Mangi Meno
JF-Expert Member
- Jun 26, 2024
- 292
- 895
- Thread starter
- #61
Ni sawa umri wa dunia inaweza kuwa miaka hiyo ila uwepo wa sisi Binadamu wa sasa kwa kulingana na uumbaji wa Pili inaweza ikawa miaka 6000 Plus.Hapa na kupinga kuna sehemu unashindwa kuelewa.
Umri wa dunia unakadiriwa kuwa takriban bilioni 4.54 (4,540,000,000) miaka. Makadirio haya yanatokana na uchunguzi wa miamba ya zamani duniani na vipimo vya isotopu za elementi kama uranium na lead. Pia, wanasayansi hutumia vipimo vya miamba ya anga kama meteorite ili kusaidia kuthibitisha umri huu.
Ukisoma Biblia katika
Mwanzo 1
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Hapa haionyeshi wala kusema ni lini. Haina "time frame " kwahiyo inawezekana ndio hiyo miaka kwani wanasayansi pia wanapima na miamba na kiukweli kwenye uumbaji kwa kufuata Biblia Mungu hakuumba nchi kavu ila aliyakusanya maji sehemu moja na nchi kavu ikaonekana ikiwemo na hiyo miamba.
Binafsi naungana na matokeo ya kisayansi kuhusu umri wa dunia.