Ni kweli; hata mimi nimeshaona tatizo la kikatiba hata. Ile katiba ya zamani ilikuwa inasema rais akifa, basi uchaguzi mwingine mdogo wa rais unafanyika kujaza nafasi yake kama ambavyo anapokufa mbunge nafasi yake inajazwa kwa uchaguzi mdogo wa bunge.
Mabadiliko ya kusema makamu wa rais anakuwa automatic rais na akishachukua madaraka anafanya lolote atakalo ikiwa ni pamoja na kupangua serikali aliyokuta linaweza kuwa na unintended consequences kwa mustkhabali wa nchi. Inabidi katiba ingaliwe upya namna ya kurithisha kiti cha uraisi aliyefariki na kuongeza checks and balances zaidi kwa mrithi wa kiti hicho. Njia rahisi sana ni ile ya kuundwa kwa kamati ya urais itakaokuwa inaongozwa na aliyekuwa Makamu wa rais kabla ya kifo cha rais; kamati hii uhai wake utakwisha baada ya uchaguzi mkuu unaofuata. Halafu rais aliyerithi asiwe na power zote za rais aliyechaguliwa; sehemu ya powers za rais aliyechaguliwa ziwe mikononi mwa kamati hii. Utaratibu huu utapunguiza kidogo tamaa ya madaraka kwa makamu wa rais.
Kusema tu kuwa waliaminiana wakati wa uchaguzi siyo hoja kabisa, binadamu huamini wenzao walio hai tu, baada ya vifo husahauliana kabisa. Kesi hii ya kifo cha Magufuli imeonyesha tafsiri hiyo kwa uwazi sana tena kwa muda mfupi sana. Ndani ya mwezi mmoja tu wa kifo chake, mkataba wa bandari ya Bagamoyo uliopingwa na magufuli unaaza kujadiliwa tena!