Hofu yatanda kwa Wabunge wa CCM, baada ya Tulia Ackson sasa Mrisho Gambo ataka jimbo la Arusha ligawanywe

Anaweweseka hata kule MURIET CCM haina ushawishi wa aina yoyote.. Labda NADO & TERATI walau watapata kura kadhaa.
 
Sasa Chadema kujitwalia majimbo 2 in 1.....😀😀😀😀
 
Huko tuendako,tuombe tu uhai,tutawaona wakitamani hata kugawa nyumba zao na kuzikana,kwani uovu hulipwa hapa hapa duniani 🏃🏃
Kama Petro alimkana Yesu, basi wao ni nani wasitamani hata kuzikana au kugawa nyumba zao???
 
Acha uongo wewe
 
Tayari Bunge tulilo nalo ni kuwa sana. Hatuhitaji kuongeza idadi ya majimbo, badala yake tufikirie kuyaunganisha.
Hoja kuwa kugawa jimbo kuna tija kwa kuwa baadae linaweza kuwa halmashauri na baadae wilaya, ni mufilisi.
Kwenye utandawazi na e-government hata eneo likiwa kubwa bado maendeleo yatawafikia wananchi.
Hatujawahi kusema kuwa wilaya iwe na idadi kadhaa ya kata au mkoa uwe na idadi kadhaa ya wilaya. Tunachoweza kudefine ni kwa mfano kuwa kila watu 5,000 wawe na kituo cha afya. Kwamba tuna vituo vya afya 30 basi ndio iwe wilaya? Hapana. Ukiwa na mtandao na uwajibikaji mzuri, kiongozi hahitaji kukanyaga kila inchi ya Tanzania ili kuleta maendeleo. Kama maendeleo hayaji hadi kiongozi afike, then kuna tatizo kubwa - tushughulike na hilo maana bila kumaliza hilo hata kila kata ikawa jimbo au kila wilaya tukaigeuza kuwa mkoa bado hatutafanikiwa.
Tusiwaongezee mzigo wananchi kwa tamaa zetu
 
Ujue mzigo ni wetu wananchi tunaowalipa kwa kutumia kodi na tozo mbalimbali tunazotozwa kila siku !!
Kuna sehemu zingine huduma azifiki Kwa wananchi inabidi majimbo yaongezwe Kwa sehemu zenye uhitaji.
 
Kama vipi majimbo yasigawanywe. Na ikiwezekana hata majimbo mengine yaunganishwe Ili yawe machache tuone kama Chadema mtachomoa.
 
Acha uongo wewe
Thibitisha!
Kwani Huko mnapofanya ulinganishi au niseme kule mnapotaka kuiga aina ya Utawala wa majimbo, walianzaje Kugawa hayo majimbo?Sababu kuu zilizowafanya kuwa na yele majimbo yalikuwa ni nini?
 
Wanyakyusa na wasafa wakimtoa Dr Tulia bila sababu za msingi basi itabidi wapimwe akili kama ziko sawa.
Sugu alishamaliza mda wake aangalie mambo yake kwani hakuna watu wengine huko Chadema? Jimbo limekuwa mali ya sugu, kwa nini baadhi ya wabunge wanataka kuwa wafalme majimboni, ni tabia mbaya na inataka kuzoeleka, hii ni kwa vyama vyote.
 
Mbona Lowassa , Makamba na Kikwete waliporithisha majimbo watoto wao hukuja humu JF Kuropoka ?
 
we unajua maana ya ukubwa wa jimbo? we akili yako ni km hao nyumbu wa Ngorongoro. Jimbo la Arusha lina wakazi 617,631 na jimbo la Ngorongoro lina wakazi 273,349. Jimbo la Arusha ni zaidi ya mara 2 ya jimbo la Ngorongoro. au umehesabu na wanyama? Hivi kwanini wapumbavu km wewe huwa wanazaliwa? Nimesikitika sana. Hata hivyo sishabikii ugawaji wa majimbo kwani nashangaa mbunge moja anashindwaje kuhudumia wakazi km laki 7.
 
Haya matusi natukanwa mimi au Mrisho Gambo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…