Hoja fikirishi: Nini kilitokea kabla ya Mwanzo 1:2

Hoja fikirishi: Nini kilitokea kabla ya Mwanzo 1:2

Inapimwa kwa madini unayotoa pili kuzijua baadhi ya siri ya vitu.

Madini kwa misingi ipi? Unajua madini ni very subjective? mfano kuna watu bila kuongelea habari za wokovu bado haujatoa madini, wengine kama haujaongelea habari za mafanikio na utajiri hapa duniani bado haujatoa madini, wengine bila kuongelea ndoa bado haujatoa madini, wengine bila kugusia uponyaji na kuwaonyesha kwamba njia unayotumia inaponya bado haujatoa madini n.k

Kila mtu ana kitu anachotaka kusikia ili ajue umetoa madini so bado swali linabaki pale pake BY WHOSE STANDARDS?
 
Hakuna siri yoyote kwenye Biblia zaidi ya hadithi za uongo njoo utamu kolea.

Baada ya kuona kwamba hadithi za Biblia hazi make sense, Wakaunda dhana uchwara kwamba lazima uwe na imani ya juu au uelewa wa roho mtakatifu kuielewa Biblia.

Kumbe ni ujinga tu.

Biblia ni hekaya kama zilivyo hekaya za Abunuwasi, Esopo, kalume kenge na Alfu lela ulela.
Na Quran je nayo ni hadithi hadithi?
 
Madini kwa misingi ipi? Unajua madini ni very subjective? mfano kuna watu bila kuongelea habari za wokovu bado haujatoa madini, wengine kama haujaongelea habari za mafanikio na utajiri hapa duniani bado haujatoa madini, wengine bila kuongelea ndoa bado haujatoa madini, wengine bila kugusia uponyaji na kuwaonyesha kwamba njia unayotumia inaponya bado haujatoa madini n.k

Kila mtu ana kitu anachotaka kusikia ili ajue umetoa madini so bado swali linabaki pale pake BY WHOSE STANDARDS?
Katika engo hizo mtu layerman na wiseman utawajua tu,aliyedeep na asiye deep
 
Katika engo hizo mtu layerman na wiseman utawajua tu,aliyedeep na asiye deep
Kwa standard zipi? Vipo kama huyo unayemuona layman mwengine anamuona ni "wiseman"? Hauoni kama italeta dillema? Nataka kujua standards za kumjua huyo mtu anayetoa "madini" nani aliziweka .
 
Hapa tayari ushafanya logical contradiction.

Unasema kwamba nchi ilikuwa tupu (bila chochote).

Halafu tena unasema nchi ilizingirwa na maji na ilikuwa na giza.

Hii tayari ni logical fallacy.

Hayo maji yalitoka wapi?

Hilo giza liliumbwa na nani?

Huyo Mungu aliumbwa na nani?
Mpak hapo haupo fit rohoni. Maswali unayujiuliza ni ya mwili, maana yake majibu utakayoyapata lazima yatakuwa na limitations tuu, uchache.

Ukijiuliza ki roho utapataa majibu yote ya mwili..hata kama ni miaka milioni imepita.

Asante
 
Siri tena
Nimeaidie kuwa sio siri...amemaanisha codes....biblia ina codes nyingi ajabu.

Na rohoni ndio kuna codes tupu.

Chukulia mfano unaota umepigwa pingu miguuni na mikononi. Wajuzi wa tafsiri wanakuambia kuwa hapo ujue mambo yako yote yashadhibitiwa na mbaya wako....yaani hautofanya kazi ya mikono ukafanikiwa, au safari, au chochote kile cha kimaendeleo.

Lakini kwenye ulimwengu wa roho, umeota tuu kuwa umepigwa pingu, au umefungea mikono na miguu.

So kila kitendo na kila kipengele kwenye ulimwengu wa roho kina maana tena sana

Sasa kwenye biblia, unaeza kuta ka kimstari kamoja tuu kumbe kakawa na maana nzito ambayo tafsiri yake ukaandika vitabu na vitabu.

Happ kwenye dunia kuwa ukiwa na utupu, niliwahi kusoma sehemu tafsiri yake, (na imeelezewa kwenye isaya hamsini na ngapi sijui...sikumbuki vizuri) kuwa dunia iliwahi kukaliwa na watu wengine na kuiharibu vibayavibaya yaani...

So process za hapo mwanzo moja ni mamilioni ya miaka kupita.

Na ni nguku kujua zaidi mambo mengine kwa sababu uandishi wa biblia ni kwa aajili ya kumtukuza Mungu pekee, na sio wanadamu, mizimu, majini, wala shetani.

