Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 2,375
- 4,784
Kwasababu huyu wajina wangu Majaliwa katupatia hoja mezani, lazima tuijadili, kwa akili za wazi kabisa
Nchi yetu sasa ina watu kama milioni 70 ambao asilimia 50 (Milioni 35) wana umri chini ya miaka 24, na Milioni 8 kati ya hao ni vijana wa miaka 15 mpaka 24.
Soma Pia: Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri
Kwa mifumo yetu ya elimu, vijana wengi sana wanaanguka na wameanguka ndani mfumo wa elimu zetu za secondari; kwa idadi yao inaweza kuwa ni milioni kadhaa achana na hawa graduates ambao hawapo kwenye ajira ambao sidhani kama wanafika 500,000
Maana yake ni nini, shida kubwa ya kukosekana kwa skills ipo kwa hawa watu ambao hawajafika chuo kabisa na ndio wengi kabisa nchi hii, ni bomu ambalo halizungumzwi, na hawana mtu wa kuwatetea kwakuwa wamesahaulika.
Maarifa ya VETA, kwenye kozi fupi fupi kama upishi, ufundi umeme, kuoka mikate, saluni, ufundi cherehani etc etc ni skills ambazo zinadharaulika sana lakini kwa aina ya uchumi wetu hizo ndo zitakomboa vijana wa taifa hili, hawa milioni zaidi ya 8 wasio na degree
Na kwanini nasema hivi, ni kwasababu ni shughuli ambazo moja kwa moja zinazalisha mali na kuongeza thamani, na hicho ndicho kinachotakiwa kwenye uchumi wetu.
Na hata sio dhambi ikiwa na graduates watajisikia kwenda VETA, kwa wastani wa hii nchi na sisi ambao tumepitia huu mfumo, mimi ilinichukua karibu miaka 2 kuja kuingia kwenye mfumo wa ajira, maana yake wala hakuna kisingizio cha kwenda kujifunza upishi wa keki kwa miezi sita na kufungua bakery yako ukiapply ujuzi wa degree yako ku attract funding, expanding and creates more jobs.
Ni akili tu za watu wajinga kudhani kwamba kumshauri graduate kwenda VETA ni ushauri mbovu.
Ambacho kinapaswa kuwa hoja mezani, ni, serikali ije na plan kama zilivyo zile JKT program, iangalia tu namna ya kuanza kutekeleza hichi kitu.
Kunaweza kuwa na options ya cost-sharing, serikali igharamie mafunzo na chakula cha bei nafuu, na wahitaji vijana wajigharamie nauli. Inaweza kuwa program ya gharama, lakini inaweza kuwa gharama sana kukaa na jeshi la watu milino 8, vijana wenye nguvu, halafu hawana kazi na ujuzi.
Hoja ya Majaliwa iwekewe tu mbolea. Na sio kwamba tuwalazimishe waende, bali washauriwe kwenda.