Hoja fikirishi: Nini kilitokea kabla ya Mwanzo 1:2

Hoja fikirishi: Nini kilitokea kabla ya Mwanzo 1:2

Wakati Nabii Mussa anaandika kitabu cha Mwanzo ilikuwa imeshapita miaka 3500 soma vizuri.
Hapa na kupinga kuna sehemu unashindwa kuelewa.
Umri wa dunia unakadiriwa kuwa takriban bilioni 4.54 (4,540,000,000) miaka. Makadirio haya yanatokana na uchunguzi wa miamba ya zamani duniani na vipimo vya isotopu za elementi kama uranium na lead. Pia, wanasayansi hutumia vipimo vya miamba ya anga kama meteorite ili kusaidia kuthibitisha umri huu.
 
Tafsiri ya Kiswahili ndio imeweka neno ukiwa, lakini kwenye Biblia zilizoandikwa Kiingereza neno ukiwa limetajwa kama formless...

Genesis 1:2
Now the earth was formless and empty, darkness was over the surface of the deep, and the Spirit of God was hovering over the waters.

Kutoka kamusi ya merrian-webster, neno formless limepewa tafsiri kama ifuatavyo:

1: having no regular form or shape
2: lacking order or arrangement
3: having no physical existence

Hivyo inaonesha dunia ilikuwa ni eneo lisilo na umbo pangiliwa
Hiyo darkness ilitoka wapi?
 
Kwenye hili mimi naweza kusema:
1. Tusitafsiri vilivyoandikwa kama vilivyo, ikumbukwe Biblia imepitia tafsiri nyingi sana kabla ya sisi kuanza kuisoma karne ya 20 na 21, lugha za kale ukute Kuna misamiati ilikuwa na maana nyingine kabisa kuliko kile "tulichokielewa"

2. Yoyote aliyekuwa anafanya nukuu ya mwanzo nina wasiwasi alichokuwa anashushiwa hakukielewa vizuri (imagine tu Malaika apewe shughuli ya kumueleze mchunga kondoonBethlehem jinsi ulimwengu ulivyoumbwa na unafanya kazi kama vile anaongea na Albert Einstein au Isaac Newton, yaani lazima muingizwe chaka, unakuta mazungumzo ya dakika 60 inabidi ayasimulie kwa dakika moja )
 
Kwanza jua kwenye Biblia umeachiwa vitu vichache sana kwa ufahamu wa wengi ukifika level za juu za ufahamu kwenye dini utajua siri nyingi.
Hakuna siri yoyote kwenye Biblia zaidi ya hadithi za uongo njoo utamu kolea.

Baada ya kuona kwamba hadithi za Biblia hazi make sense, Wakaunda dhana uchwara kwamba lazima uwe na imani ya juu au uelewa wa roho mtakatifu kuielewa Biblia.

Kumbe ni ujinga tu.

Biblia ni hekaya kama zilivyo hekaya za Abunuwasi, Esopo, kalume kenge na Alfu lela ulela.
 
Biblia katika kitabu cha Mwanzo 1:2 inaeleza

Mwanzo 1
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Katika mstari huu kuna vitu vya kujiuliza ambavyo Natumai wajuzi wa haya mambo mtanisaidia?
1. Kwanini nchi ilikuwa ukiwa tena utupu?
2. Kwanini nchi ilizingirwa au jazba na maji?
3. Kwanini giza lilitanda juu ya uso wa vilindi vya maji?
4. Kwanini Roho wa Mungu alitulia juu ya uso wa maji?

Nakaribisha mawazo huru tuweze kutengana wana JF.

Please huu sio uzi wa kidini.
NITAJARIBU HOJA MOJA PEKEE;

WATAFITI NA WANA THEOLOJIA;
Mara nyingi katika kuyachimba maandiko na kutafiti nyakati za biblia, wamefanya tafiti mbalimbali ili kujiridhisha majira na nyakati ambazo vitabu mbalimbali katika biblia kuwa viliandikwa nyakati gani katika historia.

Katika utafiti huo, kitabu cha AYUBU kimewapa wakati mgumu kujua kuwa Ayubu kuwa;
  • Aliishi nyakati gani?
  • Nchi ya Usi alikoishi Ayubu ilipatikana wapi?

Kwa kukosa majibu ya maswali hayo, hawa watafiti wa maandiko wengi wao wamejaribu kwenda mbali zaidi na kuamini;
-Huenda kulikuwa na dunia au maishi mengine kabla ya sasa
- Huenda Mungu aliiangamiza dunia ya kale kabla ya hii mpya ambayo labda nchi ya Usi alipoishi Ayubu ilipatikana.

Note;
Huu ukiwa wa dunia unaoongelewa Mwanzo 1.2 huenda umetokana na kutoweshwa kwa viumbe wa dunia ya Mwanzo.

Note; nilisema najaribu
 
Back
Top Bottom