So shika hili. Kila kilichoandikwa kwenye Biblia ni kwa ajili ya Kumtukuza Mungu na ukuu wake...na sio Mwanadamu. Sanasana mwanadamu amepewa nafasi kuonesha jinsi anavyopendwa na Mungu...basi
 
MUNGU aliumbwa na nani? and begore Dunia kuumbwa . How was the situation. And kwa nini binadamu tuliumbwa only on earth and not other planets. Je mungu wa earth.ndo.huyo huyo.wa pluto.mars.etc?
Mungu kaumba ulimwengu mzima. Wewe mpaka sasa unajua dunia na visayari vichache.

Hata shetani ni wa ulimwengu mzima, wewe unamjua shetani wa hapa duniani, haujakutana na wa andromeda, wala far side of the universe hukooo.
 
NITAJARIBU HOJA MOJA PEKEE;

WATAFITI NA WANA THEOLOJIA;
Mara nyingi katika kuyachimba maandiko na kutafiti nyakati za biblia, wamefanya tafiti mbalimbali ili kujiridhisha majira na nyakati ambazo vitabu mbalimbali katika biblia kuwa viliandikwa nyakati gani katika historia.

Katika utafiti huo, kitabu cha AYUBU kimewapa wakati mgumu kujua kuwa Ayubu kuwa;
  • Aliishi nyakati gani?
  • Nchi ya Usi alikoishi Ayubu ilipatikana wapi?

Kwa kukosa majibu ya maswali hayo, hawa watafiti wa maandiko wengi wao wamejaribu kwenda mbali zaidi na kuamini;
-Huenda kulikuwa na dunia au maishi mengine kabla ya sasa
- Huenda Mungu aliiangamiza dunia ya kale kabla ya hii mpya ambayo labda nchi ya Usi alipoishi Ayubu ilipatikana.

Note;
Huu ukiwa wa dunia unaoongelewa Mwanzo 1.2 huenda umetokana na kutoweshwa kwa viumbe wa dunia ya Mwanzo.

Note; nilisema najaribu
Upo sahihi, umejaribu vyema. Viukbe wa mwanzo walikuwepo ndio wakazingua, Mungu akawafutilia Mbali. Ndio maana kwa nuhu walipozingua wakafutiliwa mbali kwa maji. So mchezo unekua ukiendelea, na sisi tunavyozingua hivi...shauri letu..
 
Actually!
Nikiri kwamba Hii Mada Inachanganya Sana na Sidhani kama Ni Mada salama Sana kwa Wakristo kwa Sababu inaweza Ikaibua Vitu ambavyo hawakuwahi kuviamini kama vipo.. Ila Kwa wayahudi Na waislamu kwao Sio Mada Ngeni sana ila Nitaenda Kuichambua Kwa mapana Yake so tutaelewana vizuri..

Cautions!
Ninaweza Kuandika Maelezo marefu Sana So ili kuelewa Every single dot inabidi Kuyasoma Yote..na ieleweke kuwa Sipo kutetea ,Kutangaza au Kuidogosha/Kuitukana Imani ya Mtu yoyote, I am just here to explore Kijielimu nilicho nacho kwa Wote ili tupate kauelewa niliko nako..


So let me start!..
Waislamu na Wayahudi Wanakubaliana kwamba Kabla ya uumbaji (Ambao tunaufahamu) ulikuwepo Uumbaji mwingine ambao Ulipitia Upotevu na Ukaadhibiwa..

Waislamu wanaamini Kuwa kabla ya Binadamu Waliumbwa Majini kwanza Na Majini walipofanya Dhambi na Uharibifu waliadhibiwa Ikiwa ni pamoja na Kufukuzwa Duniani (Kutoikalia Dunia)..

Wayahudi wanaamini Uumbaji Ule uliharibiwa na baada ya Kuharibiwa Binadamu wa kwanza aliyefanya Dhambi "Lilith" alisababisha Dunia iharibiwe na Baadae Kutokana na Hasira aliyokuwa nayo Mungu aliharibu kila kitu ila baadae ilibidi aweke kila kitu sawa..

ili kujibu Mada hizo kwa Facts tutapitia 3 Concepts..
  • Textual Analysis of Genesis (Uchambuzi wa Andiko)
  • Agreed Theorism
  • Esoteric Knowlege and Kaballah

Textual Analysis of Genesis (Uchambuzi wa Andiko).

Tuanze na Andiko lenyewe lenye Utata Bere'shit (Mwanzo) 1:1-2

בְּרֵאשִׁית בָּרָא אֱלֹהִים אֵת הַשָּׁמַיִם וְאֵת הָאָרֶץ׃
וְהָאָרֶץ הָיְתָה תֹהוּ וָבֹהוּ וְחֹשֶׁךְ עַל פְּנֵי תְהוֹם וְרוּחַ אֱלֹהִים מְרַחֶפֶת עַל פְּנֵי הַמָּיִם׃

Inatamkika Hivi:

Bereshit bara Elohim et hashamayim ve'et ha'aretz.
Veha'aretz hayetah tohu vaBohu vechoshech al penei tehom veruach Elohim merahefet al penei hamayim.


