Hoja kwa Gwajima: Barabara ya Tegeta Nyuki hadi Baobab Sekondari huisemei na utatudai kura 2025? Tukutane 2025 Mchungaji

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Mchungaji Gwajima hii barabara ni muhimu sana. Tumeshaisemea sana SISI WANANCHI WA jimbo la Kawe hasa tunaoishi huku Bunju.

Asubuhi inakuwa kero sana kufika mjini ila sasa wizara ya Ujenzi imeleta bajeti yake hatukuoni ukiitetea ili tupate double lane muendelezo wa iliyoishia njiapanda ya Tegeta Nyuki.

Mzee baba fanya uwaambie Wizara tunahitaji double lane hapa, tunaopanga kukupinga 2025 hii tutaitumia kama pointi ya kukuchallenge.

Act accordingly Mheshimiwa.
 
Wewe unataka isemewe au ijengwe?

Waambie wananchi wenzako mdai ujenzi wa barabara yenu moja kwa moja serikalini na siyo kuwahimiza wenzako kudai "maneno ya mbunge" kwa sbb yana little impacts ya mkitakacho.

Wapo viongozi wengi tu wa serikali tu ktk maeneo yenu mf. DC, MED, Meneja TARURA, Meneja TANROAD, Rais ama waziri ambao ndio watendaji na siyo watu wa maneno. Wadaini hao mtakacho na siyo mbunge.

Ni ujinga kudhani kuwa kelele tu za mbunge zinaweza kuwapeni barabara unless muwe hamjui serikali inafanya vipi kazi zake.

Mwisho, kumbuka kuwa, ni wajibu wa serikali kutoa huduma za kijamii ikiwemo barabara, elimu/shule, afya nk nk kwa wananchi wake wa kila eneo bila kujali eneo hilo lina mbunge au halina; AMESEMA au HAJASEMA ; lina diwani au halina; AMESEMA au HAJASEMA.
 
Uliona wap Awamu hii wakijenga Barabara? Hawajajenga hata 1km, WANAKOPA Ili kujenga vyoo na madarasa ya shule, WANAKOPA kufidia ONGEZEKO la Bei za mafuta.

Mtapata mwakilishi mwingine muda ukifika, Huyo atapewa KAZI KUBWA zaidi ya hiyo Ili asimamie KAMPUNI yote. Amen
 
Awamu hii tumepigwa
 
Katika kosa alilofanya mzee wa msoga ni kutotengeneza double road ya tegeta nyuki baobab. Yaani siku nyingine tuteue wanaokaa bunju au mbweni huyu anayekaa salasala hatufai kitu.
 
Mchungaji Gwajima hii barabara ni muhimu sana. Tumeshaisemea sana SISI WANANCHI WA jimbo la Kawe hasa tunaoishi huku Bunju.

Asubuhi inakuwa kero sana kufika mjini ila sasa wizara ya Ujenzi imeleta bajeti yake hatukuoni ukiitetea ili tupate double lane muendelezo wa iliyoishia njiapanda ya Tegeta Nyuki.

Mzee baba fanya uwaambie Wizara tunahitaji double lane hapa, tunaopanga kukupinga 2025 hii tutaitumia kama pointi ya kukuchallenge.

Act accordingly Mheshimiwa.
Kweli kabisa, tumechoka na foleni. Watu potential wa nchi hii wote wapo Tegeta, Boko, Ununio, Mbweni, Bunju na bagamoyo kazi kuwasha vingora kukwepa mnyororo! Mabasi ya mikoani yanapitishwa huku alafu barabara finyu!

Sasa ina maana gani mnajenga njia nane huko kimara alafu mnahamishia matatizo bagamoyo Road? Siku hizi foleni zipo Bunju na hakuna dalili za kupanua barabara.
 
Watu potential una maana gani?

Watu potential ni wakulima na wafugaji ambao wala hawakai dar

Naomba tuendelee kuzalisha mali na tusiyumbishwe na hao wachuuzi wa hapo mzizima
 
Kweli kabisa, tumechoka na foleni. Watu potential wa nchi hii wote wapo Tegeta, Boko, Ununio, Mbweni, Bunju na bagamoyo kazi kuwasha vingora kukwepa mnyororo! Mabasi ya mikoani yanapitishwa huku alafu barabara finyu!

Sasa ina maana gani mnajenga njia nane huko kimara alafu mnahamishia matatizo bagamoyo Road? Siku hizi foleni zipo Bunju na hakuna dalili za kupanua barabara.
Bunju ni mkoa wa Pwani
 
Watu muhimu wa nchi hii tupo, oysterbay, masaki, msasani, mikocheni na mbezi beach, huko kwingine ni kwenye mashamba yetu
 
Kabisa yaani watu wazito sana wapo barabara hii wenzetu wao wanapita na ving'ola tu ila kina sie tupo tunakomaa na foleni sana asubuhi na jioni tunapoteza muda sana road kuanzia pale Nyuki ...
 
Watu muhimu wa nchi hii tupo, oysterbay, masaki, msasani, mikocheni na mbezi beach, huko kwingine ni kwenye mashamba yetu
Ilikuwa zamani huko unakokutaja walikuwa watu muhimu za kizazi cha kwanza. Kizazi cha viongozi wa nchi hii wengi hapa dar kwa sasa kimejenga Bunju, Mabwepande, Mbweni nk ukitaka kuelewa nenda kwenye eneo la makazi la Mbweni Oysterbay na Masaki hazioni ndani watu wamefumua vitu vikali na kuna paved streets saafi ila barabara kuu tatizo...Huku kuna Makatibu Wakuu, Wakuu wa Majeshi, Rais, Watoto wa Marais, Wabunge wengi, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makao ya vyombo vya ulinzi na usalama nk
 
Mkuu The Palm Beach ndiyo maana ya kuwa na mbunge as mwakilishi wenu, siyo kila mtaa mnakusanyika na kuanza kutembea na mabango kuomba gari la uchafu nk.
Ndugu TODAYS;
Haiko hivyo. Na bahati mbaya na wewe huyafahamu mambo haya na hata hukuielewa hoja yangu..

Theoritically iko hivyo. Lakini practically Kwa mfumo wa utawala wa nchi yetu, yaani demokrasia ya uwakilishi (representative democracy) haifanyi kazi ingalau hata kwa 10% tu..!

Tanzania specific, yenye "Imperial presidential system" ndiyo tatizo zaidi, kwa sababu Rais ndiye kila kitu na kamwe hadhibitiwi na taasisi nyingine yoyote si bunge wala mahakama...!

Ukitaka kuthibitisha hili, muulize mbunge wa Mbulu Mh. Flatei Massay ambaye kwa miaka zaidi kumi anapiga kelele barabara fulani ya jimbo lake ijengwe lakini hakuna aliyemsikia..!

Why?

Bunge haliamui chochote. Lipo kinadharia. Na practically haliwezi kumfanya lolote Rais na wasaidizi wake unless ameamua yeye kuwa..!
 
Back
Top Bottom