalalamikia milioni miamoja na mbili kwa kitu ambacho utakion na kizuri tena wilaya ya temeke yenye vyanzo vingi tu vya mapato je mtu wa wilaya ya buhigwe si atalalamikia hata hospitali!?!. wajameni hizo taa hata wewe ukiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo sidhani kama utazing'oa uweke karabai. wajameni chapeni kazi mjenge nchi na pia mjenge purchasing power zenu ili msiwe mnalalamikia hata vitu vidogovidogo tu. anyway mwenye fungu ni mkurugenzi akiona ni expensive ataomba ushauri kweny baraza la madiwani nafikiri na mleta uzi ni diwani utakataa
Mkuu ndio akili yako hii? Tukiwa na kizazi chenye akili Kama hizi Ni Janga kubwa la Taifa.
 
duuh, na cc watz kwa kweli!?! tunalalamikia milioni miamoja na mbili kwa kitu ambacho utakion na kizuri tena wilaya ya temeke yenye vyanzo vingi tu vya mapato je mtu wa wilaya ya buhigwe si atalalamikia hata hospitali!?!. wajameni hizo taa hata wewe ukiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo sidhani kama utazing'oa uweke karabai. wajameni chapeni kazi mjenge nchi na pia mjenge purchasing power zenu ili msiwe mnalalamikia hata vitu vidogovidogo tu. anyway mwenye fungu ni mkurugenzi akiona ni expensive ataomba ushauri kweny baraza la madiwani nafikiri na mleta uzi ni diwani utakataa
Unafurahia utakatishaji wa fedha ?

Watanzania mmerogwa na nani ?
 
Back
Top Bottom