Tafiri Iliyorasimishwa (Ambayo baadaye nitaielezea)

"Hapo mwanzo, Mungu aliziumba mbingu na dunia
Nayo dunia ilikuwa ukiwa, tena utupu; giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, na Roho wa Mungu alikuwa akitanda juu ya uso wa maji."


Neno Nililolowekea Alama Nyekundu Ndo msingi Hasa wa Kuchunguza Andiko hilo Ili kupata maana Halisia..
Neno Tohu vaBohu" (תֹהוּ וָבֹהוּ), Ukilingalia Kwa haraka haraka Unaweza Ukasema Ni neno Moja tu ila Hilo ndio neno ambalo Linaweza Kubadili Asili ya Uumbaji wote au kupreserve aslili ya Uumbaji kama Wakristo wanavyoiamini

Neno Tohu (תֹהוּ ) lina maana zifuatazo confused State, chaos au Chaotic state pia emptiness na formlessness..

Pia Va humaanisha "na" na Hiyo Bohu humaanisha Void au Emptiness..

Sasa je Yanaweza Kutafsiriwa Vipi unaweza Ukasema Kuwa Ni Chaotic Void (Vurugu Iliyotawala, Vurugu iliyozidi, Machafuko yaliyokithiri au Utupu wenye machafuko au Jangwa la Machafuko)..

Kingine Tafsiri ya Neno Roho wa Mungu haijakaa Poa kwa sababu Neno ve Ruach (וְרוּחַ)halimaanishi roho Peke yake Linamaanisha Upepo Mkali pia "Tungeweza Kusema Upepo mkali Kutoka kwa Mungu" yaani "veruach Elohim"

So Tukiacha maana Halisi tuliyoambiwa Pia Ukiangalia maana Moja moja Unaweza ukaaandila Tena Hicho kipande cha Aya Hivi.. (Mwanzo 1:1-2

"Hapo mwanzo, Mungu aliziumba mbingu na dunia
Nayo dunia ilikuwa kwenye Machafuko na ukiwa, tena utupu; giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, na Upepo Mkali kutoka kwa Mungu ulikuwa ukitanda juu ya uso wa maji."


Umeona Tulivyofanya Tafsiri Ya maneno mawili Maana Ya Andilo Ilivyobadilika?

Kwahiyo kwa Kusema Kuwa Dunia Iliumbwa Ukiwa Na Tupu Wayahudi na Watu wa Esoteric wanakataa hiyo kitu..
Tusome kwenye..Isaya 45:18

"Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa......."

Na Pia hata Tukisoma Kwenye 2 Petro 3:5-6, tunasoma:

"Kwa kuwa wanapuuza jambo hili kwa hiari yao, ya kuwa zamani za kale kulikuweko mbingu pamoja na nchi iliyotokana na maji, na kwa maji ..."


Wanatheolojia Wengi sana Wanaamini kwamba Mungu aliumba Kawaida Ila Baadaye Kukatokea Tatizo mahali Vita na Baadaye Dunia Hiyo ikaangamizwa na Baadaye Mungu akaanza Kuumba Mtu atakayeweza Kuitunza na Kuilinda..

Na wengine wanasema Kwamba Hata kitabu cha Yeremia 4:23-26 Haikuwa Tabiri wa Unabii Bali ilikuwa Ni Historia Ya Ilivyotokea Baada ya Uuambaji wa kwanza...

Yeremia 4:23-26
"23 Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru.

24 Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko.

25 Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao.


26 Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana (Edeni) limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za Bwana, na mbele za hasira yake kali."


Na Hiyo Verse Ndo inaelezea zaidi Kuhusu Mwanzo 1:2 tunayoitafuta Sasa..

Swali Ni kwamba Nini Kilifanyika Baada ya Uumbaji na Hapo Ndo inakuja 2nd concepts Inaitwa Gap Theory View attachment 3255592
View attachment 3255593


Sasa Hapa ndo Kuna Utata Wote..

Ngoja kwanza Nipumzike 😀😀
min -me | Mangi Meno | Aaliyyah

Kuna swali?
Man umeua...ushafungus codes za awali kiulainiiii
 
Ukitaka kumtawala mtu basi mfanye kipofu kwenye mambo fulani.

Mungu ametufanya vipofu kwenye baadhi ya mambo ili atutawale.
Na wewe tafuta wako wafanye vipofu ili utawale kama ni rahis
 
Back
Top Bottom