Hoja binafsi: Vyama vya siasa viwe makini sana kwenye uteuzi wa wagombea wenza katika chaguzi zijazo ama sivyo Katiba imulikwe

Mnapochagua Mgombea mwenza mjue ya kwamba Raisi akifariki yeye ndio anashika nafasi ya Uraisi .kwa hio mara ingine mjue mnachagua mtu ambe yupo tayari kushika na kuongoza nchi kuliko kuongozwa.ata sijui kama nimefahamika ,maana watanganyika wagumu kufahamu.
 
TL na Salum Mwalimu.....au unamaanisha nini..
 
kwahiyo unataka kusema Mama hafai.

Pro-Magufulism mnateseka sana
 
Ni kweli bro.
Ile seriousness inayotumika kumpata running mate wa mgombea uraisi waTanzania IPO kimdhaa kimdhaa. tofauti na umakini unaotumika kumpata rais wa Zanzibar.

Kuna ule upofu kwamba rais ni MKUU mno na hafagi njiani, na hanaga record hiyo..

kwahivyo mgombea mwenza ni sub tu wa kuridhidhisha kanuni.
Ni sub ambayo Mara nyingi haina matumizi kama ya kipa.

Ni kama leo tunavyoona ugumu ulioje Philip mpango kuwa rais kabla ya 2025.
Hili lipo kwa vyama vyote.
Hoja hapa sio kubeza wagombea mwenza waliopitishwa na vyama vyao.ila ni kuvikumbusha kuweka attention kubwa kwny nafasi hizi.

Kuna mwaka CCM. Baada ya kuona gharib bilal ana nguvu na ushawishi MKUBWA Zanzibar wakati wao tayari walikuwa wana jina lao mfukoni (Shein)
Wakaona ni heri Bilal apozwe kuwa mgombea mwenza na baadae kuwa makamu Wa Rais, kuliko bilal kuwa raisi kule.

Likewise, heri Maalim self (now late) awe makamu wa kwanza na sio wa pili,
wakiamini umakamu wa pili ni ukubwa Wa geresha.
 
Nchi iongozwe na kamati ?
 
Zanzibar ni koloni la Tanzania bara kwa mustakabali wa usalama wa Tanzania bara.

Hivyo makoloni ya sasa hayakaliwi kwa nguvu bali kwa akili na maarifa mengi.

Ni watanzania wajinga tu ndiyo watakuwa tayari kuachia Zanzibar ijitawale.
 
Ni kweli vyama vyote vilikuwa vinadharau sana juu ya hili kwa kuchagua wagombea wenza incompetent. Ila kwa hili lililotokea naamini litakuwa no funzo tosha.
Mgombea mwenza yupi ambaye alikuwa ni incompetent kwenye chaguzi zote ?

2015 wagombea urais ndiyo walikuwa incompetent kuliko wagombea wenza.
 
Mwacheni Samia afanye kazi. Mwendazake alichaguliwa na watu ila Samia kaletwa na MUNGU.

Na siku zote penye ukweli uongo hujitenga!
Dhalimu alichaguliwa na watu ama vyombo vya dola na tume ya uchaguzi?
 
Nahisi kuna fundisho watakuwa wamelipata hao wanaochagua wagombea wenza, hili la sasa lililotokea itakuwa kama CASE STUDY.

Miaka mingi wagombea wenza walichukuliwa kama watu ambao majukumu yao yanaishia kwenye KERO ZA MUUNGANO na mambo ya MAZINGIRA tu na watu waliopoa(Shein,Gharibu,Ali Jumaa) sana.
 
Nadhani sasa tushapata funzo kubwa sana Kama nchi tabia ya kuweka weka watu kisa tu kutimiza kanuni au huruma na kuwapa watu fulani kipaombele nadhani sasa itaishia hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…