Hoja fikirishi: Nini kilitokea kabla ya Mwanzo 1:2

Mangi Meno

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2024
Posts
292
Reaction score
895
Biblia katika kitabu cha Mwanzo 1:2 inaeleza

Mwanzo 1
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Katika mstari huu kuna vitu vya kujiuliza ambavyo Natumai wajuzi wa haya mambo mtanisaidia?
1. Kwanini nchi ilikuwa ukiwa tena utupu?
2. Kwanini nchi ilizingirwa au jazba na maji?
3. Kwanini giza lilitanda juu ya uso wa vilindi vya maji?
4. Kwanini Roho wa Mungu alitulia juu ya uso wa maji?

Nakaribisha mawazo huru tuweze kutengana wana JF.

Please huu sio uzi wa kidini.
 
Hapa tayari ushafanya logical contradiction.

Unasema kwamba nchi ilikuwa tupu (bila chochote).

Halafu tena unasema nchi ilizingirwa na maji na ilikuwa na giza.

Hii tayari ni logical fallacy.

Hayo maji yalitoka wapi?

Hilo giza liliumbwa na nani?

Huyo Mungu aliumbwa na nani?
 
Ndio maana mkuu nimeleta kwa wadau tujadili hilo.
 

Tafsiri ya Kiswahili ndio imeweka neno ukiwa, lakini kwenye Biblia zilizoandikwa Kiingereza neno ukiwa limetajwa kama formless...

Genesis 1:2
Now the earth was formless and empty, darkness was over the surface of the deep, and the Spirit of God was hovering over the waters.

Kutoka kamusi ya merrian-webster, neno formless limepewa tafsiri kama ifuatavyo:

1: having no regular form or shape
2: lacking order or arrangement
3: having no physical existence

Hivyo inaonesha dunia ilikuwa ni eneo lisilo na umbo pangiliwa
 
MUNGU aliumbwa na nani? and begore Dunia kuumbwa . How was the situation. And kwa nini binadamu tuliumbwa only on earth and not other planets. Je mungu wa earth.ndo.huyo huyo.wa pluto.mars.etc?
 
Na aliyeandika alikuwa wapi
 
Huu ndo mstari ulikuwa unawapa nguvu falme za giza kwamba giza lilitangulia nuru,kulikuwa na pin kubwa sana hapo mpaka Muumba mwenyewe alipotutoa hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…